Naomba kufahamishwa dawa nzuri ya kuua Panya, unga mweusi umedunda

UMUNYU

JF-Expert Member
Jan 28, 2017
685
484
Ni miezi sasa panya wamekuwa wananisumbua sana! Nimejaribu dawa za unga mweusi zinazouzwa dukani zimeshindwa, zile za pellets ndiyo hamna kitu!!

Panya hawa huingia ndani mwangu kuanzia jioni na hunichachafya hadi asubuhi! Nimewafuatilia naona wanatoka kwa jirani

Kwangu kuna fence ajabu wanaivuka na kuingia na kutoka! Nikiri ninaishi mazingira ambapo watu wakivuna mazao wanayahifadhi wenyewe tena wengine hufanya hivyo kienyeji, ndiyo maana hata panya wana afya kwa sababu hupata mlo kamili!

Imefikia hatua kwa kuwa huwa hata wanakimbizana wakiwa juu, panya akikudondokea maumivu yake ni kama umetupiwa jiwe la manati!

Naombeni msaada wa dawa nzuri ili niwateketeze!!
 
Unga dagaa zako safii.... Weka ktk njia zao kijiko kimoja kimoja...then nyunyiza Ile sumu unga mweusi kwa juu...
Hakuna panya anachomoa hapo..

Usiitoea haraka.. panya Ana akili anaweza asile siku mbili... Ya tatu atanasa. Utaanza kusikia nyumba. Inavunda. Sasa Kama una vitu vingi utajuta. Maana huwa wanaenda fia mbaali...mafichoni
 
Ni miezi sasa panya wamekuwa wananisumbua sana! Nimejaribu dawa za unga mweusi zinazouzwa dukani zimeshindwa, zile za pellets ndiyo hamna kitu!!

Panya hawa huingia ndani mwangu kuanzia jioni na hunichachafya hadi asubuhi! Nimewafuatilia naona wanatoka kwa jirani

Kwangu kuna fence ajabu wanaivuka na kuingia na kutoka! Nikiri ninaishi mazingira ambapo watu wakivuna mazao wanayahifadhi wenyewe tena wengine hufanya hivyo kienyeji, ndiyo maana hata panya wana afya kwa sababu hupata mlo kamili!

Imefikia hatua kwa kuwa huwa hata wanakimbizana wakiwa juu, panya akikudondokea maumivu yake ni kama umetupiwa jiwe la manati!

Naombeni msaada wa dawa nzuri ili niwateketeze!!
Mwaga chumvi ya mawe kwenye mapito yao yote, kama ni wa kutumwa hutawaona tena na hata kama ni wa kawaida hawatakusumbua tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni miezi sasa panya wamekuwa wananisumbua sana! Nimejaribu dawa za unga mweusi zinazouzwa dukani zimeshindwa, zile za pellets ndiyo hamna kitu!!

Panya hawa huingia ndani mwangu kuanzia jioni na hunichachafya hadi asubuhi! Nimewafuatilia naona wanatoka kwa jirani

Kwangu kuna fence ajabu wanaivuka na kuingia na kutoka! Nikiri ninaishi mazingira ambapo watu wakivuna mazao wanayahifadhi wenyewe tena wengine hufanya hivyo kienyeji, ndiyo maana hata panya wana afya kwa sababu hupata mlo kamili!

Imefikia hatua kwa kuwa huwa hata wanakimbizana wakiwa juu, panya akikudondokea maumivu yake ni kama umetupiwa jiwe la manati!

Naombeni msaada wa dawa nzuri ili niwateketeze!!
Weka house snake ndani ya nyumba, wale weusi wasiokuwa na sumu.

Hapo sasa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom