Freddie Matuja
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 1,465
- 2,857
2021 ndio tushaingia na 2025 haiko mbali sana ambapo Mkulu wa sasa atakuwa anakabidhi kijiti kwa ajae. Je tutakuwa tumefika na lengo la Mkulu la kujenga uchumi wa kati kwa kutumia viwanda na kutengeneza mabilionea 1000 kama alivyojitainisha 2019.
Wakati mmoja mwaka 2016 Mhe, Rais alitamka akiongea na waandishi wa habari IKULU, alitoa wito na kuwataka waandishi wa habari nao wanataka kujenga viwanda, wafungue kampuni then wampe Msigwa (ambae ni mkurugenzi wa mawasiliano IKULU) ili amfikishie na wapate mkopo kwa ajili ya kuendesha kampuni.
Najaribu kuwaza kwa sauti, je waandishi wa habari waliitikia wito? Baada ya kumfikishia Msigwa taarifa za kampuni waliyofungua pengine na business plan yenye kufikia soko lenye uhitaji fulani, je, walipata mkopo; walilenga sekta gani hasa ambayo waliona uhitaji mkubwa? Au hawakufikisha kabisa, nini kiliwakwamisha;
Kama sio muandishi wa habari na huna access na Msigwa, bado kuna dirisha la kumfikishia Rais yeye kama yeye; maana alisema njooni kwangu.
Kwa mfumo wa uzalishaji wa biashara yoyote rasmi lazima kusajili kampuni BRELA, kupata Cheti cha mlipa kodi TIN toka TRA, Tax Clerance Certifiate, leseni ya biashara na ofisi ambapo biashara itaanza. Nadhani kwa hatua hii Watanzania wengi wanaweza kumudu.
Hatua ya pili ni kutambua uhitaji wa soko (na hiyo inakuwa fursa) ya kwanini business plan iwepo kwa kutumia fedha za mtaji (CAPEX) pia fedha za kuendeshea biashara/uwekezaji (OPEX).
Tanzania kuna changamoto kwa benki nyingi (Commercial Banks) kutohangaika na start-up ikiwamo kutoa mikopo ya uwekezaji, ila mtu akiweza kuwekeza anavyojua yeye, then wao wanamfuata kumshawishi akope kwao apate hela ya kuendeshea biashara (OPEX).
Katika uchumi mkubwa na uchumi wa kati, uhitaji wa soko unaweza kumpa mteja/mwekezaji dhamani ya mkopo ili akizalisha na kuuza kwa soko ambalo liko wazi, anarejesha mkopo.
Tanzania tuna fursa nyingi sana za kuwekeza kukidhi mahitaji ya ndani ya soko;
Kila mwaka wizara ya afya inanunua dawa za bil zaidi ya 900 toka nje ya Tanzania; kwa tafsiri rahisi ukijumuisha na private hospital mahitaji/soko la ndani kwa madawa na vifaa tiba ni zaidi ya TRIL 1;
Kila mwaka tunanunua mafuta ya kula kwa mahitaji ya ndani zaidi ya tani 320
Kila mwaka tunanunua toilet paper
Kila mwaka tunanunua toothpick
kila mwaka tunanunua mashuka ya hospitali
Kila tuna-import mbegu za nyanya, cabbage, mahindi,
Kila mwaka tuna-import maziwa ya ng;ombe (maziwa ya unga na kimiminika)
Kila mwaka tuna-import chupi za watoto yet pamba inalimwa Tanzania
Kila mwaka tuna import leso
Kila mwaka tuna import chupi za kike na sidiria
kila mwaka tuna import chupi za kiume na yet pamba inalimwa Tanzania
Unaweza kuongeza na mengine
Wizara ya fedha ni namna gani ina focus nini tufanye ili kuongeza uzalishaji (kwa kushirikiana na wizara zingine za kisekta) ili kukuza mzunguko wa fedha ambao in-turn utaongeza tax base;
Sio sawa hata kwa watalii wanatoka Ulaya na Marekani wakija bongo kutalii bado wanakula cornflakes (imported), kahawa wanayokunywa (imported); cocoa (imported);
Kuna faida gani kila mwaka tunatenga zaidi ya bilioni 500 kugharamia elimu na baada ya hapo hatuna uhakika hiyo fedha itarejeshwa vip na wahitimu wa vyuo vikuu ambao walipata mikopo.
Hata kwa darasa la kwanza mpaka kidato cha nne, lazima tuone return on investment kwa namna moja au nyingine.
Sina imani na kejeli za misemo kama "mitano tena" au #tutaelewana tu kama zita-solve matatizo yetu.
Ila tukiamua kusililizana kuna mahali tutafika.
Mwekezaji pale chuo kikuu cha Dar es Salaam (Mlimani City) hakuwa na fedha mkononi in term of billions; alikuwa na investment strategy ambayo alihitaji serikali impatie legal agreement ya kumkodishia eneo la uwekezaji kwa miaka kadhaa na atawalipaje; makubaliano yale (yalimfanya akawekeza); inawezekana baadhi wakasema, jamaa alitupiga sana. Ila tukfanya equation kama asingekuja na kabla ya yeye kuja, thamani ya fedha na mzunguko wa fedha mwenge na ubungo ulikuwaje; ukipima uwekezaji ule positively umeingiza bei gani kwa wananchi, tax base imepanuka kiasi gani na ripple effect kwa maeneo jirani na Dar as a whole; nadhani wengi tutakubaliana, tunapata si haba ukilinganisha na wakati hayupo; kama kuna mahali tunapigwa tuna nafasi ya kukaa nae chini kwa kuangalia yeye anapata nini, deni alilokopa kujenga ana-service vip na faida anayopata tokana na fedha anayochuma Tanzania.
Tukichukua uwekezaji wa mlimani city kama moja ya investment model, kumbe hazina, wizara ya ardhi, ofisi ya mwanasheria mkuu na TIC vingeweza kuwapa watu wengine just papers (legal docx) ili kutokea hapo tujenge uchumi jumuishi ambao unatoa tumaini kwa vijana wanaosoma wajue bado kuna mwangaza wa kuweza kuajiriwa private sector.
Kumbukumbu za wakoloni wetu zinasema "1893 visionary German agronomist Dr. Richard Hindorf introduced sisal into Germany East Africa ambayo ni Tanganyika.
Huyu mzungu aliiba miche ya mbegu 1000 za katani toka Mexico; mpaka anafika Tanganyika alikuwa na miche kama 90 iiyokuwa hai; ila matokeo yake ni Tanganyika kuwa miongoni mwa wazlishaji wakubwa wa katani na viwanda vingi vya kuchakata final products vikiwa Ujeruani na baadae UK.
Ili tufike, lazima tuwe na overt operations na covert operations kwenye uwekezaji. Serikali lazima iwe upande wa mbinu ambazo hazina lengo kuhujumu wengine duniani, ila kuona namna gani tunatumia competitive advantage kujijenga, kupunguza imports na kuongeza exports ili kuongeza fedha za kigeni nchini.
Nimalizie kwa kusema nakubaliana na kujenga viwanda, ila sio sawa kuruhusu wachina kuja na viwanda vya toilet paper, viwanda vya mifuko ya kufungashia. Hii sio sawa. Huwezi kwenda China ukaweka kiwanda cha toilet paper au India wakakubali; kuna vitu ambavyo wanajua sio rocket science kama kuna serious investor kuna maeneo ambayo kweli aruhusiwe na kuwe na uwezeshaji kama aliofanyiwa wa mlimani city ili neema ya cashflow iwe kwa wingi Tanzania.
Heri ya mwaka mpya 2021.
F