Naomba kuifahamu CV ya Juma Nkamia

Bungeni kuna watu wawili pekee kupata historia za elimu zao ni kazi sana Mbowe na Nkamia,wengine wote zinajulikana mf Kibajaji ,Musukuma na Kubenea ukiwaambia kuspell Comprehensive au waachie ubunge watachagua kuachia ubunge
Mbowe A level alinusa mkuu, sijui wewe hata o level ya kuungaunga kama ulifika.
 
Ninachokijua ni kwamba huyu ndiye mbunge wa jimbo duni la Chemba mkoani Dodoma , na aliwahi kuwa kiongozi wa timu ya soka ya Simba ya jijini DSM , aliwahi pia kupiga deiwaka BBC , japo alitaka kudanganya umma kwamba aliajiriwa , hata hivyo UKAWA wakamstukia bungeni.

Mwenye mtiririko wake wa elimu na kazi zake atuwekee hapa ili tumjue tupate kumjadili kwa haki .
ZAHANATI ZAFUNGWA KWA KUKOSA WATUMISHI-CHEMBA KWA NKAMIA

ZAHANATI mbili zimefungwa kwa kukosa watumishi wa kada ya afya katika Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma na kupelekea wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya.

Hayo yalibainika juzi wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge kwa lengo la kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo. Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Dk Olden Ngassa alisema wilaya hiyo ni miongoni mwa wilaya nchini zenye upungufu mkubwa wa watumishi wa kada za afya wakiwemo madaktari na wauguzi ambapo kati ya watumishi 632 wanaotakiwa, waliopo ni 142.

Alizitaja zahanati zilizofungwa kwa kukosa watumishi ni Chase na Igunga. Alisema wilaya hiyo yenye kata 26 na vijiji 114, ina zahanati 31 ambazo mbili zilifungwa kutokana na uhaba wa watumishi na kuna vituo vya afya vinne.

Dk Ngassa alisema upungufu huo mkubwa unatokana na uchache wa watumishi kada ya afya ili mwananchi apate huduma makini. Alisema kuna uhaba mkubwa wa watumishi wa kada ya unesi na waganga na vituo vingi vinaongozwa na wahudumu wa afya na hakuna zahanati yenye watumishi zaidi ya wawili.

Alisema kama kituo kina mtumishi mmoja basi hulazimika kufanya kazi saa 24 pasipo kupumzika. Alisema wamefanya mikakati mbalimbali ili kukabiliana na changamoto hiyo ikiwemo kuwasiliana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma na sasa jitihada zinafanyika na tayari wameletewa watumishi 12, lakini mpaka sasa hawajaanza kazi kutokana na taratibu zao za mishahara kushughulikiwa.

Pia alisema wilaya hiyo haina hospitali ya wilaya, lakini mchakato wa kupata hospitali umeanza na ekari 27 zimetengwa kwa ajili ya kujenga hospitali ya wilaya. Katibu Tawala wa Mkoa, Rehema Madenge alisema tatizo la watumishi wenye vyeti feki lilichangia kwa kiasi kikubwa kupunguza watumishi kwenye kada ya afya.

Alisema changamoto hiyo wameiona na wanaifanyia kazi. Mkuu wa mkoa, Dk Binilith Mahenge alisema suala hilo linafanyiwa kazi kwani hali si nzuri.

CHANZO: Habari Leo
 
Habari Leo linataka kufungiwa ?
 
Mimi nafahamu tu make alikuwa anasapua pale chuo cha mipango. Vyuma vilikaza akasapu miaka 3 hakuchomoka mwishowe wakampiga disco.
 
Back
Top Bottom