Naomba kuelimishwa kuhusu Shudhuly

Naomba kuelimishwa kuhusu Shudhuly

Masalafi watu wa bidaa tu,kuanzia niqab mpaka kufuata 'waja wema waliotangulia'..unafuata waja wema kama muongozo wakati kuna qur'an!?..kazi ya qur'an ni nini!?
Quran si haijajitosheleza ndio maana kuna hadithi?
 
Duh Mleta mada umenikumbusha kuna mwaka niliingia msikiti mmoja jamaa waliswali rakaa 1 sahihi lakini rakaa zilizobaki WALISWALI WAKIGEUKA KAMA WAJEDA YAANI NYUMA GEUKA, KUSHOTO GEUKA HALAFU KULIA GEUKA KISHA WAKAAA TAHIYATU UKAWA MWISHO WA SALA
 
Mwambie akuelekeze dua ya kulala kma ataikuta kwenye Quran
Ni mtu mjinga peke ake anaekataa elimu ya hadithi
Hapana.

Elimu ya hadithi ina madhaifu mengi sana.

Ujinga ni kuikubali moja kwa moja elimu ya hadithi bila kuipembua.

Kuna hadithi nyingi sana za uongo na zingine zinapingana na mafundisho ya Qurani lakini waisilamu wamezishikilia kwa sababu tu zipo kwenye BUKHARI NA MUSLIM.

Elimu ya hadithi lazima iwafikiane na mafundisho ya Qurani
 
Cc : Kisai
 
Wewe msimamo wako katika hadithi ni upi ?
Wewe unatumia njia gani kuipembua hadith na uhakika hiyo njia Ina uhakika na usalama kiasi gani ?
 
Wewe msimamo wako katika hadithi ni upi ?
Wewe unatumia njia gani kuipembua hadith na uhakika hiyo njia Ina uhakika na usalama kiasi gani ?
Qurani ndio msingi,Hadithi inayoenda kinyume na mafhum ya qurani basi hiyo ni hadithi feki hata kama ipo kwenye vitabu tunavyoviita ni أصح الكتب بعد القرآن (vitabu sahihi zaidi baada ya qurani) yaani bukhari na muslim.
 
Hee kumbe huku nako huwa kuna sintofahamu....watu wanaruka na kukanyagana...
 
Huyo anaonekana haijui elimu ya Hadithi. Anaposema elimu ya Hadithi ina madhaifu mengi sio sahihi kabisa laiti kama angesoma fani hiyo.

Allah ameilinda hii dini kupitia watu wake Salio wateua, ndio maana ukifatilia utakuta hakuna dini nyingine zaidi ya Uislamu wenye elimu ya Hadithi.

Waislamu kushikilia Hadithi za uongo au dhaifu, ni matokeo ya ujinga wao wenyewe.

Ungemuuliza tu akutajie madhaifu ya elimu ya Hadithi, uone kama ataleta hata moja. Ukiangalia yeye ametaja matokeo tu.
 
Quran si haijajitosheleza ndio maana kuna hadithi?
Hakuna hadithi mkuu,na Quran imesema wazi inajitosheleza,hebu fikiria khalifa wa pili ummar ibn uk khattab,swahaba wa mtume alipiga marufuku Hadith,unaamini swahaba anaweza piga marufuku muongozo wa dini(wahyi)?
 
Asalam aleykum.

Leo sala ya Ijumaa nimesali Tabora Msikiti uitwao Shadhuly [ukitamkwa shazli]. Nakili sala yangu ilikua ngumu kwa sababu ya kupishana steps na wenzangu.

1. Rakaa ya pili baada ya kusomwa Surat fattah, kabla ya kusujudu, ikaingizwa maombi, ambao ni utaratibu mgeni kabisa kwangu.

2. Baada ya sala na dua. Nilitaka nifanye maombi binafsi. Ila Dua ile iliendelezwa kwa safu ya mbele kusimama na kutengeneza duara kwa kushikana mikono huku wakiwa kama wanarukaruka very subtly na huku baadhi wakiwa kama wanachagiza kwa kutoa sauti ya juu mithili ya mtu anayekabwa. Nilikosa utulivu hata wa dua binafsi.

wajuzi naomba elimu, hawa ni dhehebu gani? Wanaamini nini?
wewe hujutakiwa kuwafata wafanyavyo,wewe ungesali kwa jinsi unavyosali kila siku na kuondoka
 
Weka hoja zako tuzisome na sisi mkuu inamankusweke
Qur'an inasema mzinzi(bila kujali mwanandoa au laa) akithibitika apigwe bakora mia,hadith zinasema akiwa mwanandoa auawe kwa mawe, Quran inasema kila swala uchukue udhu, hadithi zinadai kama hukujamba basi udhu wa swala ya mchana unaweza utumia mpaka swala ya magharibi, Quran inasema mtoe zakka kila mpatapo faida, hadithi mpaka mtaji uzunguke mwaka bila kupata hasara, Quran inamtaka kila muumini afunge isipokua msafiri na mgonjwa,hadithi zinadai aliye kwenye hedhi asifunge, Quran inasema swala isiwe kimya wala kwa sauti kubwa hadithi swala dhuhuri na alasiri uswali kimya..na mengine mengi,sasa hapo hadithi zinakuongoza au kutoa kwenye Quran?
 
Back
Top Bottom