Naomba mnishauri kuhusiana na huyu dada yangu mkubwa

Perry

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
10,082
Reaction score
2,354
Mambo wakuu?
Nina dada yangu mkubwa ana umri kama 38yrs hivi,sasa huyu dada alikua anaishi na mwanaume wake ila hawakua wamefunga ndoa,wameishi kama miaka 8 kama sikosei.wamebahatika kupata watoto watatu mpaka sasa, mumewe ni muajiriwa kwenye shirika flani kubwa tu hapa nchini,dada yangu yeye hana kazi yoyote ni mtu wa kubangaiza tu na kuuza nguo online kwa kifupi ni mama wa nyumbani tu.
Week mbili zilizopita waligombana na huyo mumewe, dada kwa maelezo yake anasema huyo mumewe alimfukuza nyumbani kwake usiku ule pamoja na watoto wake,ila kwa uchunguzi nilioufanya mumewe hakumfukuza ila ni yeye tu aliamua kukimbilia kwa ndugu yetu mwingine na watoto wake usiku ule.
Kilichonifanya nije kuomba ushauri humu ni hiki,kuna ndugu naona kama wamemshauri dada vibaya sana,kuna nyumba yetu ya urithi tuliachiwa na marehemu wazazi wetu,ndugu wamemshauri dada aondoke mazima kwa mumewe arudi pale nyumbani kwenye nyumba ya urithi akae,kweli dada nae akachukua huo ushauri wa ndugu kaenda kwa mumewe kabeba vitu karudi nyumbani na mzigo wa watoto watatu,yule mumewe kule mpaka leo hajampigia simu yeyote nyumbani kumueleza nini tatizo yuko kimya tu,dada yeye anasema amechoka manyanyaso,sasa nimeshindwa kumuelewa dada kama nilivyosema hana kazi yoyote ni anauza tu vinguo online,ana watoto watatu wawili kati yao wanasoma shule za English medium.huko napo nasikia bwana alimuambia kama ameamua kuondoka nyumbani na watoto wake basi asikae amtafute kwa lolote lile na hao watoto amempa yeye kama zawadi.
Dada hakua na maisha yoyote magumu kwa mume wake kwani shemeji alikua anajitahidi sana kujali familia yake.
Wasiwasi wangu ni kwamba,huenda dada akaanza kuishi maisha ya shida kwa kujitakia mwenyewe na akawa msalaba kwetu sisi,kwanza kitendo cha ndugu hawa kumshauri arudi nyumbani pasipokuangalia mustakabali wake na watoto wake naona ni janga,hapa ni week ya pili tu lkn ameshaanza usumbufu wa vizinga.nawaza ada za hao watoto wa English medium atatoa wapi?

Wakuu huenda mwandiko wangu ni mmbaya but tuvumiliane.
Naomba mnishauri nifanyeje huyu mtu arudi kwa mumewe huko kwani kama nilivyoeleza soon anaenda kuwa msalaba kwetu huyu au kama kuna ushauri mwingine naukaribisha.
 
Jaribuni kumdadisi kwa kına usikute kuna masaibu mazito ambayo hua anayapitia kwa mume wake huyo.

Yeye sio mjinga wa kiwango cha kuamua kutoka kwenye mji wake kWa namna hiyo kama kweli alikua anaishi vizuri kwa mume wake.
 
Akili za wanawake ni finyu sanaa kuna haja ya kusimamiwa na ndungu wakiume kufanya maamuzi sahihi, na kuakikishia huyu mme wake atakuja kupigia mzigo humo humo kwenye nyumba ya urithi, na ata mzalisha tena bila gharama kubwa tena.
Na kushauri kama unauwezo husisikilize nini paleka gari lako upakie kila chake umrudishe kwa mme wake majadiliano ya kuachana au kuvumiliana muafanyie huko huko kwa mme, mzigo wa kulea watoto sio mchezo mkuu........
 
Jaribuni kumdadisi kwa kına usikute kuna masaibu mazito ambayo hua anayapitia kwa mume wake huyo.

Yeye sio mjinga wa kiwango cha kuamua kutoka kwenye mji wake kWa namna hiyo kama kweli alikua anaishi vizuri kwa mume wake.
Hata km, bas afuate taratibu za ndoa, ili huyo mumewe aweze kuwajibika nae, sasa kuondoka holela huoni anakua mzigo kwa ndugu? Watoto wateseke akati baba yao yupo na uwezo wa kuwatunza anao? Waachane wao wazazi, watoto wapate stahiki zao km kawaida.
 
Dada hakua na maisha yoyote magumu kwa mume wake kwani shemeji alikua anajitahidi sana kujali familia yake.
Wasiwasi wangu ni kwamba,huenda dada akaanza kuishi maisha ya shida kwa kujitakia mwenyewe na akawa msalaba kwetu sisi,kwanza kitendo cha ndugu hawa kumshauri arudi nyumbani pasipokuangalia mustakabali wake na watoto wake naona ni janga,hapa ni week ya pili tu lkn ameshaanza usumbufu wa vizinga.nawaza ada za hao watoto wa English medium atatoa wapi?
Naomba nijazie hapa !!!!

DHANA YA NDOA (Presumption of Marriage)

Je, Nini maana ya dhana ya ndoa?.

Dhana ya Ndoa ni ile hali ambayo watu huitwa wanandoa kwa kuwa wameishi pamoja kama mume na mke kwa kipindi cha miaka miwili na kuendelea.Wanawake wengi wamekuwa wakiaminishwa vibaya kuwa akikaa na mwanaume kwa miezi 6 tu basi hapo mwanamke anatambulika kama mke halali wa huyo mwanaume, jambo hili si sahihi, sababu sheria inatambua kipindi cha miaka miwili (2) mfululizo kuishi kama mke na mume, hapo ndipo dhana ya ndoa hutambulika.

Dhana ya ndoa humalizikaje? Je nayo huombewa talaka?

HAPANA, dhana ya ndoa huvunjwa na mahakama kwa kutolewa kwa amri ya kubatilisha dhana hiyo (decree of annulment) na sio talaka. Talaka hutolewa kwa wanandoa rasmi tu.
Vipi kuhusu mali na mgawanyo wa watoto waliopatikana katika dhana ya ndoa?
Mgawanyo wa mali, na uangalizi wa watoto pamoja na matunzo yao hufanyika kwa kuzingatia mambo yaleyale yanayozingatiwa wakati wa utoaji wa talaka.
 
Kukosa ajira/kipato Kwa Dada yenu kisiwe kigezo cha yeye kunyanyaswa Kwa namna yeyote na huyo mumewe/Mzazi mwenzie

Kuna taratibu za kufuata ili mumewe/Mzazi mwenzie aendelee kuhudumia familia yake/watoto

Mwambie azifuate hizo

Mnaweza kumlazimisha aendelee kuishi na huyo mumewe/Mzazi mwenzie mkaja kukuta ndugu yenu ameuawa
 
Kwani umemuuliza wewe binafsi akakwambia nini kimejiri?? Ushauri wangu, mfuate dada yako, muulize na mwambia asikufiche hata chembe juu ya nini kimejiri baada ya kupata ABC zake ndio uje hapa tushauri kama utashindwa peke yako. Binafsi naogopa kushauri bila kujua shiida nini maana ndoa zinamengi na ni Kati ya watu wawili.
 
Mkuu hebu jaribu kujiuliza kama mtu mwenye akili timamu kama yeye na mme wake walikuwa wanaishi vizuri kwanini dada yako ameamua kurudi nyumbani? Kuna uwezekano mkubwa huyo shemeji yako ana matatizo ambayo nyie bado hamjayajua.

Halafu inakuwaje huyo shemeji yako agome kuwalipia watoto wake ada kisa amegombana na mke wake? Hili pekee linaonyesha huyo jamaa ana matatizo.
 
Kukosa ajira/kipato Kwa Dada yenu kisiwe kigezo cha yeye kunyanyaswa Kwa namna yeyote na huyo mumewe/Mzazi mwenzie

Kuna taratibu za kufuata ili mumewe/Mzazi mwenzie aendelee kuhudumia familia yake/watoto

Mwambie azifuate hizo

Mnaweza kumlazimisha aendelee kuishi na huyo mumewe/Mzazi mwenzie mkaja kukuta ndugu yenu ameuawa
Amewekwa chini akaulizwa changamoto zinazomkabili kwa mumewe binafsi nimeona ni za kawaida tu kwa wanandoa.
1.Mume anamgombeza sana tena mbele za watoto na dada wa kazi.
2.mume anaweza akamkasirikia hata mwezi mzima kwa kosa dogo tu.
3.sijui mume mkali sana.
4.mume kamwambia asifanye shughuli yoyote akae nyumbani tu.
5.Recently ndio mume kaanza pia kumpiga.
Kwackifupi me sijaona zito la kukimbia hapo.
 
Mambo wakuu?
Nina dada yangu mkubwa ana umri kama 38yrs hivi,sasa huyu dada alikua anaishi na mwanaume wake ila hawakua wamefunga ndoa,wameishi kama miaka 8 kama sikosei.wamebahatika kupata watoto watatu mpaka sasa, mumewe ni muajiriwa kwenye shirika flani kubwa tu hapa nchini,dada yangu yeye hana kazi yoyote ni mtu wa kubangaiza tu na kuuza nguo online kwa kifupi ni mama wa nyumbani tu.
Week mbili zilizopita waligombana na huyo mumewe, dada kwa maelezo yake anasema huyo mumewe alimfukuza nyumbani kwake usiku ule pamoja na watoto wake,ila kwa uchunguzi nilioufanya mumewe hakumfukuza ila ni yeye tu aliamua kukimbilia kwa ndugu yetu mwingine na watoto wake usiku ule.
Kilichonifanya nije kuomba ushauri humu ni hiki,kuna ndugu naona kama wamemshauri dada vibaya sana,kuna nyumba yetu ya urithi tuliachiwa na marehemu wazazi wetu,ndugu wamemshauri dada aondoke mazima kwa mumewe arudi pale nyumbani kwenye nyumba ya urithi akae,kweli dada nae akachukua huo ushauri wa ndugu kaenda kwa mumewe kabeba vitu karudi nyumbani na mzigo wa watoto watatu,yule mumewe kule mpaka leo hajampigia simu yeyote nyumbani kumueleza nini tatizo yuko kimya tu,dada yeye anasema amechoka manyanyaso,sasa nimeshindwa kumuelewa dada kama nilivyosema hana kazi yoyote ni anauza tu vinguo online,ana watoto watatu wawili kati yao wanasoma shule za English medium.huko napo nasikia bwana alimuambia kama ameamua kuondoka nyumbani na watoto wake basi asikae amtafute kwa lolote lile na hao watoto amempa yeye kama zawadi.
Dada hakua na maisha yoyote magumu kwa mume wake kwani shemeji alikua anajitahidi sana kujali familia yake.
Wasiwasi wangu ni kwamba,huenda dada akaanza kuishi maisha ya shida kwa kujitakia mwenyewe na akawa msalaba kwetu sisi,kwanza kitendo cha ndugu hawa kumshauri arudi nyumbani pasipokuangalia mustakabali wake na watoto wake naona ni janga,hapa ni week ya pili tu lkn ameshaanza usumbufu wa vizinga.nawaza ada za hao watoto wa English medium atatoa wapi?

Wakuu huenda mwandiko wangu ni mmbaya but tuvumiliane.
Naomba mnishauri nifanyeje huyu mtu arudi kwa mumewe huko kwani kama nilivyoeleza soon anaenda kuwa msalaba kwetu huyu au kama kuna ushauri mwingine naukaribisha.
Mpuuzeni wala msihusike kwa jambo linalomhusu yeye wala kumuuliza. Kuweni wapenzi watizamaji tu.
 
Mkuu hebu jaribu kujiuliza kama mtu mwenye akili timamu kama yeye na mme wake walikuwa wanaishi vizuri kwanini dada yako ameamua kurudi nyumbani? Kuna uwezekano mkubwa huyo shemeji yako ana matatizo ambayo nyie bado hamjayajua.

Halafu inakuwaje huyo shemeji yako agome kuwalipia watoto wake ada kisa amegombana na mke wake? Hili pekee linaonyesha huyo jamaa ana matatizo.
Shem yeye anasema hawezi kuhudumia watoto ambao hawakai nyumbani kwake,kama Mama yao amewachukua that means wana baba yao mwingine.
 
Back
Top Bottom