Wacha nikujibu hili pia, kufuga ndevu, kutokuburuza nguo mpaka chini ya kongo mbili, na kuvaa hijabu ya kisheria haya ni mambo yamefundishwa katika uislamu, na nimekuwa nikikueleza kila siku, kuwa hakuna hoja utakayoileta, yote haya yamo katika maneno sahihi ya mtume swala na salaam ziwe juu yake.
Na wewe hutaki mafunzo yeyote ya mtume swala na salaam ziwe juu yake, kumbe ungeyajulia wapi? na muongozo wa namna ya kumtizama mwanamke kabla ya kumuoa umewekwa wazi katika vitabu vya fiqh wanavyosoma watoto tu, wachilia mbali watu waliopiga hatua na uislamu haukuacha kitu.
Kwa kukupa faida, ukitaka kumuoa mwanamke unakwenda kwa jamaa zake na huu ndio muongozo wa Qur'an:
".....basi waoeni kwa idhini ya jamaa zao...."
Qur'an 4:25
Hawa ndio wenye binti, nenda kwao na ukamtizame vile vitu wanavyotizamwa wanawake wakitaka kuolewa, kama nywele, miguu, mikono, uso na yale mepesi kuonekana, huu ndio utaratibu wa uislamu, maswahaba walioa wanawake, mtume swala na salaam ziwe juu yake alioa, hutaki kujua walifanyaje kupata wake zao? kwasababu hutaki kutizama muongozo wa mtume swala na salaam ziwe juu yake, lazima upotee.
Ama suala la kuinamisha macho ni kuwatizama wanawake kando wasiokuwa halali kwa mtu na hili halihusiani kabisa na kumtizama mwanamke kwa jamaa zake baada ya kumposa, tizama malengo ya kukodoa macho barabarani ni nini? halafu utizame malengo ya kumtizama mwanamke wakati umeenda kumposa.
Ama kuzungumzia sheria tukufu ya Allah kwa istihzai na dharau, kama kwamba ndevu ni kitu kidogo sana, au hijab ya kisheria au kuvaa nguo inayoburuza, ukaongea kama kwamba ni maneno tu yapo kwenye katiba tahadhari mkuu, kuna mstari mwembamba sana baina kuwa muumini na kafiri, hayo ni mafunzo ya mtume muhammad swala na salaam ziwe juu yake na yeye alikuwa na ndevu nyingi, na akivaa nguo zisizoburuza na wakeze walivaa hijabu ya kisheria na walifunika nyuso zao, labda kama huamini kuna mtume unaamini kuna Allah tu, sasa sijui naye umemjulia wapi?.
"....basi na watahadhari wale wanaokwenda kinyume na amri yake, usije ukawapata wao msiba au ikawapata wao adhabu chungu."
Qur'an 24:63