mayowela
JF-Expert Member
- Nov 2, 2014
- 2,124
- 1,746
Habari wana Jf!
Naombwa kujuzwa nini kilikuwa lengo hasa ya kuanzisha inspirations na motivations speech, hadi kuelekea watu kuanza kuandika vitabu?
Je tofauti na faida ya kumjenga kiimani ni faida gani kiuchumi mtu hupata( excludes wanaoandaa event)?
Ni kweli ukisikiliza motivations kila wakati utakuja kuwa millionaire?
Kuna uhusiano gani wa mtu kufanikiwa na hizi inspiration?
Je kusoma vitabu vingi ndio rahisi ufunguo wa mafanikio?
Ukisikia mtu anaongelea hizi events za motivations unazitafsiri vipi katika jamii ya sasa? mfano Dar kuna game changer na ile ya Joel Nanauka inaitwa mentalship program.
Je zimebadili uchumi wako kiasi gani?
Na kama zinainfluince katika jamii kwanini baadhi ya maeneo hazifiki?
How to get started? Ans: Start where you are with what you have.
inspiration/motivation speech ni wauza mbinu za mafanikio kupitia makongamano, kupitia hiyo makongamano ambayo lazima utoe pesa wao ndio hupatia pesa humo humo plus wadhamini, kwa nchi yetu sijaona mtu anaeongea hayo mambo kafanikiwa tukamwita billionea,
kingine naona mtu akishika million kadhaa na yy anakuwa muhamasishaji wa mafanikio eg: Idris, millard, jokate, etc ila tukumbuke kila mtu anafamilia aliyotoka na support zinatofautiana, wakati mwenzio anakwambia alianza kazi ya posho 30 huku nauli akipewa na mama yake, wewe hujui hata nauli ya kwenda kila siku sehemu ambayo wanataka ujitolee hujui utaipata wapi