Naomba kujua lengo la kuanzishwa inspirations talks, motivations etc

Principal Focus

JF-Expert Member
Jan 4, 2013
923
547
Habari wana Jf!

Naombwa kujuzwa nini kilikuwa lengo hasa ya kuanzisha inspirations na motivations speech, hadi kuelekea watu kuanza kuandika vitabu?

Je tofauti na faida ya kumjenga kiimani ni faida gani kiuchumi mtu hupata( excludes wanaoandaa event)?

Ni kweli ukisikiliza motivations kila wakati utakuja kuwa millionaire?

Kuna uhusiano gani wa mtu kufanikiwa na hizi inspiration?

Je kusoma vitabu vingi ndio rahisi ufunguo wa mafanikio?

Ukisikia mtu anaongelea hizi events za motivations unazitafsiri vipi katika jamii ya sasa? mfano Dar kuna game changer na ile ya Joel Nanauka inaitwa mentalship program.

Je zimebadili uchumi wako kiasi gani?

Na kama zinainfluince katika jamii kwanini baadhi ya maeneo hazifiki?

How to get started? Ans: Start where you are with what you have.
 
kwa kweli mimi kusoma kitabu cha page mia tano kinachoeleza mambo rondomly nilishindwa aisee,motivation ni muhimu katika maisha ila ziendane na lengo mfano:unataka kujua mbinu za kuacha uvuvi badala ya kusoma kitabu cha page miatano nibora kutafuta makala au kitabu kidogo tofauti tofauti zinazoelezea mbinu za kuacha uvivu,ukisha maliza kujifunza mara moja anza utekelezaji.

kitabu kama rich dad poor dad ni kitabu kizuri sana lakini kina mambo mengi sana kiasi kwamba unaweza kujufunza mambo na usiyatumie kwa wakati huo hivyo baada ya muda utakuwa umesahau,hapo utaona ni bora kusoma kwa malengo na sio kusoma mavitabu mradi umesikia ni kizuri.
 
Unamawazo kama yangu... Sema bado huwa najiuliza kama biblia na kuruhani watu wamezikataa inakuaje mtu akaongozwa na mawazo ya mtu?
 
Uhuni
Wizi
Hakuna lolote

Wakukutia moyo ni familia na ndugu zako.. Ukiona wanazingua jitie moyo mwenyewe.. Au nenda kanisani

Mie sifanyi ujinga huo kwenda kumlipa MTU aniambie unaweza.. Maana popote nilipoweza niliamka nikaenda nikaanza kufanya.. Na naamini hakuna anayeweza kwa kukaa na kusikiliza.
 
Ni mpuuzi pekee ambaye hajui umuhimu wa vitabu ndio anaweza kujitokeza hadharani na kusema usomaji vitabu hauna umuhimu wowote kwa binadamu

Laiti hayo mnayosema yangekuwa sahihi binadamu tusingekuwa na maisha tuliyonayo sa iv kwani sehemu kubwa yanayogunduliwa sa iv muongozo wake upo kwenye maandishi kutoka kwa mababu wa kale

Umuhimu wa vitabu ni latika kupngeza maarifa yaan unaweza kuwa unafanya biashara bila ya kuwa na maarifa uka struggle sana lkn siku ukisoma kitabu chenye maarifa ya namna bora ya kuendesha biashara then tegemea mabadiliko makubwa kwenye biashara yako

Khs motivation speaker yes zina umuhimu wake hasa kwa wale wenye self doubt, hswa jamaa kazi yao ni kukupa courage kuwa inawezekana haina haja ya kuogopa so huwezi kuwakebehi watu km hawa wana umuhimu wao kwenye jamii, na hta jeshini watu wa motivation wapo, mwanajeshi kabla hajaingia kwenye ulingo wa vita lazima atakuwa na uoga flani sasa kazi ya kamanda wa notivation speaker ni kumpa speech ili kumjaza ujasiri hyu mwanajeshi ili kumuondolea hofu aliyokuwa nayo na kupambana , kwa hyp hawa jamaa wana umuhimu sio vizuri kuwakebehi
 
Uhuni
Wizi
Hakuna lolote

Wakukutia moyo ni familia na ndugu zako.. Ukiona wanazingua jitie moyo mwenyewe.. Au nenda kanisani

Mie sifanyi ujinga huo kwenda kumlipa MTU aniambie unaweza.. Maana popote nilipoweza niliamka nikaenda nikaanza kufanya.. Na naamini hakuna anayeweza kwa kukaa na kusikiliza.

Kumbe basi wewe ni mmoja wa wale wanaosema action speak louder than words.
 
Ipo siku nitatoa ushuhuda wa ni kwa namna gani motivations and inspirations zilinisaidia kufanikiwa katika maisha yangu. Achana na hizi inspiration talks za wachumia tumbo wa kibongo, hapa nazungumzia zile speeches za watu mashuhuri duniani. Kwa mfamo one of the best speech ambayo napenda kuiangalia mara nyingi ni ile Commencement speech ya Sean Combs (P Diddy) ambayo aliitoa mwaka 2014 akiwa anagraduate Howard University.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom