Naomba kuelimishwa kuhusu Shudhuly

Naomba kuelimishwa kuhusu Shudhuly

Wildlifer

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2021
Posts
1,883
Reaction score
5,270
Asalam aleykum.

Leo sala ya Ijumaa nimesali Tabora Msikiti uitwao Shadhuly [ukitamkwa shazli]. Nakili sala yangu ilikua ngumu kwa sababu ya kupishana steps na wenzangu.

1. Rakaa ya pili baada ya kusomwa Surat fattah, kabla ya kusujudu, ikaingizwa maombi, ambao ni utaratibu mgeni kabisa kwangu.

2. Baada ya sala na dua. Nilitaka nifanye maombi binafsi. Ila Dua ile iliendelezwa kwa safu ya mbele kusimama na kutengeneza duara kwa kushikana mikono huku wakiwa kama wanarukaruka very subtly na huku baadhi wakiwa kama wanachagiza kwa kutoa sauti ya juu mithili ya mtu anayekabwa. Nilikosa utulivu hata wa dua binafsi.

wajuzi naomba elimu, hawa ni dhehebu gani? Wanaamini nini?
 
Bida'a.
 
Umenikumbusha kuna kipindi tulihamia maeneo fulani, ulikuwa mwezi wa Ramadhani mi na mdogo wangu tukasema tukasali sala ya Taraweh!

Tulisali rakah 4 tu tukashindwa tukaondoka! Kila kitu ni kigeni, tukijaribu kujitahidi kwenda nao sawa ikija rakah nyingine inakuja kivingine!

Kwakweli tuliondoka na hatukurudi tena hadi tulipopata msikiti mwingine wenye utaratibu tuliouzoea.
 
Hata nyie pia mnapandisha mapepo kwenye ibada ?
 
Umenikumbusha kuna kipindi tulihamia maeneo fulani, ulikuwa mwezi wa Ramadhani mi na mdogo wangu tukasema tukasali sala ya Taraweh!

Tulisali rakah 4 tu tukashindwa tukaondoka! Kila kitu ni kigeni, tukijaribu kujitahidi kwenda nao sawa ikija rakah nyingine inakuja kivingine!

Kwakweli tuliondoka na hatukurudi tena hadi tulipopata msikiti mwingine wenye utaratibu tuliouzoea.
Aise, poleni.

Sikuwahi tilia maanani tofauti zetu waislam hadi leo. Kwa kweli sala yangu leo imekua bure kabisa.
 
Ukitaka usipate tabu kwenye miji ulizia misikt ya watu wa sunna hasa masalafi utaswali kwa amani kabisa mustarehe ila hao jamaa wengne wao kila mji na taratibu zao ila hao watu wa sunna utaratibu ni mmoja tu dunia yote
Masalafi watu wa bidaa tu,kuanzia niqab mpaka kufuata 'waja wema waliotangulia'..unafuata waja wema kama muongozo wakati kuna qur'an!?..kazi ya qur'an ni nini!?
 
Hao waja wema ni maswahaba na wanafunzi wao, Qur'an imewatukuza kuwatukuza kwa juu, na allah amewasifu, bila wao kutupasia mafundisho hiyo Qur'an ungeitoa wapi.

Watu Allah amewaridhia unasema kuwafuata ni uzushi, uko mzima kweli mkuu.

"Na wale waliotangulia wa mwanzo, katika muhajirina na answari, na waliowafuata wao kwa wema, allah amewaridhia na wao wamemridhia, na amewaandalia bustani zipitazo mito chini yake, hali ya kudumu humo milele, na huko ndiko kufaulu kukubwa."

Qur'an 9:100

Bila shaka hawa ndio walioelewa zaidi mafundisho ya uislamu, ni usalama mkubwa kufuata quran na sunnah kwa ufahamu wao, kuliko kila zama kutegemea ufahamu wake.
 
Umenikumbusha kuna kipindi tulihamia maeneo fulani, ulikuwa mwezi wa Ramadhani mi na mdogo wangu tukasema tukasali sala ya Taraweh!

Tulisali rakah 4 tu tukashindwa tukaondoka! Kila kitu ni kigeni, tukijaribu kujitahidi kwenda nao sawa ikija rakah nyingine inakuja kivingine!

Kwakweli tuliondoka na hatukurudi tena hadi tulipopata msikiti mwingine wenye utaratibu tuliouzoea.
Ishanitokea Lindi hii mwaka 2008
 
Hao waja wema ni maswahaba na wanafunzi wao, Qur'an imewatukuza kuwatukuza kwa juu, na allah amewasifu, bila wao kutupasia mafundisho hiyo Qur'an ungeitoa wapi.
Sasa wanafunzi wa maswahaba wanasifiwaje na qur'an wakati mtume alikua kishafariki!?..miongoni mean hai maswahaba ndiyo wale waliotegea kwenda vitamin qur'an ikawananga,ndiyo wale waliosingizia wanawake wema kuzini quran ikawananga,ndiyo waliopigana vita kugombea madaraka hadi leo ummah umegawanyika na wakauwana,mtume saw aliandikisha qur'an akiwaambia wasome asikie ikiwa walichoandika ndicho alichowasomea
 
Muongozo ni Quran,hayo mengine ni uzushi,ndiyo yanakuja ya kufuga ndevu,usipofuga kafiri,kukata suruali,usipokata moroni,uvae niqab usipovaa upo uchi,wakati hayo yote hayapo kwenye qur'an!!
Muongozo ni Qur an ila unatakiwa kuangalia je hayo mambo yanapingana na Qur an !? Kama hayapingani hamna tatizo na hadithi zipo .

Sunnah sio lazima ila ni bora zaidi ,kwa sababu nje ya kiburi cha binadamu wote mpo sawa ..
 
Ni sahihi kuwatumia kama miongozo ya maisha?
Bila shaka, kwasababu wao wameshakufa na ni watu Qur'an imewasema kwa uzuri sana bali imeamrisha kuwaheshimu na kuwaombea dua, na mtume ametukemea vikali sana kuwatukana na kuwasema vibaya.

Mathalan utapata hasara gani kumsoma abu bakr au umar au uthmaan allah awaridhie wote, utajifunza mengi makubwa na hao ni watu wa peponi kabla hata hawajakutwa na mauti.
 
Back
Top Bottom