Ukifatilia matendo ya Masufi asili yake ni katika Ukristo huko wakayaingiza katika Uislamu.Hata nyie pia mnapandisha mapepo kwenye ibada ?
Ukifatilia matendo ya Masufi asili yake ni katika Ukristo huko wakayaingiza katika Uislamu.Hata nyie pia mnapandisha mapepo kwenye ibada ?
Sio Dhikri?Asalam aleykum.
Leo sala ya Ijumaa nimesali Tabora Msikiti uitwao Shadhuly [ukitamkwa shazli]. Nakili sala yangu ilikua ngumu kwa sababu ya kupishana steps na wenzangu.
1. Rakaa ya pili baada ya kusomwa Surat fattah, kabla ya kusujudu, ikaingizwa maombi, ambao ni utaratibu mgeni kabisa kwangu.
2. Baada ya sala na dua. Nilitaka nifanye maombi binafsi. Ila Dua ile iliendelezwa kwa safu ya mbele kusimama na kutengeneza duara kwa kushikana mikono huku wakiwa kama wanarukaruka very subtly na huku baadhi wakiwa kama wanachagiza kwa kutoa sauti ya juu mithili ya mtu anayekabwa. Nilikosa utulivu hata wa dua binafsi.
wajuzi naomba elimu, hawa ni dhehebu gani? Wanaamini nini?
Walifanya DhikriBida'a.
Unaelewa nini ukiambiwa waja wema ? Una elimu yoyote kuhusu Qur'an ? Maana unaandika kama huna ukijuacho katika Qur'an.Masalafi watu wa bidaa tu,kuanzia niqab mpaka kufuata 'waja wema waliotangulia'..unafuata waja wema kama muongozo wakati kuna qur'an!?..kazi ya qur'an ni nini!?
Sasa utajuaje kama wanaswali kawaida au kimakosa na wewe sio msomi wa dini ?Qaadiriya wanaswali kawaida tu,ungeenda gongoni,msikiti nliokua nikiswali ijumaa udogoni
Mno bali ni jambo la dharura kabisa.Ni sahihi kuwatumia kama miongozo ya maisha?
Ukiwa hujui dini,uliza msikiti wa ijumaaSasa utajuaje kama wanaswali kawaida au kimakosa na wewe sio msomi wa dini ?
Quran haisemi tufuate waja wema,ambao kwa muktadha wa sallafiy na shia ni maswahaba,tabiina na tabi tabiina,quran inataka tufuate yenyewe na imesema 'ni nyepesi kueleweka'..ingekua maswahaba wako sahihi 100% ali na muawiya wasingetofautiana wala kupiganisha vita waislam wakauana kwa maelfu,wajukuu wa mtume hassan na hussein waliendeleza vita na uzao wa muawiya alina yazid,hawa wako kwenye waja wema,lakini hussein aliuawa karbala na waislam(waja wema) wenzie,ndiyo maana quran 3:103 ikatutaka tushikamane kwayoUnaelewa nini ukiambiwa waja wema ? Una elimu yoyote kuhusu Qur'an ? Maana unaandika kama huna ukijuacho katika Qur'an.
Unaposema Kuna Qur'an unamaanisha nini ? Hao waja wema ndio wanaijua Qur'aan kushinda watu wote waliopo hapa duniani, lazima tufate ufahamu wao sababu waliishuhudia Qur'an ilishuka, waliifanyia kazi na kuielewa dini vizuri, mpaka ikatufikia sisi.
Ukisoma Qur'an utakuta zimeelezwa fadhila zao katika Sunnah ndio usisema. Bali katika tunaambiwa kama walivyoamini wao badi hakika tutafauli.
Mbona unaandika kwa wingi na kuwahusisha maswahaba wote ? Walio tegea wangapi na ilikuwaje mwisho wa siku ? Sababu haya mambo yako wazi na yamedhibitiwa kwenye vitabu.Sasa wanafunzi wa maswahaba wanasifiwaje na qur'an wakati mtume alikua kishafariki!?..miongoni mean hai maswahaba ndiyo wale waliotegea kwenda vitamin qur'an ikawananga,ndiyo wale waliosingizia wanawake wema kuzini quran ikawananga,ndiyo waliopigana vita kugombea madaraka hadi leo ummah umegawanyika na wakauwana,mtume saw aliandikisha qur'an akiwaambia wasome asikie ikiwa walichoandika ndicho alichowasomea
Kwani kitu gani kilisababisha mzozo ukatokea baina yao ?Quran haisemi tufuate waja wema,ambao kwa muktadha wa sallafiy na shia ni maswahaba,tabiina na tabi tabiina,quran inataka tufuate yenyewe na imesema 'ni nyepesi kueleweka'..ingekua maswahaba wako sahihi 100% ali na muawiya wasingetofautiana wala kupiganisha vita waislam wakauana kwa maelfu,wajukuu wa mtume hassan na hussein waliendeleza vita na uzao wa muawiya alina yazid,hawa wako kwenye waja wema,lakini hussein aliuawa karbala na waislam(waja wema) wenzie,ndiyo maana quran 3:103 ikatutaka tushikamane kwayo
Hapa tutapajadili baadae maana naona unazidi kuonyesha ni kwa jinsi gani huujui Uislamu na Qur'an.Ukiwa hujui dini,uliza msikiti wa ijumaa
Hata mtume swala na salaam ziwe juu yake alituachia wasia akasema "shikamaneni na sunnah zangu na sunnah za makhalifa wangu waongofu wenye kuongoza...." alhadiythIt make sense.
Ahahaaaaa,mnapenda kuwafanya wenzenu hawajui dini, sallafiy bnaHapa tutapajadili baadae maana naona unazidi kuonyesha ni kwa jinsi gani huujui Uislamu na Qur'an.
Mbona maswali ya kijinga na ulijinasibu kujua dini!?..kwani pakisemwa 'somo la jiografia ni rahisi kueleweka' we unaelewa vipiKwani kitu gani kilisababisha mzozo ukatokea baina yao ?
Inaposema nyepesi kieleweka wewe unaelewaje ?
Aya gani ya qur'an Allah sw kawasamehe kundi la ali na kundi la muawiya kwa kuuana!?...Mbona unaandika kwa wingi na kuwahusisha maswahaba wote ? Walio tegea wangapi na ilikuwaje mwisho wa siku ? Sababu haya mambo yako wazi na yamedhibitiwa kwenye vitabu.
Maswahaba wangapi waliowasingizia wanawake wema kuwa wamezini ? Naona unatumia wingi kuwachafua maswahaba wakati mambo unayo yaandika kwa uhalisia ni ya mtu mmoja mmoja?
Wanawake wangapi walisingiziwa uzinifu ?
Vita gani walipigana kugombea madaraka na ilikuwaje na mwisho wa siku ikawaje ? Fafanua tukuhoji.
Lakini kwa ujumla maswahaba ni wanadamu na wanakosea na kwa yote walio yafanya na kwa fadhila za Allah aliwasamehe na kuwaridhia wote.
Maana yake ukileta au unapoleta lawama kwao ni kuonyesha huijui Qur'an.
Wacha nikuoneshe aya, wewe unajinasibu kufuata Qur'an pekee ila umenyimwa kuifahamu na kuijua, kwanza unapata wapi guts za kuwasema vibaya watu ambao allah aliwachagua kuishi na mtume wake? unadhani alichagua watu wa ajabu kama unavyotaka kutuaminisha? Qur'an imewasifu mno maswahaba, wao wote ni waadilifu na wanapata na kukosea kama wanadamu wengine.Walk qur'an imesema imesamehe makosa ya maswahaba!?..kwa kuuwana kwa malaki baada ya kifo cha mtume saw!?..qur'an inasema mtume kasemehewa dhambi zilizotangulia na zijazo
Aya ngapi zinasema mwenyezi mungu ni msamehevu na mrehemevu!?..hata wewe ukifanya toba ya kweli Allah anakusamehe,hili lipo dhahiri ndani ya Quran,hizo aya ulizotoa hazimaanishi maswahaba dhambi zao zote za awali na zijazo wamesamehewaWacha nikuoneshe aya, wewe unajinasibu kufuata Qur'an pekee ila umenyimwa kuifahamu na kuijua, kwanza unapata wapi guts za kuwasema vibaya watu ambao allah aliwachagua kuishi na mtume wake? unadhani alichagua watu wa ajabu kama unavyotaka kutuaminisha? Qur'an imewasifu mno maswahaba, wao ni wote ni waadilifu na wanapata na kukosea kama wanadamu wengine.
"Kwa hakika Allah amekwisha pokea toba ya nabii na muharijina na answari, ambao walimfuata katika saa ya dhiki, pale baada ya kukaribia nyoyo za baadhi yao kugeuka, basi akakubali toba yao, hakika yeye kwao wao ni mpole na ni mwenye kuwahurumia."
"Na {amewakubalia pia} wale watatu waliocheleweshewa toba yao, hata ikawa dhiki ardhi juu yao pamoja na ukunjufu wake, na zikawa na dhiki juu yao nafsi zao , na wakayaqini kuwa hapana pa kumkimbia Allah isipokuwa kwake yeye tu, kisha akawapokelea toba yao, ili waendelee kutubia, hakika Allah ndiye Mwenye kupokea toba mwenye huruma."
Qur'an 9:117-118
Unapata wapi ujasiri wa kuyazungumza makosa ya watu ambao tayari allah kishawasamehe?! wewe una uchungu zaidi na makosa yao kuliko mola wao aliyetangaza toba yao kwenye Qur'an? hawa ka'ab ibnu maalik, hilaal ibn umayyah na muraara ibni rabiy'ah hawa walibaki nyuma wakaacha kwenye vitani pasi na udhuru, toba yao imetangazwa kwenye Qur'an pasi na kuficha kitu, Allah awaridhie, wewe ujasiri wa kuongelea habari hizi unatoa wapi.
"Kwa hakika Allah amewaridhia waumini walipokupa kiapo cha utiifu chini ya mti, na alijua yaliyomo nyoyoni mwao, basi akateremsha utulivu juu yao, na akawalipa kwa ushindi wa karibu."
Qur'an 48:18
Uko wapi wewe na aya hizi? kwahyo watu hawa Allah aliwaridhia kwa muda tu, sio? Mimi ushauri wangu jitahidi sana ukae darasani usome, nikitizama post zao unaonekana ni mtu mzima, jitahidi uanze upya jambo hili, na ujiepushe kabisa na heshima za maswahaba wa mtume swala na salaam ziwe juu yake.
Yaliyotokea katika fitan na mtihani yote mtume aliyabashiri akiwa hai, na wao maswahaba wakiwa pembeni yake, ili Allah alihukumie jambo ambalo ilikuwa lazima litokee, hakuna watu bora baada ya mitume isipokuwa ni hawa maswahaba wa mtume swala na salaam ziwe juu yake, ajabu iliyoje kuandika kwa ujasiri kabisa, makosa ambayo allah ameshawasemehe.
Na yule ambaye Allah amemridhia hawi muovu milele.
MashaAllah. Imejibu sahihi. Allah akuhifadhiHao waja wema ni maswahaba na wanafunzi wao, Qur'an imewatukuza kuwatukuza kwa juu, na allah amewasifu, bila wao kutupasia mafundisho hiyo Qur'an ungeitoa wapi.
Watu Allah amewaridhia unasema kuwafuata ni uzushi, uko mzima kweli mkuu.
"Na wale waliotangulia wa mwanzo, katika muhajirina na answari, na waliowafuata wao kwa wema, allah amewaridhia na wao wamemridhia, na amewaandalia bustani zipitazo mito chini yake, hali ya kudumu humo milele, na huko ndiko kufaulu kukubwa."
Qur'an 9:100
Bila shaka hawa ndio walioelewa zaidi mafundisho ya uislamu, ni usalama mkubwa kufuata quran na sunnah kwa ufahamu wao, kuliko kila zama kutegemea ufahamu wake.
Aisee..Umenikumbusha kuna kipindi tulihamia maeneo fulani, ulikuwa mwezi wa Ramadhani mi na mdogo wangu tukasema tukasali sala ya Taraweh!
Tulisali rakah 4 tu tukashindwa tukaondoka! Kila kitu ni kigeni, tukijaribu kujitahidi kwenda nao sawa ikija rakah nyingine inakuja kivingine!
Kwakweli tuliondoka na hatukurudi tena hadi tulipopata msikiti mwingine wenye utaratibu tuliouzoea.
Naam. Hao ni masufi. Itikadi yao imejaa shirki, uzushi ktk dini na upotevu mwingi mno. Allah awaogozeNdio qadriah hao?