Naomba kujua lengo la kuanzishwa inspirations talks, motivations etc

Hahahaha! Wanauza mbinu za kufanikiwa sio..
Shida inakuja unapojaribu kufananisha wanachokiongea na hali za kimaisha/kiuchumi ni vitu viwili tofauti wengi wanamaisha ya kawaida tu ,tofauti na hayo wanayokaa kuwaahubiria watu kupitia vitabu na kazi zao nyingine , ambacho wengi hatujui sisi ndio tunaowapa ugali wao wa kila siku.
 
Anatufanya sisi ndo fursa...honestly sijawahi kuona umuhimu wa hawa watu labda kama ingekua ni free service.
Jamaa motivational speaker lakini kamshindwa mkewe form 4 failure, kuimba gospel tu kumemshinda, sijui anammotivate nani kiukweli. Masikio yamemsimama ka popo. Na wabongo walivyo maboya wanajaa kwenye hizo talk baadae wanalia Bakayoko kabana.
 
Shida inakuja unapojaribu kufananisha wanachokiongea na hali za kimaisha/kiuchumi ni vitu viwili tofauti wengi wanamaisha ya kawaida tu ,tofauti na hayo wanayokaa kuwaahubiria watu kupitia vitabu na kazi zao nyingine , ambacho wengi hatujui sisi ndio tunaowapa ugali wao wa kila siku.
Yah hapo ndipo msala huja
 
Habari wana Jf!


Naombwa kujuzwa nini kilikuwa lengo hasa ya kuanzisha inspirations na motivations speech, hadi kuelekea watu kuanza kuandika vitabu?

Je tofauti na faida ya kumjenga kiimani ni faida gani kiuchumi mtu hupata( excludes wanaoandaa event)?

Ni kweli ukisikiliza motivations kila wakati utakuja kuwa millionaire?

Kuna uhusiano gani wa mtu kufanikiwa na hizi inspiration?

Je kusoma vitabu vingi ndio rahisi ufunguo wa mafanikio?

Ukisikia mtu anaongelea hizi events za motivations unazitafsiri vipi katika jamii ya sasa? mfano Dar kuna game changer na ile ya Joel Nanauka inaitwa mentalship program.

Je zimebadili uchumi wako kiasi gani?


Na kama zinainfluince katika jamii kwanini baadhi ya maeneo hazifiki?


How to get started? Ans: Start where you are with what you have.
[HASHTAG]#mentorship[/HASHTAG]
 
Kuna mdau humu jf aliwahi kusema "ukiona unakaribishwa kwenye fursa ujue wewe ndio fursa yenyewe"

Hakuna mtu atakaye kukaribisha kwenye hela..
Umewahi kuona wapi chenge akiwakaribisha watu kwenye madeal ya pesa
 
Kuishi unahitaji kula, kunywa na pumzi lakini lengo linahitaji linahitaji njia ya kupitia so unapokuwa njiani unatafuta hamasa ama motisha ya kufika kwenye lengo.
Kumbe tunaelewana.Mtu timamu haishi tu kwa pumzi na kula pekeake.Binadamu ana malengo,ktk kutimiza malengo unahitaji hamasa (inspiration).Unaweza kuwa self-inspired (unajihamasisha mwenyewe) au watu wengine wana kuhamasisha.
We binafsi unaweza usione umuhimu wa inspiration/motivational speakers,labda huwahitaji.Lakini watu wanaeatumia sana hawa inspiration/motivational speakers.Mfano kuna jamaa anaitwa Azim Jamal.Huyu jamaa ni motivational speaker anaishi Canada lakini amezaliwa Tanzania.Jamaa huyu huwa analetwa na Makampuni mbalimbali hapa Tanzania kuongea na wafanyakazi wa Makampuni hayo ili awa motivate na hatimae kuongeza ufanisi ktk kazi.Pia kuna motivational/inspiration speakers wengine ambao wanapendwa na kufuatiliwa sana kama vile;Dr.Cris Mauki,Paul mashauri,Dr.Elli VD Waminian,Robert Mwan`gamba,Eric Shigongo,Harris Kapiga.
Tatizo letu sisi wabongo,tunawachukuliwa hawa watu kuwa ni watu wanaojidai wanajua sana.Huo mtazamo sio sahihi,wao wapo gifted kuwa inspire na ku motivate watu wengine,sio lazima wao binafsi wawe perfect.Nikweli sio kila inspirational/motivational speaker ata ku inspire au kuku motivate.Mfano mimi binafsi Harris Kapiga na Eric Shigongo viwango vyao viko chini sana kiasi kwamba hawanihamasishi kabisa.Lakini kuna watu huwaambii chochote kuhusu Harris Kapiga na Eric Shigongo wanawapenda na kuwafuatilia sana.Mimi binafsi na mkubali sana Dr.Elli Waminian,pia Paul Mashauli hasa kwenye inspiration za biashara na ujasilia mali.
 
Prof. Mauki (PhD) na Dr. Pilipili (PhD) ndo Motivational Speaker wenye pesa ndefu nchini walioingia kwenye list ya Forbes 2018
 
kupoteza mda wa kwenda katika mikusanyiko ya inspiration talk ni ujinga.

haina tofauti na kupoteza mda kwenda kuombewa katika makanisa ya wachungaji wa kileo.

mmewahi kujiuliza kuhusu bakhresa, mengi na watu wengine waliofanikiwa nchini kama katika ujana wao waliowahi kuhudhuria inspiration talk?.

siwezi kuwa inspired kwa porojo, nakuwa inspired kwa vitendo.
Faiza Ally kaandaa event ya single mazas, kiingilio 15,000. Sasa sijui anaenda kuwamotivate nini huko?
 
Motivation speech zinafaida nyingi saana hasa pale unapojua jinsi na namna ya kuzifata

N.b utajiri haufundishwi
 
kwa kweli mimi kusoma kitabu cha page mia tano kinachoeleza mambo rondomly nilishindwa aisee,motivation ni muhimu katika maisha ila ziendane na lengo mfano:unataka kujua mbinu za kuacha uvuvi badala ya kusoma kitabu cha page miatano nibora kutafuta makala au kitabu kidogo tofauti tofauti zinazoelezea mbinu za kuacha uvivu,ukisha maliza kujifunza mara moja anza utekelezaji.

kitabu kama rich dad poor dad ni kitabu kizuri sana lakini kina mambo mengi sana kiasi kwamba unaweza kujufunza mambo na usiyatumie kwa wakati huo hivyo baada ya muda utakuwa umesahau,hapo utaona ni bora kusoma kwa malengo na sio kusoma mavitabu mradi umesikia ni kizuri.
Yaani kuacha uvivu ni mpaka ukasome kitabu? sawa bwana
 
Ukitembea na walioshindwa 9 basi ujue namba 10 utakuwa ww. Acha wenzako tushibe maarifa ya akina less brown, paul sineck, Dr myles Monroe, dale carnigie, Robert kiyosaki, the late Jim rohn, zig zigral, denzel Washington, Arnold Shwarzinegal, depak Chopra, Ali daniel, Eric Thomas, Anthony Robbins, Stephen covey na wadau wengine endeleeni kuweka vichwa vingine. Tusaidie hichi cha wasio na imani. Mafanikio ni Imani kama ww huamini katika vitabu na motivational huwezi kuona impact yeyote. Kumbuka Bible is the most inspirational and Motivational book ever written in the history of mankind's.
 
Back
Top Bottom