Naomba kujua namna ya kuingiza silaha (Bastola) kwa matumizi binafsi

pansophy

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
502
320
Habari wanajamvini

Nimepita Tanganyika Arms kwa lengo la kujua utaratibu wa kuingiza silaha (bastola) kwa ajili ya matumizi binafsi lakini sikufanikiwa kupata majibu. Naomba muongozo kwa anayefahamu utaratibu wa kuingiza kifaa hiki.
 
'utaratibu wa kuingiza silaha (bastola) kwa ajili ya matumizi binafsi'.

Kuingiza bastola kutoka wapi boss?

dodge
 
Habari wanajamvini

Nimepita Tanganyika Arms kwa lengo la kujua utaratibu wa kuingiza silaha (bastola) kwa ajili ya matumizi binafsi lakini sikufanikiwa kupata majibu. Naomba muongozo kwa anayefahamu utaratibu wa kuingiza kifaa hiki.
Unanunua unakuja nayo kwenye ndege kwa mfano silaha anapewa rubani. Ukifika nchini unaiacha hapo uwanja wa ndege. Unakuja kuleta kibali cha kuwa na silaha ya aina hiyo basi unaichukua. Shida NI KIBALI CHA KUWA NA SILAHA HASA BASTOLA. Nimewahi kuona aliyeinunua SA alipewa rubani wa ATC yaani wale waliomwuzia waliipakia kwenye ndege aliyopanda yule jamaa. Kama ni kuishika na kujaribu ni kule kwenye duka.
 
Zipo Thread Nyingi Kuhusu Utaratibu Wa Kumiliki
Ila Nadhani Inaanzia Kamati Ya Ulinzi Ya Wilaya
 
nunua weka kwa begi,
panda majahazi bubu,
unashuka unakua nayo.
Ila ukikamatwa nayo mjomba haaa haa ugtakukumbuka kile kicheko cha mkuu "hiiihiiihiiiiiii"
 
Zipo Thread Nyingi Kuhusu Utaratibu Wa Kumiliki
Ila Nadhani Inaanzia Kamati Ya Ulinzi Ya Wilaya
utaratibu wa kumiliki naufahamu, tatizo hauelezei namna ya kuingiza kutoka nje ya nchi. Kitu ninayotaka haipo kwenye maduka yetu ya ngome ya tanganyika arms
 
nunua weka kwa begi,
panda majahazi bubu,
unashuka unakua nayo.
Ila ukikamatwa nayo mjomba haaa haa ugtakukumbuka kile kicheko cha mkuu "hiiihiiihiiiiiii"
sina hamu ya kugombana na JAMHURI
 
Anza kwanza kuomba kibali cha kumiliki silaha ukishapata NDIO ununue .Ikishafika nchini unapofanya clearance waonyeshe kibali unaondoka na silaha yako.

Taratibu nenda ofisi ya POLISI WILAYA AU MKOA WATAKUPA MAELEKEZO
 
Hauwezi kufanya taratibu bila kuwa na namba ya bastola na aina. Nataka kujua nikinunua nani anakuwa custodian wa silaha yangu mpaka hapo ntakapo kamilisha taratibu za kiserikali
 
Ndiyo mana nkakupa njia mbadala ya kununua kupitia deepweb. Uko mkoa gani wewe? Kuna duka la silaha moja nalijua liko dar na lingine liko pale morogoro. Mikoa mingine sijui kama yapo au hakuna.
nataka kufuata taratibu za nchi, changamoto hakuna sehemu ambayo wanatoa maelekezo ya kutosha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo mana nkakupa njia mbadala ya kununua kupitia deepweb. Uko mkoa gani wewe? Kuna duka la silaha moja nalijua liko dar na lingine liko pale morogoro. Mikoa mingine sijui kama yapo au hakuna.

Sent using Jamii Forums mobile app
nataka kuagiza kutoka nje ya nchi, haya maduka hawatoi maelekezo ya kutosha namna ya kuingiza
 
Back
Top Bottom