Naomba kufahamu umri wa Bwana Kangi Lugola

Ni kweli Magu itakuwa alimfundisha Kangi make kwenye CV yake Magu kahitimu chuo cha ualimu Mkwawa akichukua masomo ya diploma ya kemia hesabu na elimu 1981-1982.
Alimkuta Lugola pale SESESCO akampiga pindi la chemistry na maths.
Lugola alirudia sana primary au alichelewa kuanza shule.
 
Wakimuondolea walinzi kuna mapolisi watamla matako
Aliwanyanyasa sana viongozi wa polisi. Kweli malipo ni hapa hapa Duniani. Kama ni watu wa visasi atajuta ni kwa nini alichaguliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani

Hakujua kwamba angeachia ngazi ya uwaziri na kuwaacha mapolis wakiendelea na kazi yao ya upolisi. Lakini pia hakujua polisi anaweza kuwa waziri lakini waziri hawezi kuwa polisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa siku hizi ndiyo haiwezekani, lakini zaman ilikuwa mtu unaemzidi umri angeweza kuwa mwalim wako pia. Enzi hizo ilikuwa mwanafunzi wa miaka 18 anasoma darasa moja na mwanafunzi wa miaka 12.

Kumbuka JPM mzazi wake (baba) alikuwa ni mwalim so kuna uwezakano alisoma kwa umri mdogo nae Lugola alikuwa ni mtoto wa mkulima so alirudia shule mara kibao hachaguliwa kwenda secondary. Zamani ilikuwa ni kuchaguliwa kwenda secondary na siyo kushinda, kwa sababu ya uhaba wa shule. Enzi hizo kurudia shule hata mara nne ilikuwa ni jambo la kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
20200123_171529.jpg
 
Kwani Diploma ya ualimu enzi hizo ilikuwa inasomwa kwa miaka miangapi ?
20200123_171529.jpg
20200123_171544.jpg
 
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, ambaye anatoka Chama cha Mapinduzi, kitaaluma ni mwalimu na mtalaamu wa kemia.

Alizaliwa Oktoba 29 mwaka 1959 huko Chato mkoani Kagera, Kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Magufuli alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi huko huko Chato kuanzia mwaka 1967 hadi 1975 na baadaye akajiunga na shule ya sekondari ya Lake iliyoko Mwanza mwaka 1977 hadi 1978.

Kiongozi huyo alijiunga na chuo cha ualimu cha Mkwawa kilichoko Iringa, Kusini mashariki mwa Tanzania kati ya mwaka 1979 na 1982 ambapo alitunukiwa Stahahada ya Ualimu.

Baada ya kufuzu, alifundisha masomo ya hisabati na kemia katika shule mbalimbali za sekondari kuanzia mwaka 1983.

Magufuli hakuishia hapo kielemu kwani aliamua kujiendeleza zaidi na kujiunga na chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1985 hadi 1988 ambapo alitunukiwa shahada ya ualimu katika masomo ya kemia na hisabati.
 
Mkuu hii bado sijaelewa,ina maana alisoma chato primary kwa miaka 9? Na secondary mwaka mmoja?(hapa hujasema kama Ni O-level au A -level)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwamba mtu wa 59 hawezi kumfundisha wa 64? Hivi mmeisahau Tanzania ya kabla ya MMEM na MMES! Kuna watu kwa bahati mbaya wanaotokea familia za wazazi wasio na mwanga wa elimu walikuwa wanasoma ni wakubwa sana. Mfano mimi wakati naenda kuanza drs la kwanza kuna mwamba alikuwa anaishi jirani yetu hana mpango kabisa wa kwenda shule maana alikuwa tayari ana hang out na washkaji flani wanafanya kazi kwenye mabasi flani kutoka wilayani kwetu kuja Mwanza. Ila mama yangu akawa kapambana akamuombea nafasi pale shuleni tukaanza nae. Bingwa alikuwa kijeba kweli kiasi kwamba kuna washkaji tuliwakuta drs la 7 ila walikuwa wakituonea tukashtaki kwa huyu mwamba anawpiga dizain hadi wanaruka madirishani wanakimbia. Imagine mtu wa drs la kwanza anampiga mtu wa drs la saba. Huyu mwamba alikuwa na umri gani jiulize. Sasa mfano dada yangu ambae mi naanza la kwanza yeye yuko la 5 angemaliza akaendelea na kuwa mwalimu asingeweza kuja kumfundisha huyu mwamba tuliekuwa nae japo kuwa sista angekuwa kamzidi kidogo au wamelingana na huyu jamaa? Zamani kulikuwa na watu wa ajabu mashuleni mtu mnasoma nae shule ya msingi ila wikend akienda kuchunga ng'ombe ndama akagongwa na nyoka au akapata shida yoyote jamaa anambeba ndama makumi ya kilomita kutoka alikokuwa anachungia hadi nyumbani, unajiuliza mtu wa hivi ana umri gani unabaki mdomo wazi
 
Back
Top Bottom