Naomba kuelekezwa jinsi ya kufungua non goverment organization (NGO)

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,571
13,399
Habari za mwaka mpya wakuu, bila Shaka ni wazima kabisa wa Afya na poleni kwa majukum ya kila siku.

Katka mizunguko yangu ya hapa na pale Nilipata safari moja ya kwenda Morogoro sehemu moja wanapaita chamwino.
Hali huku kwa kweli ni mbaya hasa utumiaji wa madawa ya kulevya.

Vijana wanajilipua tu hawaogopi kabisa na Bahat nzuri niliweza kuongea nao wengine walisema kuwa Kama watapata msaada bas wanaweza kuacha kabisa.

According to that point ya wao kuacha nikawa nimepata wazo la kuwa mwanaharakati nifungue NGO yangu watu wapate msaada maana nguvu kazi inapotea.

Naomba nisiwachoshe ninachohitaji kutoka kwenu wakuu ni mchango wenu wakunipa jinsi ya kufungua Hiyo REHABILITATION Center naanzia Wapi na ofisi gani?????

Kama kuna watu hapa Moro watapenda kufanya hizo harakati mnakaribishwa.

Nawasilisha hoja wakuu
 
TARATIBU ZA USAJILI WA NGOs CHINI YA SHERIA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGOs) NA. 24 YA MWAKA 2002

Maombi ya usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yatakuwa na viambatanisho vifuatavyo kama ilivyopendekezwa na Sheria hii katika kifungu cha 12(2)

a) Katiba ya Shirika lisilo la Kiserikali
b) Taarifa yenye majina na saini za wanachama waanzilishi
c) Maelezo binafsi ya wanachama na picha
d) Ada ya usajili
e) Anuani na sehemu yalipo makao makuu ya ofisi za Shirika Lisilo la Kiserikali
f) Maelezo yoyote au taarifa kama itakavyohitajiwa na Msajili

Maombi ya usajili wa Shirika Lisilo la Kiserikali yatakuwa kwenye fomu maalum NGO A form No. 1
Maombi ya Cheti cha ukubalifu (certificate of Compliance) yatakuwa na viambatanisho vifuatavyo: -

a) Kivuli halisi cha Katiba ya Shirika Lisilo la Kiserikali.
b) Cheti cha usajili chini ya Sheria nyingine tofauti na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
c) Taarifa yenye majina na saini za wanachama waanzilishi.
d) Maelezo binafsi ya wanachama na picha
e) Anuani na sehemu yalipo makao makuu ya ofisi za Shirika Lisilo la Kiserikali.
f) Maelezo yoyote au taarifa kama itakavyohitajiwa na Msajili.

Maombi ya Cheti cha ukubalifu yatakuwa kwenye fomu maalum NGO A form No, 3.

ADA
Ada ya usajili ngazi ya Wilaya itakuwa ni Shs 41,500/= kama ifuatavyo:
- Ada ya faili 15,000/ =
- Ada ya usajili 25,000/=
- Stamp duty 1,500/=

Ada ya usajili ngazi ya Mkoa itakuwa ni Shs 56,500/= kama ifuatavyo:
- Ada ya faili 15,000/=
- Ada ya usajili 40,000/=
- Stamp duty 1,500/=

Ada ya usajili ngazi ya Taifa itakuwa ni Shs 66,500/= kama ifuatavyo:
- Ada ya faili 15,000/=
- Ada ya usajili 50,000/=
- Stamp duty 1,500/=

Ada ya Mashirika ya Kimataifa itakuwa ni USD 267 kama ifuatavyo:
- Adayafaili US$ 15
- Ada ya usajili US$ 250
- Stamp duty US$ 2

Kila Shirika lisilo la Kiserikali lililosajiliwa na kupatiwa cheti cha ukubalifu chini ya Sheria hii, linatakiwa kulipa ada ya mwaka ya Shs. 50,000/= au US$ 60 kwa Mashirika ya Kimataifa.
Mashirika haya pia yatapaswa kuwasilisha taarifa zake za kazi za kila mwaka (Annual Report) ambazo zitakuwa kwenye Fomu maalumu NGO A Form Na. 10 kwa Msajili Mkuu kupitia kwa Wasajili Wasaidizi.
Mashirika ya Kitaifa na Kimataifa yatasajiliwa moja kwa moja na Msajili Mkuu. Taratibu zake zitakuwa kama zilivyo taratibu za usajili katika ngazi nyingine isipokuwa kutakuwa na tofauti katika ada ya usajili, halikadhalika maombi ya usajili katika ngazi hizi yatawasilishwa moja kwa moja kwa Msajili Mkuu.

MAMBO MBALIMBALI YA KUZINGATIWA
Utaratibu wa malipo ya ada ya usajili/ mwaka

Malipo ya ada ya usajili wa NGOs na ada za mwaka yatafanyika kama ifuatavyo:

(i) NGOs zote zitakazosajili katika ngazi ya Mikoa na Wilaya watalipa fedha katika Akaunti Nambari 16:29 Miscellaneous Deposit (Akaunti hii ni ya Hazina iliyoko kila mkoa) kwenye matawi ya Benki ya NMB katika maeneo yao.

(ii) NGOs zitakazosajili ngazi ya Kitaifa na Kimataifa watalipa fedha zao katika Akaunti Nambari 16:140 Miscellaneous Deposit (Hazina Ndogo mkoa wa Dar es Salaam). Kiutendaji Idara ya Uhasibu, Ofisi ya Makamu wa Rais itapokea fedha hizo na kutoa stakabadhi halali ya malipo hayo.

KWA MAELEZO ZAIDI NIPM NIKUPE FORMAT YA KATIBA INAYOTAKIWA.
Unaweza kusajiri kupitia wizara ya afya, maendeleo ya jamii, wazee, jinsia na watoto au wizara ya mambo ya ndani.
 
Asante Sana mkuu umenisaidia Sana
 
Back
Top Bottom