Chibike
JF-Expert Member
- Aug 16, 2024
- 4,896
- 7,522
Wazo kuu hapa ni kwamba utajiri wa kweli wa matajiri haujatokana na kuwa na rasilimali asilia (kama mafuta, madini, au ardhi yenye rutuba) bali ubora wa rasilimali watu (human capital), yaani, ujuzi, maarifa, ubunifu, nidhamu, na uwezo wa kufanya kazi kwa pamoja wa wananchi wake.
Naomba niongelee nchi kadhaa hapa.
Japan ni nchi ya visiwa yenye milima na ardhi ndogo ambayo haina rasilimali asilia zinazohitajika (haina mafuta, gesi asilia, au madini mengi). Lakini kwa kuwekeza kwa nguvu katika elimu ya hali ya juu, sayansi, teknolojia na nidhamu ya kazi, imekuwa uchumi mkubwa wa pili ulimwenguni kwa muda mrefu.
Uswisi pia haina bahati ya kuwa na rasilimali asilia. Lakini imejenga utajiri wake kwenye mabenki, usimamizi bora, ubora wa viwanda (kama saa), na uvumbuzi wa dawa. Hii yote inatokana na akili na ujuzi wa watu wake.
Singapore, ilikuwa nchi ndogo, isiyo na rasilimali asilia yoyote, hata maji safi yaliagizwa kutoka kwa jirani yake. Mwanzilishi wake, Lee Kuan Yew, aliwekeza karibu kila kitu katika kuunda rasilimali watu bora. Alijenga mfumo wa elimu wa kipekee, serikali yenye uadilifu na utendaji, na utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii. Leo, Singapore ni moja ya matajiri duniani.
Lakini je tunawezaje kujifananisha na nchi kama Japan, Singapore, na Uswisi?
Sisi Tanzania na nchi nyingine tuna kitu kinaitwa "Laana ya Rasilimali"
Kuna nchi nyingi zenye rasilimali asilia nyingi (kama sisi, Venezuela, Nigeria, na nyinginezo nyingi za Afrika) lakini bado tuna umaskini mkubwa na maendeleo duni. Hii inaitwa "Laana ya Rasilimali" (The Resource Curse). Na sababu za "Laana ya Rasilimali" ni mapato yanayotokana na rasilimali asilia huwafanya viongozi kuwa wafujaji na wanyonyaji wakubwa, hawajali kukuza sekta nyingine. Huzalisha rushwa na mambo chungu nzima.
Mchango wa rasilimali watu kwa ukuaji wa kiuchumi unapimwa kwa viwango bora vya uongozi, vya elimu, ujuzi, na afya, na ni kiashiria bora cha ukuaji wa kiuchumi wa muda mrefu kuliko uwepo wa rasilimali asilia. Rasilimali asilia ni msaidizi, si msing, rasilimali asilia zinaweza kuwa faida ya nyongeza (a bonus) ikiwa utajiri wake utatumiwa kwa hekima ili kuwekeza tena katika watu (elimu, afya, miundombinu) na katika sekta mbadala za kiuchumi. Je, sisi tuna uongozi bora wenye maarifa na hekima ? Je tuna elimu bora? Je tuna ujuzi? Majibu mnayo.
Norway ni mfano mzuri wa nchi iliyotumia mafuta yake kwa hekima kukuza mtaji wake wa kitaifa na kuwekeza katika jamii yake.
Ubora wa rasilimali watu (uwezo wao wa kufikiri, kubuni, na kushirikiana) ndio huunda utajiri, teknolojia bora, miundombinu bora, mifumo ya kifedha bora, na bidhaa zenye thamana kuongezeka. Je tujihoji sisi tuna uwezo wa kufikiri, kubuni, na kushirikiana? Au tumemezwa na siasa maji taka na uchawa?
Rasilimali asilia zinaweza kuleta utajiri, lakini ili uendelee na ukue, inahitaji akili na usimamizi bora wa binadamu. Je sisi tujihoji tuna akili na usimamizi bora? Watu tuliowapa dhamana ya kusimamia hizo rasilimali Wana akili? Akili za kununua magari ya bilioni 20? Hizo ndio akili? Kama tu watu wanapewa makaa ya mawe kama karanga...tuna usimamizi bora kabisa kabisa ???
Bila kua na rasilimali watu lakini bora, rasilimali asilia huwa hazikusaidii kwa muda mrefu na mara nyingi huleta matatizo zaidi kama ambavyo tunaona Sasa.
Pia soma David Kafulila: 62% ya Utajiri wa nchi tajiri duniani haujaletwa na Maliasili walizonazo ila ubora wa Rasilimali watu walionao ampongeza Rais Samia