samahani wanajamvi, kujua CV ya mtu ni muhimu sana ila si lazima sababu unaweza kuwa na PhD za kukariri za bongo na ukawa na akili za darasa la saba tu, ukweli mimi sihitaji kujua CV ya mtu ila huwa nahangaika kupata LOGIC ya jambo la mtu mwingine! ukweli natamani kila mwananchi angekuwa japo na vidigrii viwili, sisi sote brains zingekuwa zinachaji sawasawa! na tungeweza kuzama kujua athari za muda mfupi na za kudumu kwa mtu mmoja mmoja na kwa jamii nzima kwa mambo ya ajabu tunayoyaanzisha kwa wenzetu wasio na kofia tulizonazo! in short wasio mjengoni! hakuna kitu nachukia kama mtu mmoja kuamka na kukurupuka kuanzisha jambo ambalo litagusa watu mil 50 hadi vitukuu vyangu na labda kwa athari mbaya zaidi , kwanini usihangaike na familia yako ndugu!!kwa mtazamo wangu miaka kumi inatosha sana, tena labda ingepunguzwa , katiba is independent of aliekalia kiti, jambo la kuwaza ni je aliepewa kiti akikitumia vibaya kwa manufaa yake na ukoo wake je miaka 14 kutapukutika wangapi bongo kwa njaa na magonjwa na ajali za magari na ajali za silaha kama SMG? je hujui kuwa madaraka hulevya watu wakajisahau kuwa wao ni binadamu na kujifanya miungu watu kwa kuwa wanaweza kuagiza mtu akamatwe, ateswe au auwawe wakijisikia tu? je hukuwaza kuwa mkuu akiwa na udikteta hakuna boma litasalimika hata la kwako, mf mkuu anaweza kuagiza nchi nzima iwe inalala saa nane mchana , wewe na familia yako mtatoka nje saa nane mchana? ziko wapi fikra pevu za baba Nyerere aliekwenda zake na kapu lote la akili na weledi? tumebaki makapi tupu! japo naelewa siku sote mwenye shibe hamjui mwenye njaa! mimi ni mkereketwa wa kutupa wa kiongozi wetu na muumini wa kijani asietetereka ila siamini katakata katika kuongeza miaka ya kiti cha uraisi, tunapowaza mabadiliko ya katiba tuwaze siku sisi tukiwa mavumbi je watoto wajukuu na vitukuu vyetu wataumia au watanufaika , tusijiwazie sisi tu na matumbo yetu na tusiwaze ya leo tu!tuwaze aliepewa rungu atalitumiaje kwa miaka kumi nne? that is too much time brother muanzilishi wa mada! laiti wabongo wote wangekuwa na elimu ya juu wangezama na kuchambua athari za kudumu kwa maisha yao na uzao zao kwa unachokianzisha naamini wasingetamani kuwa na mwakilishi wa dizaini hizi!