Kwa maelezo haya sitakwenda Driving school, ni kuingia tu barabarani na kupambana na watumiaji wengine😁.Kwa mwanafunzi hii ni ajali kabisa
Atumie mguu mmoja kuendesha gari na si miguu yote
Kwa sababu hii miguu miwili huwa inawachanganya wanafunzi kwa sababu bado hawajakariri vizuri inapotakiwa breki badala ya breki hukanyaga mafuta na hiyo ndiyo ajali
Kwanza awe anajua pedel ya mafuta na ya breki ni ipi
Alafu kabla ya kuwasha gari lazima akanyage breki kwanza ndiyo awashe gari mguu uwe kwenye brake
Washa gari tia kirungu kwenye D alafu shusha handbrake anza kuachia brake ya mguu taratibu utaona gari inaanza kutembea toa mguu kwenye brake weka kwenye pedel ya mafuta kussuport mwendo
Lakini pedel ya mafuta siyo kama brake hii haihitaji nguvu yoyote kama brake
hii unagusisha tu mguu kidogo sana
Tumia mguu mmoja ukiona mwendo mkali unatoa mguu kwenye mafuta unakanyaga brake mguu huohuo mmoja mguu mwingine huwa hauna kazi kwenye gari hizi outo
Hakuna tofauti na gari, Tuanze na gari lenye manual gear yaani unabadili gia kwa kutumia vitu viwili mguu na mkono, mguu una kanyanga Klachi kwa mguu huku unabadilisha gia kwa utaratibu ufuataoNipe darasa mzee maana baiskeli naweza ila pikipiki Sina ujanja nayo
Ni kweli mkuu, tunaweka mizengwe mingi sana, lakini hili la udereva linahusu maisha ya watu kwa kiwango kikubwa sana.Tufanye research kutafuta chanzo cha ajali za barabarani....je, ni kweli nyingi zinasababishwa na madereva kutokujua kuendesha magari?
Kuna tofauti kati ya kutofuata sheria za barabarani na suala ninaloongelea hapa. And guess what muda mwingi ajali zinazopostiwa hapa ni za madereva wa STK ambao wamepita shule nzuri za udereva.
Hoja yangu ni kwamba tumefungwa kwenye mentality ya kikoloni ya kuamini kuweka vigezo vingi kwenye skills za kawaida ambazo ni basic kwa binadamu anayeishi mwaka 2025 ni muhimu.
Wakoloni walifanya kama njia ya kuendelea kututawala.
Mfano:
1. Upatilanaji wa passport
2. Leseni ya udereva
3. Leseni ya biashara
4. Mitihani shuleni
Kama hakuna bureaucracy basi Kuna siri kibao zisizojulikana vizuri na wananchi wengi. Hii yote ni wivu wa wanasiasa na watumishi wa umma.
Wanasema kwenye pikipiki Kuna kuvuta mafuta nkHakuna tofauti na gari, Tuanze na gari lenye manual gear yaani unabadili gia kwa kutumia vitu viwili mguu na mkono, mguu una kanyanga Klachi kwa mguu huku unabadilisha gia kwa utaratibu ufuatao
1. Hakikisha hand breki iko mahali pake imekaza,
2. Gia Iko kwenye neutral
3. Washa gari lako
4. Kanyanga Klachi ili uweze kubadili kwasababu Iko kwenye neutral iwe kwenye gia namba 1
5. Legeza hand breki na kuachilia Klachi pole pole na huku mguu wa kulia ukiwa kwenye accelerator pedal na yenyewe unakanya taratibu gari yako itaanza kutembea
6. Badili gia kwenda namba 2 Kwa kukanyaga Klachi utafanya hivyo huku unaongeza mafuta kwa kunyaga accelerator pedal
7. Ukitaka kusimama utapunguza Kwa kunyaga breki taratibu huku unabadili kwa change down toka labda 4 hadi 2 ndiyo utasimama
Kwenye pikipiki vivyo hivyo lakini Klachi mkono wa kushoto accelerator mkono wa kulia, gia unatumia mguu
Maswali tafadhali
Bila shaka alishafundishwa akafundishika.