Je, umeshajua umuhimu wa processor kwenye simu yako na processor ipi ni bora zaidi?

TECNO Tanzania

Senior Member
Jul 6, 2016
192
216
Jina sahihi la processor zilizopo ndani ya simu ni CHIPSET kwa kifupi CHIP. Processor ni moja ya kitu ambacho huisaidia simu yako kufanya kazi kwa ufasini na ni kama ubongo au injini ya simu yako. Hiki ni Kichakataji chenye kasi zaidi kwenye simu na ni sehemu muhimu sana.

Katika simu yako unapofungua programu yoyote au kitu chochote, inachukua muda gani kufungua, hiyo yote inategemea processor. Kama processor yako ina kasi Zaidi inaipa simu yako wepesi wa kufanya kazi vizuri bila shaka na kwa kasi kubwa ya ajabu.

Je ni processor gani yenye kasi zaidi kwenye simu za mkononi?

Processor za Octacore ni aina ya processor ambazo huundwa na core nane(8). Mgawanyo wa core hugawanyika katika sehemu mbili mpaka tatu. Processor aina ya octacore zinaweza kugawanyika katika core zenye nguvu sana na core zenye nguvu ndogo. Mfano wa octacore processor ni MediaTek Helio G96 na simu za TECNO ndizo zinatumia Processor hizi za MediaTek Helio.

sa.png

TECNO CAMON 19 inatumia processor ya MediaTek Helio G96 ikiwa ni moja kati ya processor yenye nguvu zaidi na kuipa simu yako kuwa na uwezo wa kupangusa program kwa haraka (120Hz Refresh rate) na kwa upande wa SPARK 9 inatumia processor ya Media Tek Helio G85. Lakini pia toleo la Phantom X2 ambalo ni la hali ya juu litakuja na processor ya MediaTek Dimensity 9000 ambayo ni kubwa kuliko.

gd.jpg

Licha ya kuwa na processor bora, toleo hili la CAMON 19 lina sifa zingine nzuri ukilinganisha na matoleo ya simu zingine.

20230119-102626.jpg

Vivyo hivyo kwa SPARK 9, licha ya kuwa na processor nzuri, toleo hili la lina sifa zingine nzuri.

MediaTek Helio processor zimethibitshwa kuwa na ubora kwenye utendaji wa kazi wa simu. Ikiwa inasaidia simu yako isiwe nzito (Lagging Behind) na kuipa uwezo wa kufanya shughuli nyingi kwa wakati mmoja (multitasking), kucheza games kubwa bila kukwama au kuganda. Sasa jionee ubora wa simu zetu.
 
Yaani Xiaomi POCO M5, simu ya laki tatu na nusu inatumia MediaTek Helio G99 halfu we unakuja kuisifia Tecno yenye Helio G96?

Halafu maelezo yako yanaonesha kuwa hiyo ni miongoni mwa chipset zenye nguvu zaidi kwenye simu za mkononi utawadanganya wasiojua.

Unaziacha wapi Qualcomm Snapdragon 8 Gen 1, Snapdragon 8+ Gen 1, Snnapdragon 8 Gen 2, chipset ambazo TECNO hana hadhi ya kutumia?

Na hiyo Tecno Spark 9 ina 50MP lakini inavyopiga picha utafikiri 8MP
Hizo simu ni mbaya bwana. Watanunua watu ambao hawajali kuhusu simu.
 
Lipeni watu baki kuwaandikia makala za kiuchambuzi. Sasa wewe jina lako ni TECNO Tanzania halafu unaandika makala ya kusifia TECNO... umejifunza wapi marketing?
Hii sio makala ya uchambuzi ni makala ya kutoa elimu ndo maana hamna kampuni pinzani tulio ifanyia comparison wala kuishambulia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom