Naomba kujua ubora wa Oppo na Xiaomi mi red 4.

umetumia simu za Huawei? naona battery zake zina capacity kubwa mpaka 5000mAh ila bila ushuhuda kwa heavy user hayo maandishi yanabakia mtandaoni tuu.
Huawei honor note 10 yenye 5000mAh na honor c8 nyenye 4000mAh?
Zingatia ukubwa wa betri pekee haufanyi simu kubwa inakaa ma moto sana ziko other factors zin support hilo mkuu.
 
Hakuna hatua moja matatizo ya Tecno ndio matatizo ya infinix na itel simu za kishamba sana
Mkuu unaweza kunisaidia definition ya Mshamba?maana Nimeshaona Watu wenye majumba mjini na Uwekezaji mzuri wanatumia Nokia za tochi na tecno,na nimeona wanaoishi kwa Shemeg zao wana cm Kali apple et al,.
Mshamba ni mtu wa namna gani?
 
Ile simu ni kati ya 400,000 na 450,000 bwana

Mm nlikuwa najua ni bei hiyo lkn bei nlioona pale nkaogopa...laki 4 ni reasonable price kwa simu hizi ikishazidi hapo huwa bora kununua simu ya kueleweka zaidi
 
Mkuu umeandika
-simu ya Oppo ambayo bado haipo sokoni, xiaomi ya kizamani sana na infinix ya karibuni.

1. Kwa simu za sasa maintanance ni kitendawili, majority ya hizo simu kubadili tu battery kunahitaji kupasha kioo moto na kukibandua. Si wachina mpaka brand kubwa.

2.kupata simu ndogo za 5inch napo pia ni kazi sana.

3. Simu nyingi za sasa utakazopata ni either zina notch ama zina kioo cha 18:9 ambacho ni kirefu sana kuliko upana.

Kwa Oppo kama ukaaji chaji ndio priority yako tafuta Oppo realme 2 ina decent soc ya snapdragon 450 battery kubwa la zaidi ya 4000mah na ram ya kutosha ya 4gb kwa multitasking
oppo-realme-2-3.jpg


Kwa xiaomi mi max series zinakaa sana na charge ila ni masimu makubwa sana sidhani kama yanafit udogo unaotaka.

Nikiangalia nje ya brand ulizotaja simu inayofit vitu vingi unavyotaka ni Sony xperia xz1 compact. Inakaa na chaji,processor kali ya mwaka jana, kioo cha 4.6 etc ila sio bei rahisi sababu ni flagship level ujiandae close to 1m.
 
Nakushauri nunua Oppo kwa uzoefu wa ninayoitumia (Oppo F5) ni simu nzuri sana. Uzuri wake unatokana na:
1. Mwonekano
Ina mwonekano mzuri wa kuvutia
Ni nyembamba na ina rangi nyeusi ya kung'aa isiyopauka wala kuchubuka kirahisi

2. Utunzaji chaji
Inakaa sana na chaji, kwa mfano mm sizimi data muda wote, kuichaji labda usiku naporejea nyumbani

3. Mtandao
Ni 4G (LTE) ; line mbili

4. Camera
Kama ww ni mtu wa picha bhasi umepata jawabu. Ina 20MP/16MP! Self vs Rear

5. Security
Ina mifumo mitatu ya utambuzi kwa finger, face na passcode

6. Spare na accessories
Ukweli mm bado sijapata changamoto kwa kuharibika. Ila nilipata changamoto kwenye kununua cover hadi kupata nilisota sana kwn hii cm nilinunulia Mombasa, Kenya. Jp kwa ss nimeambiwa na jamaa mmoja Kkoo, accessories zinapatkn lkn kwa bei ya juu kwn bado sio cm (model f5) nyingi sokoni hapa Tanzania

Mengine angalia screenshot naambatanishaView attachment 895380
Mkuu oppo ya laini 2 uliiipata wapi? Oppo nimeitumia tangu zimetoka nawapongeza kwa kutunza charge, camera, laini 1 lakini na 4G.
 
Back
Top Bottom