Naogopa kuoa nifanyeje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naogopa kuoa nifanyeje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ogm12000, Jan 31, 2010.

 1. ogm12000

  ogm12000 JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Hii wana JF

  Umri wa kuoa ndio umewadia ila story za maisha ya ndoa ninavyosikia nakata tamaa kabisa ya kuoa. Nimeona wengi wanatoka nje ya ndoa wake kwa waume, cha ajabu ni kwamba watu kibao wanakuwa wanafahamu kuhusu cheating inayoendelea kasoro mume au mke anaezungukwa.

  Kuwa single bila familia nayo issue!. Maisha ya kudate kama bf and gf ni easy kila mtu anakwao ni easy na matamu lkn nayo yanamwisho.

  Hebu tusaidiane hapo


  Regards
   
 2. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 6,500
  Likes Received: 7,802
  Trophy Points: 280
  Nimekusoma.

  KUMBE unakwepa majukumu na gharama za kuoa.

  Listen, hata GF wako anaweza kuwa anacheat tu kama kawaida.
   
 3. ogm12000

  ogm12000 JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Hamna bwana sinyolita! . Naogopa kuwa na ndoa isiyokuwa na furaha. Vile vile naogopa kuzidiwa kete maana siku hizi mambo yamebadilika.

  Majukumu ni sehemu mojawapo ya maisha hayakwepeki....Aisee yani ukiona watu wanavyozidiwa kete we acha tu.

  Ukiona mmeo/mkeo anapata chance ya kwenda seminar 1 months mkoa mwingine au kampuni imempa scholarship ya kuja kusoma Master n.k jua hapo kuna possibility kubwa sana ya kuzidiwa kete!
  Mambo haya ndio yananiogopesha na sio majukumu..lol
   
 4. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  Binafsi naamini binadamu hupita katika hatua mabalimbali za maisha na kuoa binafsi na kiimani naamini ni hatua mojawapo! Unaposema umeona wengi wanatoka kwenye ndoa ongeza pia kuwa umeona wengi zaidi wakiiingia kwenye ndoa! Ndoa kwa imani yangu ni kusudio la Mungu na mpango maalum ulianzishwa na Mungu mwenyewe! yaani akatiak maagizo yote Mungu alitupatia NDOA ni agizo la kwnza kabisa alilolifanya YEYE MUNGU MWENYEWE! Ukisoma Kitabu kitakatifu cha Biblia; Kitabu cha Mwanzo unakuatana na haya yote! Hakumtuma nabii kuifanya ndoa; Aliiumba apale alipobaini kuwa Baba yetu Adamu alikuwa ni pweke na akajisemea yeye nafsini mwake kuwa Na tutmtengenezee mwenza; amabaye ni Hawa.

  Tukirudi kwenye wasiwasi wako; kwanza ni mapokeo ya binadamu na kauli mbaya kabisa ni ile isemayo Ndoa ni mahali ambapo waliondani wanatamani kutoka na walio nje wanatamani kuingia! Hii ni kauli ya kushindwa na si ajabu woga wako umo kaika hili; unaogopa kushindwa!

  Nakushauri kwanza upate wwasaa wa kujifunza nini maana ya ndoa; jifunze pia namana ya kuishi na mwenzio utakapokuwa ndani ya ndoa kwa kuzielewa tofauti zenu maana hakika nyie ni watu tofauti; achana hadithi za kisasa za eti hobbies zenu zinaendana; nazungumzia tabia zenu! baada ya hapo uwe tayari kumpenda na kumsamehe mwenzio! Ukifanya haya na maandalizi mengine ndoa yako itakuwa ya furaha!
   
 5. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  Ukimpenda mwenzio kitu cha kwanza kufanya ni kumwamini; usijitoe kinusunusu kwani ndivyo hata yeye atakavyokufanyia; mathalani kama hapa akijua kabisa wewe unamuwekea asilimia 50 za kumegwa atamegwa akijua hata asipomegwa wewe nafsini mwako unajua kuna kitu kinaendelea; ki ujumla unaku wewe ndo umempleka kwenye dhambi!

  binafsi unatuhakikishieje kuwa wewe hakuna possibility kubwa ya kumega nje wakati yeye yupo masomoni? Mifan hai tunayo; mama kasafiri masomomoni anajibana huko anarudi anakuta baba amezaa na nyumba ndogo!
   
 6. ogm12000

  ogm12000 JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Thanks ndugu yangu kwa mawazo mazuri.. Nitayafanyia kazi.
   
 7. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,795
  Likes Received: 1,430
  Trophy Points: 280
  In order to get something you dont have, u must do things u have never done before - by sinyolita.

  Usiogope ww oa tu! Mambo mengine utadeal nayo mbele.
   
 8. y

  yegomwamba Member

  #8
  Jan 31, 2010
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Nakushauri ukaoe mwanawane manake maisha ya kukaa na bf and or gf is nat so good given that the so called Aids is spread all over the world.why afread of getting marriege?if you are an impotent one please be open so that jf members could help u
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Mlume kamata mke. Maisha ya ndoa ni kama maisha mengine tu, unahitaji kujitune ktk rhythm hiyo na mambo mengine yote yanakuwa mswano.

  Kuwa na familia kuna advantages kuliko disadvantages. Mojawapo ni kuwa tunahitaji kama taifa, utuzalie watoto na kuwatunza vyema wewe ukishirikiana na mkeo. Taifa linahitaji uhai.
   
 10. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu karibu katika ulimwengu wa waliooa, usikimbie challenge kaka zikabili tu, si ndoa zote zinakosa uaminifu. Oa Mpende Mkeo, mjali, mtimizie kila kitu kwa uwezo wako kama atakuwa ni muelewa hawezi kwenda Nje.
   
 11. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Umewahi kuiba mke wa mtu? kama ndivyo nawe utaibiwa tu ukioa. Kama ulishaiba mke au mpenzi wa mtu, hiyo kumbukumbu haitakutoka hivyo ni vile umebeba bomu. Amua kukubali kuibiwa.

  Kama hujawahi iba usiogope kwa huo mzuka wa kuiba hautakusumbua sana kichwani, na itakuwa rahisi kwako kuamini mwenza wako, popote pale utakapokuwa.

  Kumbuka pia wanawake ni watu wa siri sana, na wanachofanya ni kusoma tabia yako ili kuweza kudeal na wewe. Akigundua kuwa wewe ni mwizi, au umeshawahi kuwa mwizi, au umeshawahi kuuvunja moyo wa mtu, atakuwa na wewe for the sake kwamba ameolewa na ana mume (wanawake wanapenda sana kuolewa), lakini kumoyo, kwamba anakupenda 100% na kwamba hata cheat, ni kubahatisha tu.
   
 12. ogm12000

  ogm12000 JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  lol.. Kumbukumbu zangu hazionyeshi kama nimewahi kuiba mke wa mtu. Umeongea ukweli ni kupiga moyo konde na kuingia ktk maisha ya ndoa na kuona itakuwaje. Thanks kwa ushauri
   
 13. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,284
  Likes Received: 758
  Trophy Points: 280
  Kuoa si lazima jamani, kama hautaki kuoa usioe. Haya mambo ya kulazimisha ndo yanawatokea puani akina Tiger Woods, bora angekuwa single kusingekuwa na tatizo kabisa.
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Jan 31, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 77,846
  Likes Received: 39,867
  Trophy Points: 280
  Mimi nasema usioe wala nini. Kwa nini uji set up kuja kuvunja au kuvunjwa moyo hapo baadae? Ukioa utakuwa unajiingiza kwenye matatizo tu. Kama vipi wewe zaa tu na huyo demu wako na utakuwa na familia. Hakuna kitu chenye raha hapa duniani kama kuwa na amani kichwani mwako na hakuna kitu kibaya kama kuishi na wasiwasi kuwa mkeo atakuibia. Sasa shida yote hiyo ya nini?
   
 15. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,734
  Likes Received: 251
  Trophy Points: 180

  ...kama unaogopa unataka kujipa shida za nini? ama weye?!
   
 16. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #16
  Feb 1, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,469
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mke akimegwa nje inauma zaidi kuliko GF!!
   
 17. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #17
  Feb 1, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kwa taarifa yako, kati ya ndoa 100, huenda ni 3 tu ndio hudmu kuwa salama kwa mwezi, (japo ni hisia tu). Yaani hizo zingine zote, kwa mwezi zinakuwa aidha mmoja au wote wametoka nje ya ndoa ndani ya mwezi. Hivyo, habari ndio hiyo, kama hutaki kuoa, hulazimishwi, acha.
   
 18. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #18
  Feb 1, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  uwezi kukwepa majukumu ktk maisha na ukifanikiwa kukwepa majukumu utakwepa matokeo kama kuoa tabu basi jaribu kuolewa
   
 19. f

  furahaeliud Member

  #19
  Feb 1, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu kinachokusumbua saana sana ni hofu, maisha ya ndoa ni kama maisha ya kawaida tena ukioa matumizi ndio yanapungua kabisa huwezi amini, usiwe na hofu na wala usisikilize kelele za mashabiki, sio ndoa zoote zinamatatizo kikubwa muombe mungu akupatie mkwe wa chaguo lako then ukishamuoa mpende mvumilie mjali basi, mwanamke kikubwa anataka kuona unamjali na kumpenda basi it wont cost u
   
 20. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #20
  Feb 1, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 6,500
  Likes Received: 7,802
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Yeye kasema anaogopa kuoa kwa vile watu wanatoka nje ya ndoa - kumega/kumegwa nje.

  Sasa, unless ana sababu nyingine, swala la kufyatuka nje lipo pale pale tu, hata kwa GF. Ni tabia tu
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...