Felix Aweda
JF-Expert Member
- Jun 23, 2012
- 507
- 145
Mimi ni mpenzi sana wa magari makubwa na pia ni dereva,mara nyingi nikipita hapa friends corner kushuka unga ltd hapa arusha naona scania nyingi lakini zimekufa za iliokua kampuni ya tango kwa kuziangalia inaonyesha zililetwa hapo zikiwa nzima,je huyu jamaa alipatwa na nini?
Tango Transport Ltd mmiliki wake ni Verani aka Kwaang Yame mtu wa Babati -MWIRAQ Tajiri sana hajawahi kutoke na kama uliona magari yake ushahidi unayo tatizo lake hajui kuwekeza ndo maana hana nyumba za kutosha. Yard ya unga Ltd alipewa na Nino Chalangi baada ya kumsaidia Nino katika kesi yake. Ana magari ya mafuta Dar. Yeye anamagari machache ya kutembelea na anaishi Uzunguni Arusha. Huyu jamaa aligombana na Nyerere miaka ya 60-miaka ya ujamaa na nationalization akilazimisha kununua ndege wakati hana uwanja.
Swala la magari kuwa pale wachangiaji wengi wamezungumza.
Kama unamwenyeji wa Manyara atakuambia histora yake.