Naomba kuelimishwa kuhusu Shudhuly

Naomba kuelimishwa kuhusu Shudhuly

Kwa yeyote mwenye nia ya kupata elimu ya dini iliyo sahihi tafadhali wasiliana nami kwa Whatsapp no. 0688999006 nikuunganishe na link za Maduat wa Kisalafi Tanzania. Humo utapata elimu na faida kubwa zitakayokusaidia ktk ibada na miamala mbalimbali ya kimaisha.
 
Aya ngapi zinasema mwenyezi mungu ni msamehevu na mrehemevu!?..hata wewe ukifanya toba ya kweli Allah anakusamehe,hili lipo dhahiri ndani ya Quran,hizo aya ulizotoa hazimaanishi maswahaba dhambi zao zote za awali na zijazo wamesamehewa
Na kwa uliponijibu,nimeuliza aya ipi imewasamehe kundi la muawiya na ali kwa kuuana!?
Sidhani kama kuna mahala nimetaja kuwa wamesamehewa madhambi yao yaliyopita na yaliyotangulia, hili ni khaswa kwa mtume swala na salaam ziwe juu yake, ama maswahaba zake Allah ametangaza waziwazi amewaridhia katika Qur'an na watapata pepo zipitazo mito chini yake, nilikunukulia aya kule nyuma, hayo yaliyotokea baina ya ali na muaawiyah allah awaridhie wote, ni katika mitihani iliyowapitikia waislamu wakati wa kilele chake.

Na hilo halifuti kuwa Allah tayari alishawaridhia na ametaja kwenye Qur'an habari hizo zitasomwa mpaka siku ya qiyamah hazikufutwa, swala linakuja kupigana kumewafanya sio maswahaba wa mtume? ule uswahaba wao na heshima yao imeisha kwasababu hiyo? majibu bila shaka ni hapana kabisa.

Basi kama ndivyo, mengi tu yalitokea baina yao na Allah ametufundisha katika Qur'an tuwaombee msamaha, hili ndilo tuliloamrishwa ama kuzunguka huku na kule kutafuta aibu na makosa yao, ni kutangaza vita na Allah waziwazi, kwani hawa ni watu wameishi na kuinusuru dini hii, kwa mali zao na damu zao, na allah amewasifu kwenye Qur'an kuwa ni watu wakweli!.

"Wapewe pia {mali ya fay'i } mafakiri wa muhajirina waliotolewa majumbani mwao na mali zao kwa ajili ya kutafuta fadhila za Allah na radhi zake, na wanamnusuru Allah na mtume wake, hao ndio wakweli."

"Na wale waliokuja baada yao {maswahaba} wanasema: mola wetu! tusamehe sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu chuki kwa walioamini, mola wetu! hakika wewe ni mpole, mwenye huruma."
Qur'an 59:9-10

Hili ndilo jambo la sawa, ama vita havikubadilisha kuwa mua'awiyah ibnu abiy sufyaan allah amridhie yeye na baba yake kuwa alikuwa mwandishi miongoni mwa waandishi wa wahy, na haibadilishi kuwa ali ibnu abi twaalib allah amridhie kuwa ni mmoja wa makhalifa waongofu, na mmoja katika maswahaba waliobashiriwa pepo wangali hai, bali mtume swala na salaam ziwe juu yake, alitangaza waziwazi kuwa Allah na mtume wake wanampenda yeye, al muhim tuwe makini na heshima za maswahaba hawa watu ni bahari isiyopunguzwa maji yake kwa ndoo ya lita kumi.
 
Asalam aleykum.

Leo sala ya Ijumaa nimesali Tabora Msikiti uitwao Shadhuly [ukitamkwa shazli]. Nakili sala yangu ilikua ngumu kwa sababu ya kupishana steps na wenzangu.

1. Rakaa ya pili baada ya kusomwa Surat fattah, kabla ya kusujudu, ikaingizwa maombi, ambao ni utaratibu mgeni kabisa kwangu.

2. Baada ya sala na dua. Nilitaka nifanye maombi binafsi. Ila Dua ile iliendelezwa kwa safu ya mbele kusimama na kutengeneza duara kwa kushikana mikono huku wakiwa kama wanarukaruka very subtly na huku baadhi wakiwa kama wanachagiza kwa kutoa sauti ya juu mithili ya mtu anayekabwa. Nilikosa utulivu hata wa dua binafsi.

wajuzi naomba elimu, hawa ni dhehebu gani? Wanaamini nini?
Hiyo ni bid'aa haifai na haipo katika mfumo wa dini wapotoshaji wachache walio ingiza Hilo wanaita dhikr

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Muongozo ni Quran,hayo mengine ni uzushi,ndiyo yanakuja ya kufuga ndevu,usipofuga kafiri,kukata suruali,usipokata moroni,uvae niqab usipovaa upo uchi,wakati hayo yote hayapo kwenye qur'an!!
Tahadhari na unayoyasema usije ukajikuta unakufuru. Kumbuka Allah anashuhudia kila unachokiandika hapa. Usiisemee dini pasina na elimu. Allah akuongoze
 
DINI HIZI!
Nilienda Rufiji kusurvey. Nikaingia mskiti mmoja kusali we ! nilichokikuta mle niliogopa. Hizo DUA hatari. HOTUBA KIARABU MWANZO MWISHO.
Baada ya SALA ya ADHUHURI ILIPIGWA SALA YA ALASITI mda huo huo. Mpaka leo huwa najiuliza sipati majibu. Mtoto wa KIGOMA NILIBROO ! kwa watu wa RUFIJI af wana VIBE la hatari unaweza kutorokaka kabla sala haijaisha.
Mpaka leo nimeamua kuishi ki gangstar maana dini zina swaga nyingi sana. Mwaka wa 6 sijatia maguu misikitini.
Hii hasa ndio Aqida yaan khutba isomwe kwa lugha ya kiarabu na kama mhutubu ataweza basi aitafsiri kwa lugha ya waenyeje wapate kujua maana

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Quran haisemi tufuate waja wema,ambao kwa muktadha wa sallafiy na shia ni maswahaba,tabiina na tabi tabiina,quran inataka tufuate yenyewe na imesema 'ni nyepesi kueleweka'..ingekua maswahaba wako sahihi 100% ali na muawiya wasingetofautiana wala kupiganisha vita waislam wakauana kwa maelfu,wajukuu wa mtume hassan na hussein waliendeleza vita na uzao wa muawiya alina yazid,hawa wako kwenye waja wema,lakini hussein aliuawa karbala na waislam(waja wema) wenzie,ndiyo maana quran 3:103 ikatutaka tushikamane kwayo
Acha uongo wewe Qur'an imetaja tuwafanye maswawaba na imewasifu maswawaba na hata ahadu salaafina swalehe wametajwa kama Imran

Acha uongo wewe

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Wacha nikuoneshe aya, wewe unajinasibu kufuata Qur'an pekee ila umenyimwa kuifahamu na kuijua, kwanza unapata wapi guts za kuwasema vibaya watu ambao allah aliwachagua kuishi na mtume wake? unadhani alichagua watu wa ajabu kama unavyotaka kutuaminisha? Qur'an imewasifu mno maswahaba, wao wote ni waadilifu na wanapata na kukosea kama wanadamu wengine.

"Kwa hakika Allah amekwisha pokea toba ya nabii na muharijina na answari, ambao walimfuata katika saa ya dhiki, pale baada ya kukaribia nyoyo za baadhi yao kugeuka, basi akakubali toba yao, hakika yeye kwao wao ni mpole na ni mwenye kuwahurumia."

"Na {amewakubalia pia} wale watatu waliocheleweshewa toba yao, hata ikawa dhiki ardhi juu yao pamoja na ukunjufu wake, na zikawa na dhiki juu yao nafsi zao , na wakayaqini kuwa hapana pa kumkimbia Allah isipokuwa kwake yeye tu, kisha akawapokelea toba yao, ili waendelee kutubia, hakika Allah ndiye Mwenye kupokea toba mwenye huruma."

Qur'an 9:117-118

Unapata wapi ujasiri wa kuyazungumza makosa ya watu ambao tayari allah kishawasamehe?! wewe una uchungu zaidi na makosa yao kuliko mola wao aliyetangaza toba yao kwenye Qur'an? hawa ka'ab ibnu maalik, hilaal ibn umayyah na muraara ibni rabiy'ah hawa walibaki nyuma wakaacha kwenda vitani pasi na udhuru, toba yao imetangazwa kwenye Qur'an pasi na kuficha kitu, Allah awaridhie, wewe ujasiri wa kuongelea habari hizi unatoa wapi.

"Kwa hakika Allah amewaridhia waumini walipokupa kiapo cha utiifu chini ya mti, na alijua yaliyomo katika nyoyo zao, basi akateremsha utulivu juu yao, na akawalipa kwa ushindi wa karibu."

Qur'an 48:18

Uko wapi wewe na aya hizi? kwahyo watu hawa Allah aliwaridhia kwa muda tu, sio? Mimi ushauri wangu jitahidi sana ukae darasani usome, nikitizama post zao unaonekana ni mtu mzima, jitahidi uanze upya jambo hili, na ujiepushe kabisa na heshima za maswahaba wa mtume swala na salaam ziwe juu yake.

Yaliyotokea katika fitan na mtihani yote mtume aliyabashiri akiwa hai, na wao maswahaba wakiwa pembeni yake, ili Allah alihukumie jambo ambalo ilikuwa lazima litokee, hakuna watu bora baada ya mitume isipokuwa ni hawa maswahaba wa mtume swala na salaam ziwe juu yake, ajabu iliyoje kuandika kwa ujasiri kabisa, makosa ambayo allah ameshawasemehe.

Na yule ambaye Allah amemridhia hawi muovu milele.
Huyo punguani hizbi mkubwa

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Sidhani kama kuna mahala nimetaja kuwa wamesamehewa madhambi yao yaliyopita na yaliyotangulia, hili ni khaswa kwa mtume swala na salaam ziwe juu yake, ama maswahaba zake Allah ametangaza waziwazi amewaridhia katika Qur'an na watapata pepo zipitazo mito chini yake, nilikunukulia aya kule nyuma, hayo yaliyotokea baina ya ali na muaawiyah allah awaridhie wote, ni katika mitihani iliyowapitikia waislamu wakati wa kilele chake.

Na hilo halifuti kuwa Allah tayari alishawaridhia na ametaja kwenye Qur'an habari hizo zitasomwa mpaka siku ya qiyamah hazikufutwa, swala linakuja kupigana kumewafanya sio maswahaba wa mtume? ule uswahaba wao na heshima yao imeisha kwasababu hiyo? majibu bila shaka ni hapana kabisa.

Basi kama ndivyo, mengi tu yalitokea baina yao na Allah ametufundisha katika Qur'an tuwaombee msamaha, hili ndilo tuliloamrishwa ama kuzunguka huku na kule kutafuta aibu na makosa yao, ni kutangaza vita na Allah waziwazi, kwani hawa ni watu wameishi na kuinusuru dini hii, kwa mali zao na damu zao, na allah amewasifu kwenye Qur'an kuwa ni watu wakweli!.

"Wapewe pia {mali ya fay'i } mafakiri wa muhajirina waliotolewa majumbani mwao na mali zao kwa ajili ya kutafuta fadhila za Allah na radhi zake, na wanamnusuru Allah na mtume wake, hao ndio wakweli."

"Na wale waliokuja baada yao {maswahaba} wanasema: mola wetu! tusamehe sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu chuki kwa walioamini, mola wetu! hakika wewe ni mpole, mwenye huruma."
Qur'an 59:9-10

Hili ndilo jambo la sawa, ama vita havikubadilisha kuwa mua'awiyah ibnu abiy sufyaan allah amridhie yeye na baba yake kuwa alikuwa mwandishi miongoni mwa waandishi wa wahy, na haibadilishi kuwa ali ibnu abi twaalib allah amridhie kuwa ni mmoja wa makhalifa waongofu, na mmoja katika maswahaba waliobashiriwa pepo wangali hai, bali mtume swala na salaam ziwe juu yake, alitangaza waziwazi kuwa Allah na mtume wake wanampenda yeye, al muhim tuwe makini na heshima za maswahaba hawa watu ni bahari isiyopunguzwa maji yake kwa ndoo ya lita kumi.
Hizo aya unazinasibisha sivyo,unalazimisha yako,ilhali ziko wazi
 
Madhehebu ya hovyo ni haya ambayo hayafai misingi na Aqida za kiislam

1-ahlu shia(sh'ighally)

2-ahlu Sufi(masufi)

3-Ahlu twariqa(wazee wamadufu)

4-Quraniyyu(Hawa wanaamini Qur'an Tu wanafata Ile Aya ya Qur'an inayosema "fabiayy hadithi baghdau yuuminun" )

5-ibadhi( Hawa wapo omani huko)

6-Ahlu shafi( Hawa wanachukua mafundusho ya imam shafii Tu wengine hawataki)

7-tabligh(wazee wa misimamo mikali elimu hakuna)

yapo mengi mno ila misingi na Aqida Bora kabisa ni ahlu Sunna waljamaa

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Wacha nikuoneshe aya, wewe unajinasibu kufuata Qur'an pekee ila umenyimwa kuifahamu na kuijua, kwanza unapata wapi guts za kuwasema vibaya watu ambao allah aliwachagua kuishi na mtume wake? unadhani alichagua watu wa ajabu kama unavyotaka kutuaminisha? Qur'an imewasifu mno maswahaba, wao wote ni waadilifu na wanapata na kukosea kama wanadamu wengine.

"Kwa hakika Allah amekwisha pokea toba ya nabii na muharijina na answari, ambao walimfuata katika saa ya dhiki, pale baada ya kukaribia nyoyo za baadhi yao kugeuka, basi akakubali toba yao, hakika yeye kwao wao ni mpole na ni mwenye kuwahurumia."

"Na {amewakubalia pia} wale watatu waliocheleweshewa toba yao, hata ikawa dhiki ardhi juu yao pamoja na ukunjufu wake, na zikawa na dhiki juu yao nafsi zao , na wakayaqini kuwa hapana pa kumkimbia Allah isipokuwa kwake yeye tu, kisha akawapokelea toba yao, ili waendelee kutubia, hakika Allah ndiye Mwenye kupokea toba mwenye huruma."

Qur'an 9:117-118

Unapata wapi ujasiri wa kuyazungumza makosa ya watu ambao tayari allah kishawasamehe?! wewe una uchungu zaidi na makosa yao kuliko mola wao aliyetangaza toba yao kwenye Qur'an? hawa ka'ab ibnu maalik, hilaal ibn umayyah na muraara ibni rabiy'ah hawa walibaki nyuma wakaacha kwenda vitani pasi na udhuru, toba yao imetangazwa kwenye Qur'an pasi na kuficha kitu, Allah awaridhie, wewe ujasiri wa kuongelea habari hizi unatoa wapi.

"Kwa hakika Allah amewaridhia waumini walipokupa kiapo cha utiifu chini ya mti, na alijua yaliyomo katika nyoyo zao, basi akateremsha utulivu juu yao, na akawalipa kwa ushindi wa karibu."

Qur'an 48:18

Uko wapi wewe na aya hizi? kwahyo watu hawa Allah aliwaridhia kwa muda tu, sio? Mimi ushauri wangu jitahidi sana ukae darasani usome, nikitizama post zao unaonekana ni mtu mzima, jitahidi uanze upya jambo hili, na ujiepushe kabisa na heshima za maswahaba wa mtume swala na salaam ziwe juu yake.

Yaliyotokea katika fitan na mtihani yote mtume aliyabashiri akiwa hai, na wao maswahaba wakiwa pembeni yake, ili Allah alihukumie jambo ambalo ilikuwa lazima litokee, hakuna watu bora baada ya mitume isipokuwa ni hawa maswahaba wa mtume swala na salaam ziwe juu yake, ajabu iliyoje kuandika kwa ujasiri kabisa, makosa ambayo allah ameshawasemehe.

Na yule ambaye Allah amemridhia hawi muovu milele.
Upo sahihi akhy maswahaba wana daraja ya juu sana kwenye Uislam....lakini Qur'an ndiyo muongozo Bora zaidi unaopaswa kufuatwa Kwa kuwa maswahaba licha ya ubora wao lakini ni binadamu na wanafanya makosa.....Kwa mantiki hiyo kuna vizuri vingi vya kujifunza kutoka kwao lakini hawawezi kuwa level moja na Qur'an kama muongozo., na hiyo sio chuki bali ni uhalisia kwamba Muongozo wa kufuatwa muda wote tena usio na Kona kona wala makosa ni Qur'an.
 
Hahaaaaa ati nakufuru,unajua maana ya kufuru!?
Naam. Najua maana ya kufuru. Mimi kwa siku 6 kila wiki nakaa kitako kujifunza dini kwa Masheikh wangu. Umri wangu... Miaka 60. Kikubwa nimekufikishia na kukutahadharisha. Kwako wewe hekima ni kukaa kimya. Na kwa msaada zaidi mtu mzima mwenzangu wasiliana nami kwa Whatsapp 0688999006 nikuunganishe na links mbalimbali za Maduat wa Kisalafi. Elimu sahihi itakuacha huru. Kwa Pamoja tutafute mwisho mwema akhy.

Na kama uko Dodoma basi karibu sn nyumbani ewe Bwana inamankusweke ... Na ulifikiria nini hadi ukajipa jina
Hilo!!! Subhanallah

Hitimisho: Hapa tunajadiliana masuala ya dini na akhy anayejiita inamankusweke. Nasaha yangu ya mwisho kwako... Ewe ndugu yangu ktk Uislam. Badilisha hilo jina lako.
 
Upo sahihi akhy maswahaba wana daraja ya juu sana kwenye Uislam....lakini Qur'an ndiyo muongozo Bora zaidi unaopaswa kufuatwa Kwa kuwa maswahaba licha ya ubora wao lakini ni binadamu na wanafanya makosa.....Kwa mantiki hiyo kuna vizuri vingi vya kujifunza kutoka kwao lakini hawawezi kuwa level moja na Qur'an kama muongozo., na hiyo sio chuki bali ni uhalisia kwamba Muongozo wa kufuatwa muda wote tena usio na Kona kona wala makosa ni Qur'an.
Unamaanisha nini haswa kwa kusema hivi akhy? Tunafuata Quran na Sunnah au Quran tu peke yake kwa sababu haina konakona? Kama unaipinga Sunnah je, ni wapi tunajifunza utaratibu mzima wa Swala? Maana kupitia Sunnah ndio tumejifunza utaratibu mzima wa Swala kwa ukamilifu wake ndugu yangu ktk Uislam.
 
Tunafuata Qur'an na Sunnah,.....nilichomaanisha ni kwamba Qur'an ndiyo muongozo bora zaidi yani imenyooka 100% ,. Maana nje ya hapo lazima utakuta udhaifu wa kibinadamu.,

Siipingi Sunnah, wala sipingi kufuata wema waliotangulia yani ni muhimu mno kwa Muislam, lakini hiyo haiondoi ukweli kwamba Muongozo ulio Bora zaidi usio na shaka kabisa ni Qur'an.
 
Back
Top Bottom