Wahitimu elimu ya juu na changamoto ya ukosefu ajira

sky walker

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
1,160
824
Tafiti za mwaka 2010 hadi 2014 za Shirika la Kazi Duniani (ILO) zinaonesha kupanda kwa viwango vya ukosefu wa ajira barani Afrika, hata tafiti zilizofanyika kati ya mwaka 1991 hadi 2000 zinazungumzia ukosefuwa ajira kwa kiasi kikubwa.
graduation.jpg

Tanzania inakadiriwa kuzalisha vijana zaidi ya laki sita tayari kuingia katika soko la ajira kwa mwaka (2014), wakati soko lenyewe haliwezi kuchukua vijana zaidi ya 50,000.

Katika makala haya nipo na Joel Nanauka ambaye ni mwandishi wa vitabu, mwanadiplomasia wa uchumi katika maendeleo ya kimataifa, pia amebobea katika biashara na uongozi.

Nanauka anasema kinachoendelea sasa ni kwamba muelekeo wa uchumi umebadilika duniani kote ambapo kumekuwa na matumizi makubwa ya teknolojia ambayo yanapunguza idadi ya watu wanaohitajika katika kazi.

Kwa mfano kuingia kwa mashine za kutolea fedha (ATM) ina maana wale waliokuwa wanafanya hiyo kazi benki wamepungua pia. Na hii imeenda kwenye kila sekta si mabenki tu, kinachofanyika ni kwamba teknolojia imechukua nafasi za watu.

Anasema dunia kwa sasa ipo katika uchumi ambao unatumia zaidi mtaji (Capital intensive) kuliko nguvu za watu katika kazi (human intensive), na sio Tanzania pekee bali mfumo huu umeenea dunia nzima.

Madhara ya mfumo huu wa uchumi ni kwamba unapelekea fursa kuwa chache na si kwa sababu uzalishaji unapongua bali ni matumizi ya mashine yamekuwa makubwa zaidi.

“Sasa kama uchumi umebadilika tunatakiwa kubadilisha mitaala yetu ili tuweze kukabili hizi changamoto kwa sababu mitaala iliyopo ilikuwa ya uchumi uliyopita (human intensive),” ameeleza.

“Turudi upya tuangalie kama kinachofundishwa kinaendana na mazingira ya sasa, kwa sababu kinachotokea sasa ni kupishana kati ya kile kinachohitajika kwenye uchumi na kile tunachotoa kwenye elimu yetu,” anasema.

Anasema wahitimu wengi wa vyuo vikuu kuna vitu vingi sana vya msingi ambavyo hawavijui na ndivyo vinawakwamisha katika soko la ajira, jambo hilo ni ujuzi ambao upo wa aina mbili.

Kwanza ni ujuzi ambao mtu anafundishwa darasani (hard skills) ambapo utafundishwa vitu kama kanuni za biashara, namna ya kuongeza mtaji nakadhalika. Ujuzi wa pili ni ule unaokuwezesha kutumia vile vitu ambavyo umevisoma darasani (soft skills) ambao haufunishwi sehemu yoyote.

“Kwa mfano uwezo wa kuwasilisha wazo mbele za watu, kujijengea kujiamini, uwezo wa kuandika vizuri watu wakakuelewa, hivi vitu havifundishwi.

“Vijana wengi wanapohitimu shule wanajua kanuni na baadhi ya mambo waliyokariri, hawajui namna gani upate wazo la kibiashara au unawezaje kumiliki biashara yako, hivi ni vitu ambavyo havifunzwi, kinachotakiwa kubadili elimu yetu iendane na mahitaji,” anaeleza Joel.

Anasema vijana wengi wamejikita katika ujuzi wa mwanzo (hard skills) ambao pekee haukidhi, akitolea mfano wa kopyuta mezani bila kuwepo kwa CPU, hakuna kitakachofanyika.

Ripoti za Shirika la Kazi Duniani (ILO) zinaeleza Tanzania kuna tatizo la watu wengi kutoajirika, na si kwa sababu ajira hazipo bali hawana sifa za kuajiriwa ambazo si vyeti pekee bali ni uwezo binafsi wa kazi (soft skills).

Wahusika Wanasemaje?

Charlotte Katron ni wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Mbeya Sayansi na Teknolojia (MUST) katika fani ya usanifu majengo, anaeleza mtazamo wake kuhusu hilo.
timthumb.jpg

Anasema wahitimu wanamaliza shule wakiwa na uwezo mdogo wa kiutendaji kazi, hivyo wanapoenda katika soko la ajira kuna vitu wanatakiwa kufundishwa kwanza.

“Kwa soko la ajira lenye ushindani ambalo watu wanataka waone uwezo wako ndipo wakulipe, hiyo ndio changamoto kubwa,” anasema.

“Pia suala la kustaafu pia linachangia kwa sababu wanaostaafu ni wachache, wakati wanahitimu ni wengi zaidi, hivyo hawawezi wakawaajiri watu kama hamna nafasi hiyo.” anaeleza Katron.

Je, Nini Kifanyike?

Nanauka anapendekeza awali ya yote mfumo wa elimu kuangalia kama unakidhi mahitaji ya sasa. Anabainisha kwa mtazamo wake haukidhi na ndio sababu ya kujitokeza changamoto ya ukosefu wa ajira.

Pili serikali iwekeze kwenye sekta ambazo zinaajiri watu wengi zaidi, kwa sababu sasa hivi uchumi wa Tanzania unakuwa kwa asilimia sita hadi saba, lakini sekta zinazokuwa ni mawasiliano, benki na madini ambayo wanaajiri watu wachache sana.

Anasema sekta ya kilimo ambayo ina ajiri watu karibia asilimia 80 ya wananchi inakuwa kwa asilimia nne pekee.

“Unaposema uchumi unakuwa ni kweli ila unawanufaisha watu wachache sana, lakini mabadiliko yakitokea kwenye kilimo yatawagusa watu wengi.

“Watu wana shahada za kilimo lakini wanaogopa kwenda kulima kwa sababu kilimo hakijapewa mfumo wa kibiashara, sio vijana hataki kwenda kulima bali ni mfumo si rafiki ingawa maeneo ni mengi,” anasema Nanauka.

Vipi kuhusu kujiajiri; Nanauka anaeleza ni sawa vijana kujiajiri lakini angalizo ni kwamba ujuzi mkubwa unahitajika katika eneo hilo, na hatari kubwa zaidi katika shule zetu ujuzi wa kujiajiri haufundishwi.

“Unakuta mtu amesoma biashara Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), lakini biashara aliyosoma yeye ni ya kwenye vitabu, hajui chochote kuhusiana na uhalisia wa mambo huko mtaani.

“Tunaposisitiza watu wajiajiri, cha kwanza lazima tuwape maarifa yanayotakiwa ambayo yatewalekeza wapi wakajiajiri na mazingira yawe yameandaliwa tayari kwa ajili yao,” anasema Nanauka.

Nickson Saimoni (Nikki wa Pili) msanii wa muziki wa Bongo Flava na msomi wa PhD kupitia mitandao ya kijamii aliwahi kuanzisha mjadala kuhusu wahitimu na suala la kuajiriwa kwa kueleza tujiulize kama vyuo vinafundisha kwa ajili ya kwenda kujiajiriwa au kuwa wafanyakazi.

Anahoji hivyo kwa sababu kwenye matangazo ya vyuo husika wanajinadi kuwa wahitimu wetu wanafanya vizuri katika soko la ajira. Sasa hivi ajira hazipatikani, je tufunge vyuo hadi pale ajira zitakapokuwa zinapatikana ndio vyuo vianze kazi ya kuwafundisha wafanyakazi?, hapana!.

“Vyuo vitengeneze watu wanaoweza kufikiri, kuchambua, kutafuta na kuzalisha maarifa kwa lengo la ukombozi wa jamii na si kuwatengeneza wanafunzi kama bidhaa ya kwenda kujiuza sokoni,” alieleza.

Anasema faida ya mtu aliyenje ya mfumo wa ajira au kuajiriwa ni kwamba bidhaa yake ina wateja wengi, wakati yule aliyeajiriwa bidhaa ya ina mteja mmoja (bosi wake) siku mteja akikinai bidhaa ina maana kazi hana tena.
 
Janga la kidunia sasa na si Tanzania pekee..

Kwetu ukosefu wa ajira unachangiwa na mambo meengi mengi,.moja wapo ni elimu yetu,mitaala yetu haiendani kabisa na hali halisi ya wakati uliopo serikali lazima iliangalie upya jambo hili..wasomi wengi wa kibongo tunakosa soko na hatuuziki,.mfumo wetu MBOVU na sio rafiki kwa wakati huu..

Vijana ambao ndio wahanga wa kukosa ajira,tunahitaji sera na mipango bora ya maendeleo(japo IPO),.sekta kama viwanda,madini,utalii,kilimo/ufugaji na miundombinu ya kiuchumi inahitaji kuangaliwa kwa jicho la tatu ili kuwezesha upatikanaji wa ajira pamoja na kujiajiri.
 
Janga la kidunia sasa na si Tanzania pekee..

Kwetu ukosefu wa ajira unachangiwa na mambo meengi mengi,.moja wapo ni elimu yetu,mitaala yetu haiendani kabisa na hali halisi ya wakati uliopo serikali lazima iliangalie upya jambo hili..wasomi wengi wa kibongo tunakosa soko na hatuuziki,.mfumo wetu MBOVU na sio rafiki kwa wakati huu..

Vijana ambao ndio wahanga wa kukosa ajira,tunahitaji sera na mipango bora ya maendeleo(japo IPO),.sekta kama viwanda,madini,utalii,kilimo/ufugaji na miundombinu ya kiuchumi inahitaji kuangaliwa kwa jicho la tatu ili kuwezesha upatikanaji wa ajira pamoja na kujiajiri.
Well,
Unadhani pande zote husika zimefanya ya kutosha au kuna maandalizi yoyote ya kisera na ki mifumo kukabiliana na hali hii?
 
Well,
Unadhani pande zote husika zimefanya ya kutosha au kuna maandalizi yoyote ya kisera na ki mifumo kukabiliana na hali hii?
kazi ya serikali ni kupanga mipango ya kuleta maendeleo,na wananchi ni wajibu wao kutekeleza mipango hiyo kwa mujibu wa nafasi ya kila mwananchi..lakini pande zote hizi zinahitajiana katika kufikia lengo,.

Sasa sijui kama kuna maandalizi mapya au sera mpya ya kukabiliana na hali hii,au kama kuna mfumo mpya ambao upo au unakuja,hili sina hakika nalo.
 
Sera za kazi ni mbovu wadosi ,wachina ,masirilanka wanachukua kazi kilaini tena za kawaida sana ambazo wapo wenye uwezo (wazawa).Tanzania kuna CPA nyingi na wahasibu wengi tu ila Private sector asilimi 80 FC,AFC,CA zinashikiliwa na wageni
 
................pia Tanzania tulikurupuka kuwa na vyuo vikuu vingi badala ya kuwa na vyuo vingi vinavyotoa mafunzo ya ufundi, matokeo yake leo kila mtu ana degree na anataka aajiriwe awe anakaa ofisini anapigwa na kiyoyozi.

Tunakokwenda ni kugumu sana.
 
kazi ya serikali ni kupanga mipango ya kuleta maendeleo,na wananchi ni wajibu wao kutekeleza mipango hiyo kwa mujibu wa nafasi ya kila mwananchi..lakini pande zote hizi zinahitajiana katika kufikia lengo,.

Sasa sijui kama kuna maandalizi mapya au sera mpya ya kukabiliana na hali hii,au kama kuna mfumo mpya ambao upo au unakuja,hili sina hakika nalo.
Ahsante,

So tusitegemee miujiza kama hali ndiyo hii,as we speak huu ni mwaka wa tatu sasa vijana waliomaliza chuo kuanzia cheti mpaka degree ya kwanza wako kitaa, private sector ambayo inasaidia ku absorb nayo sina hakika kama imepanuka zaidi ya shrinking (wenye takwimu halisi za viashiria vya ukuaji wa uchumi wanajua).

Mbaya zaidi ndio hii ya "white colar jobs mentality" neither kuajiriwa nor kujiajiri.. typical a time bomb!

Nani amfunge paka kengele!
[HASHTAG]#mumu[/HASHTAG]
 
Ahsante,

So tusitegemee miujiza kama hali ndiyo hii,as we speak huu ni mwaka wa tatu sasa vijana waliomaliza chuo kuanzia cheti mpaka degree ya kwanza wako kitaa, private sector ambayo inasaidia ku absorb nayo sina hakika kama imepanuka zaidi ya shrinking (wenye takwimu halisi za viashiria vya ukuaji wa uchumi wanajua).

Mbaya zaidi ndio hii ya "white colar jobs mentality" neither kuajiriwa nor kujiajiri.. typical a time bomb!

Nani amfunge paka kengele!
[HASHTAG]#mumu[/HASHTAG]
Ni kitendawili,.lakini lazima kiteguliwe..nani wa kutegua??,.mm na ww pengine hatujui,.
 
Back
Top Bottom