Naomba msaada jinsi ya kuandika barua

Naomba msaada jinsi ya kuandika barua

Niomi kaka

Member
Joined
Feb 28, 2025
Posts
66
Reaction score
131
Habari za mchana wakubwa,

Naomba kama kuna mtu ambae amesha Wahi kupata changamoto kama niliyo kutana nayo mimi anisaidie, kwa kifupi ni kwamba mimi Niko nchii jirani ya Zambia. Sasa kuna mdogo wangu alitaka kuja kunitembelea

Baada ya kukamilisha taratibu zote za kupata hati ya kusafiria huko mkoani kwetu amesafiri ili aje kuvukia mpakani Tunduma pale. Lakini chakushangaza uhamiaji upande wa Tanzania wame mzuwia na kushikilia hati yake ya kusafiria eti kwa sababu yuko chini ya umri wa miaka 18. Kwamba kunahitajika barua kutoka kwa wazazi, nakala za vitamburisho vyao vya taifa, na barua kutoka kwangu,

Sasa hapa nimebaki njia panda kwa sababu sijawahi kukutana na changamoto kama hii na sijui na iandikaje, kwahiyo naombeni wazoefu mnisaidie
 
wazazi waandike consent letter (waelezeee wanafahamu hiyo safari na wamemruhusu dogo kusafiri na wanakufahamu) wewe uandike barua ainisha uhusiano wako na yeye na kama umemuita na utawajibika kwa kila kitu kuanzia kula kulala kuvaa na kila kitu pindi atakapokua huko (invitation letter)
 
asante
 
maoni yako ni muhimu kwangu,
naomba nielekezwe hata kwa mfano
 
maoni yako ni muhimu kwangu,
naomba nielekezwe hata kwa mfano
Copy ulichoandika hapa, paste chatgpt ikupe mfano wa barua ya utambulisho .

Kwa kifupi ni barua kama barua za kazi tu, wala haihitaji maelezo marefu zaidi ya mzazi kujitambulisha, kukiri kuitambua safari na kukutambua wewe na malengo yampelekayo mwanae kwako.
 
Back
Top Bottom