Naomba kujua tofauti Kati ya Ujasusi na Ugaidi

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,152
33,351
Wasalaam,
Naomba kujua tofauti Kati Ugaidi na Uajsusi,hasa kwenye vitendo.
Kwa mfano watu wa nchi moja wakie da nchi nyingine na kumuua mtu Fulani wa nchi nyingine,nchini kwake
ama akiwa nchi nyingine ambaee kimsingi hao wauaji wamemuona kua mtu huyo kweli Ni hatari kwa maslahi au Usalama wa nchi yao au raia wao.

Je kitendo hicho Ni kitendo Cha kijasusi ama kitendo Cha kigaidi?

Naomba tofauti Kati ya Ujasusi na Ugaidi.
 
Mifano Kama ifuatavyo (tafsiri hii sio rasmi 👇
Ugaidi- mwanajeshi kuhasi nchi, au kujaribu kupindua serikali.
Ujasusi- IT kuhuck taarifa za kiongozi,gvt n.k
Kumbuka ujasusi unaweza kipelekea ugaidi
 
Ugaidi ni uhalifu ujasusi ni upelelezi
Navyojua Mimi Wapelelezi Ni Askari hufanya kazi zao kwa usiri.
Kama wakibaini kwenye nchi jirani Kuna kambi inawasaidi kifedha kimafunzo na hifadhi ili baadae waje kuhujumu nchi yao au kuasi baadhi ya wananchi wa nchi ya hao Wapelelezi .
Kisha Wapelelezi hao wakaenda kuiteketeza kambi hiyo ya mafunzo na kuua watu wale na waalimu wao.
Je tukio Hilo Ni la kigaidi au kijasusi?
 
Jasusi ni mtu mtafuta habari kwa njia ya siri, habari ambazo huwa zinahitajika na kikundi flani, serikali au hata na kikundi cha kigaidi. (Hutafuta habari hizo kwa ajili mipango ya muda mfupi au mrefu)

Gaidi ni mtu ambae hutumia njia ya vitisho au vitendo vya fujo katika kuwakilisha madai yake.
 
Mara nyingi majasusi taarifa wanazozitafuta kwa udi na uvumba,hata wao wakikabidhi hawajui zinaenda kutumika wapi na nani?
 
Mara nyingi majasusi taarifa wanazozitafuta kwa udi na uvumba,hata wao wakikabidhi hawajui zinaenda kutumika wapi na nani?
Iko hivi kila agent mara nyingi huwa kuna agent aliyemtuma au huwa ni agent wa shirika linalojulikana.
Naweza kusema kuna agent wa mashirika. Hawa huwa wanajua wanachokifanya kwavile wanafanya kazi na mashirika hayo, mfano M15, KGB, CIA, NISS, MOSSAD, BND.

Pia kuna agent ambaye hutumika na agent (sio agent wa moja kwa moja) aidha toka kwenye mashirika yanayojulikana au hata mwenyewe asijue shirika analolifanyia kazi.
 
Wasalaam,
Naomba kujua tofauti Kati Ugaidi na Uajsusi,hasa kwenye vitendo.
Kwa mfano watu wa nchi moja wakie da nchi nyingine na kumuua mtu Fulani wa nchi nyingine,nchini kwake
ama akiwa nchi nyingine ambaee kimsingi hao wauaji wamemuona kua mtu huyo kweli Ni hatari kwa maslahi au Usalama wa nchi yao au raia wao.

Je kitendo hicho Ni kitendo Cha kijasusi ama kitendo Cha kigaidi?

Naomba tofauti Kati ya Ujasusi na Ugaidi.
Ugaidi ni uhuni ulio vuka level za kuwazingua washikaji mtaani hadi kufikia hatua za kuizingua nchi,

ujasusi ni umbea wenye manufaa
 
Ujasusi ni kitendo cha kitengo cha serikali au taifa kufanya upelelezi, utafiti, uchunguzi wa jambo fulani la kisiasa, kiuchumi, kiteknolojia au kijamii nje au ndani ya mipaka ya nchi husika kwa manufaa au matumizi ya nchi hiyo. Ujasusi unahusisha opereseheni mbalimbali za kuangamiza mfumo, mtu, miundombinu au kikundi hatarishi kwa maslahi ya nchi mmiliki wa kikundi cha ujasusi. Mataifa mengi yanamiliki na kugharimia vitengo vya kijasusi na vinatambulika kimataifa.

Ugaidi ni uwanaharakati wa kikundi cha watu wenye itikadi za kidini au kisiasa uliopitiliza, uliovuka mipaka ya matumizi ya nguvu ya hoja kufanya madai yao na kuamua kutumia nguvu ya silaha, vitisho, kuteka, kushambulia, kuua na hata kumiliki sehemu ya ardhi au nchi kwa lengo la kujitanua na kusambaza hoja na matakwa yao ndani na nje ya mipaka ya mataifa Ugaidi unapoanzia. Ugaidi ni uhalifu kimataifa ingawa baadhi ya nchi hufadhili ugaidi kwa kificho. Ugaidi huendeshwa kwa fedha haramu, za wizi au biashara haramu au za kificho na hata michango isiyo rasmi.
 
Ugaidi inategemea ni upande gani unatafsiri.
Upande unaoshambuliwa unaweza tafsiri waliowashambulia kama magaidi,ila upande unaoshambulia unaweza tafsiri kama wapigania uhuru/wapigania haki.
kwa mantiki hiyo,Mpelelezi anayekwenda kuua nchi nyingine,anaweza tafsiriwa kama gaidi(International terrorism) au lah,inategemea na aliyeshambuliwa atamuitaje.
So gaidi ni tafsiri tu inategemea ni upande gani una nguvu ta kusambaza iyo tafsiri.Mfano marekani lile shambulio la 2001,walimuita Osama gaidi,ila kwa upande wa kula Alquida/Taliban Osama na wale vijana waliogonda jengo wataonekana kama fredom fighters.
So,yeyote anaweza kuwa gaidi ni tafsir tu.
 
Back
Top Bottom