Naomba msaada wa TENDE misikiti ya Rufiji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba msaada wa TENDE misikiti ya Rufiji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by HM Hafif, Aug 23, 2009.

 1. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Assalamu alaykum.

  Kwa waislamu wanaoweza kutoa msaada wa tende ili tutoe kwa waislamu wenzetu wa wilaya ya Rufiji, kuanzia jaribu mpakani, Bungu, Kibiti, Ikwiriri, Nyamwage, Chumbe mpaka Muhoro. na huku kuelekea mpaka nyamisati na salali, mpombwe, bila kusahau mkongo, kilimani, kipo ,mwaseni mpaka Nyaminywili.

  Huko hali mbaya sana.
  Tunaomba msaada.
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  .

  hakika nazifahamu vizuri sehemu hizo, nilikuwa napita kwenda kuwinda Selou na Kingupira. kuna jama zangu pale Mkongo, Utete diwani na Ikwiriri na Mohoro.

  Ok all in all, tuwasiliane kwenye mail na ubainishe unahitaji kiasi gani cha Tende tuangalie uwezekano.

  Nakuomba sana usije ukatumia msaada huo kwa madhumuni ya kisiasa.

  Dr Hamza Yousuf Al Naamani.
  Doha
   
 3. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dr hamza,
  nimeshukuru kwa reply yako. Nimekutumia namba yangu ya simu ili tuweze fanikisha mambo haya haraka iwezekanavyo.

  natanguliza shukurani. karibu sana Ikwiriri

  hakika Allah atakulipa .
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nashukuru nimeipata Insh'Allah nitakupigia jioni baada ya magh'ribi.

  swaumu njema
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Aug 23, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,021
  Trophy Points: 280
  ..siyo mnapeleka tende wakati wa Ramadhani halafu mnatokomea hadi Ramadhani nyingine.

  ..wananchi wa Rufiji na mikoa ya kusini kwa ujumla wanahitaji msaada mkubwa ktk masuala ELIMU.

  ..wasaidieni ktk kuboresha mazingira ya elimu pia.
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  hivi kweli tende ndio kitu cha kuomba na kusisitiza kwamba huko hali ni mbaya, hivi watu wanafungia tende au, hii msg au ombi halina maana na linadhalilisha uislamu
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Aug 23, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,021
  Trophy Points: 280
  ..kipindi hiki kitumike kugawa tende pamoja na vitabu vya masomo kama hisabati.

  ..kipindi hiki yafanyike mashindano ya kusoma Quran, na mashindano ya hisabati na chemsha bongo, uandishi wa insha na utunzi wa mashairi, Kaswida etc.

  ..HII NI KARNE YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA.
   
 8. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mkuu....aisee kweli kabisa..na hiyo elimu sio madrassa kwa saaana...
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  nafikiri Tanzania kuna sera maalum za Ilmu na wengi tunachangia hilo kupitia TEA, na halmashauri.

  lakini suala la njaa halina mbadala. Ndio maana ukisoma magazeti ya leo ya huko Tanzania unaelezwa rais JK katembelea Longido kujionea hali ya Ukame.

  Hakika vyote ni muhimu. kama waislam tuna wajibu mkubwa sana kuhakikisha kuwa Mwezi huu mtukufu wa ramadhani watu wote tunapata futari iwe tajiri au maskini.

  Hiyo ni sera ya dini , ndio maana unaona walionacho wanatoa kwa wasionacho ili wote wafunge kwa furaha.

  HM Hafif, tueleze bayana unahitaji kiasi gani? tupe data kamili.

  Dr Hamza
   
 10. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  maneno yako Kuntu. Sisi Rufiji tuna UMAKURU ( Umoja wa maendeleo ya kujitolea Rufiji) Chini ya Uenyekiti wa Col Matope, na Prof Idrisa Mtulia, Idi Simba na wengine.hawa wanashughulikia mambo yote ya Elimu na mengineyo.

  Sisi wengine ni wachangiaji wakubwa wa Elimu huko. Suala la Futari ni nyeti sana hususan mwezi huu. kwani mwezi huu utokea mara moja tu katika mwaka.

  mahitaji yetu ni kama katuni 100 hivi za tende za kilo 20 each. hapo tutaweza kutoa swadaka kwa misikiti mingi sana huku.

  lakini Dokta Hamza kama itapatikana ziada haitakuwa mbaya tutawapa waislam wengine wa jirani kama kilwa na mkuranga.

  nakupigia simu naona upokei najua labda una swali. tuwasiliane dokta
   
 11. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #11
  Aug 25, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  As discussed in the phone. wasiliana na Islam kesho atakupa kila kitu.

  Nimefurahi sana kusikia Col Mzee matope, Huyu bint yake Fatma matope alisoma na mke wangu jangwani sec na zanaki high sch. Bint alikuwa rafiki sana wa mke wangu na alikuwa na akili sana darsani. Prof Idrisu Mtulia yeye ni jirani yangu sana pale Upanga. yeye yupo mazengo mimi Alikhan.

  Nilipata kusikia kidogo kuhusu hii UMAKURU kupitia balozi wa Tanzania nchini saudi Arabiya jaji Hamisi Msumi.
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Aug 25, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu kipindi hiki cha toba Tende ni muhimu sana tena mno.
   
 13. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dokta Hamza na Mkeo na Familia yenu, napenda kutoa shukrani zangu za dhati, mzigo nimepata katuni 117 za tende aina ya hanees jioni ya leo ila tu nilikuwa sikuwa na usafiri wa kuzichukua. Namshukuru pia Sheikh Islam yeye anatoa usafiri wa kuzipeleka mpaka Ikwiriri kisha mimi nitazisambaza.

  Kwa Kweli Allah atawalipa zaidi na zaidi sheikh.

  Shukrani sana sana
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Aug 26, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  hebu fanya harambee ya maana bana,wasaidiwe kwa kusomesha watoto wao na sio kuwapa tende,
   
 15. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #15
  Aug 26, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kweli hiki ni kipindi kigumu sana kwa Waislam ambao ni maskini hakika wanateseka sana,
  Wanaitaji kusaidiwa juzi nilikuwa Tilapia nikaona jamaa wamekuja kubalizi na kula vitu nikajiuliza kwa wale wenye kipato cha chini inakuwaje maana muda wakutoka kazini unapungua mahitaji yanaongezeka na matumizi na pia mwili unakuwa hauna nguvu kutokana na kushinda njaa.

  Miogo ipo juu viazi kila kitu kiko juu Kwakweli wenye uwezo wawasaidie hawa ndugu zetu.

  Poleni sana kwa hiki kipindi
   
 16. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #16
  Aug 26, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Hivi lazima mgeze hata kula matunda ya kiarabu? Au ndio usilamu kusujudu uarabu?

  Tanzania imejaa matunda kede kede, lakini hawa jamaa lazima waweke umanga. Sasa wanombana tende kwenye mtandao. Huko rufiji kumejaa mabibo, kule hayo.

  Hii si dini ya wote bali inaonyesha kwa hali kubwa sana kuwa ni ya waarabu.

  Kaazi kweli kweli
   
 17. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #17
  Aug 27, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  waafrika especially wa waTz wana pombe zao za asli kama mbege, dengerua, ulaka, tembo, ulanzi, chimpumu,lubisi nk. sasa vipi kule kanisani wanapewa DIVAI ambayo ni ya kizungu.
  Hii si dini ya wote bali inaonyesha kwa hali kubwa sana kuwa ni ya wazungu.
  kazi kweli kweli
   
 18. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #18
  Aug 27, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  .

  Mashuur ya Hafif,
  Naelewa sana wagalatia inawauma sana kupewa huu msaada wa Tende. lakini hata ikiwauma lakini lengo letu limefanikiwa watu wapate futari nzuri wakati huu ramadhani.

  unajuwa sana mwezi wa ramadhani watu wanapoteza sana nguvu hivyo wanapofungua wanahitaji glucose kwa wingi sana kurejesha nguvu. sasa kwenye tende unapata glucose kwa wingi sana.

  hata mkichukia lakini watu watakula tende.
   
 19. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #19
  Aug 27, 2009
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa waislamu wanaoweza kutoa .....jamani ambao si waislamu hawawezi kujumuika?samahani kama nimewakwaza.
   
 20. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #20
  Aug 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Kwenye Biblia imeandikwa (Luka 22:18) kuwa divai itakayotumika kwenye misa au ibada inatakiwa iwe ni mvinyo unaotokana na "tunda la mzabibu". Isitoshe Divai ni sehemu ya ibada kwenye Ukristo.

  Jee, kula tende ni sehemu ya ibada ya Kiislamu? Wapi kwenye Kurani imeandikwa Waislamu wanatakiwa kula tende pamoja na futari?
   
Loading...