nani wa kulaumiwa?

Luv kama huyo dada mwenyeji wa Tanga au kusini i mean Lindi na Mtwara p'se ni PM.

ni mtoto wa kinyaki, kaenda hewani! nina hakika ukimuona utataharuki....ngoja nifanye mpango wa kuku2mia pic yake...ule kwa macho.
 
...alivyorudi home mume akataka unyumba mke akamwambia mie kwangu ni laki kwa bao, mume akajua dili limebumburuka wakagombana vibaya na mume akakiri kweli alifanya hivyo na akaahidi kumwacha huyo kimada,

....mke hataki kumpa mpaka na yeye alipwe laki kwa bao, jana frnd ananical ananiambia wametengana na mr wake kwa kisa hiki mana mr wake anasema wife anamdharau na wife anasema "ulianza wewe mie namalizia"......nani wa kulaumiwa?......

...aaah, laki tena ya nini wakati alishatolewa mahari yake bana?
 
ni mtoto wa kinyaki, kaenda hewani! nina hakika ukimuona utataharuki....ngoja nifanye mpango wa kuku2mia pic yake...ule kwa macho.

Hahahahaha duh haya luv tuma sijawahi ona toto la kinyaki twiga na sijawahi ona toto la kinyaki white dah ngoja nilicheck labda ni mixer huyo chotara.
 
Basi kama lengo ni hilo basi kawin shost wako maana hapo the game is over-

ameshamkalisha chini sana tu kwa kweli na mie mwenyewe nikiwa shahidi....mdada ana akili ya maisha sana na mie mwenyewe nikamwambia hii rafu kwa ninavyokujua umeicheza ili ndoa ife kibudu, akaniambia ni kweli yaani nimetafuta kitu ambacho ctaki 2je aniombee msamaha wa kurudiana wala nini na hata akienda kuwaelezea ndugu zake nao wamwonye kunirudia....

Ndoa yao ni ya kanisani au kwa mkuu wa wilaya?na kama ni kanisani wakati wanakalishana chini kuna mzee wa kanisa padri au askofu aliyehusishwa au walikuwa wakilkalishana baa?

Kingine ni kweli waliowana kwa mapendo au walipeana mimba na kulazimishana kuoana?

Je vipi kabla ya kuoana walikutania kwenye matendo wayafanyao kwa sasa ya baa hotelini au kwenye matamasha?
 
Ama kweli MTENDA..HUTENDWA.!
MWanaume ndio wa kulaumiwa kwani yeye ameanza kuivuruga ndoa mpaka akili ya mke nayo imevurugika hivyo ameamua kumalizana kibingwa watoto wamjini wanaita NIPE NIKUPE.
 
wote wawili ni wa kulaumiwa,
Swadakata!

kinachomuumiza zaidi ni kwamba yeye akipata tatizo na kumuomba mr wake msaada huwa hapewi au ama ni laki atapewa 30 au 40 huo ni mfano tu lakini nje anatoa 30 kwa bao na maelezo ya mdada wa saloon jamaa anaenda bao 3, so ni 90 wakati yeye pesa ya mr wake anaickilizia bombani.....
Kweli huyu ni mume au mfano wa mwanaume?

Mjinga mwambie watu hawaendi hivyo lazima ajichunguze kwa nini mmewe anakubali kutoa elfu 30/= kwa bao? Basi anapata kitu adimu kutoka kwa huyo dada wa saloon.
Fidel... hivi ndugu yangu mnajua maana ya ndoa?..kulikoni uoe halafu uje ufanye vituko hivi? Ina maana ukiwa na visenti vya kubadilisha mboga wewe unabidilishia wanawake? hilo bao au sijui mabao ni nini kwa maisha yako? Mtu mwenye uchu namna hii ni hatari kwa maisha!

dada huyo wifi yetu kwa nini amekubali kulipiza katika mapenzi? angekaa na mumewe amweleze yote anayoyajua kisha aulize mapungufu yake
Mj1.
Uonavyo huyu bwana ni wa kushauriwa? Nakataa hili lka kusema ati kila mara mwanamke mumeo akitembea nje basi wewe ndio ujilaumu na kujiuliza una mapungufu gani?! Akha babu! yeye ndio ana mapungufu na bila shaka wanawake wangestahili kuwahoji hao mabwana kujua upungufu wao unaowapelekea hadi kujidharaulisha kila kona ya mji.Ona mdada wa saloon alivyokuwa anamuongelea upungufu wa akili wa kulipa 30,000/-kwa bao!

nilivyoona mie mdada alikuwa anatafuta njia ya wazi wazi ya kuachana na mumewe, mana wamevumiliana kwa mengi, ndoa ikiwa na mwaka jamaa alikutwa mchana na mkewe wakijivinjari chumbani kwa house gal, mdada alihuzunika sana akaombwa msamaha yakaisha, baada ya muda kidogo akackia jamaa ana mrembo na ana mimba, hajakaa sawa anaambiwa jamaa anatembea na sekretari wake, mara mrembo wa saloon, naona akayajumlisha akaamua na kutoa hapo hapo....

Huyu bwana ana pepo chafu linalostahili kuombewa! Kutembea na mmoja tungesema bahati mbaya shetani kampitia... sasa na hausgeli, sekretari, dada wa saloon, na huyo aliyempa ujauzito! Kweli anastahili kushtuliwa kwa shock therapy kiaina!Huenda sasa atajifahamu upungufu alio nao ajirekebishe.

ameshamkalisha chini sana tu kwa kweli na mie mwenyewe nikiwa shahidi....mdada ana akili ya maisha sana na mie mwenyewe nikamwambia hii rafu kwa ninavyokujua umeicheza ili ndoa ife kibudu, akaniambia ni kweli yaani nimetafuta kitu ambacho ctaki 2je aniombee msamaha wa kurudiana wala nini na hata akienda kuwaelezea ndugu zake nao wamwonye kunirudia....
Ama kweli ndoa inaweza kumfikisha mtu pabaya kumgeuza malaika akawa shetani lucifer!

Ila mwisho napenda kusema kuwa ndoa siyo lelemama... watu wanapitia mengi wameyaweka vifuani mwao.Ukiona mtu hadi anafanya hiki alichokifanya huyu dada - basi ujue yamemfika ya kumfika!
 
Ndoa yao ni ya kanisani au kwa mkuu wa wilaya?na kama ni kanisani wakati wanakalishana chini kuna mzee wa kanisa padri au askofu aliyehusishwa au walikuwa wakilkalishana baa?

Kingine ni kweli waliowana kwa mapendo au walipeana mimba na kulazimishana kuoana?

Je vipi kabla ya kuoana walikutania kwenye matendo wayafanyao kwa sasa ya baa hotelini au kwenye matamasha?

ndoa ni ya kanisani, mdada jana ananiambia amejichokea, na hana muda wa kwenda kwa wazazi mana ndoa ni ya wawili na yamemshinda basi anawaachia wanaoweza,hajaolewa na jamii na wala hatajali jamii itamfikiaje mana shida anazipata yeye na sio jamii..... walizoeana bank, mambo ya kwenda bank kiofic ndio yakaanzisha uhusiano, na uchumba wao ulikuwa wa miaka 2 kabla ya ndoa, wakati wa uchumba niliona kila mtu anampenda/thamini/jali mwenzake, kweli mapenzi yao yalikuwa moto moto....
 
Hahahahaha duh haya luv tuma sijawahi ona toto la kinyaki twiga na sijawahi ona toto la kinyaki white dah ngoja nilicheck labda ni mixer huyo chotara.

haaa luv black is beauty....utamkubali walaah
 
Huenda kweli institution of marriage katika zama za leo inahitaji overhaul.Hakuna mahali utasikia watu hawalalamiki kuhusu ndoa.Ukienda Ulaya na Marekani talaka ndio usiseme.Asia wahindi nao wana makasheshe yao hadi kuchomana moto wakiwa hai.Huku Afrika nako hatujatulia.Watu wanajifanya all is well lakini hamkani si shwari tena.Ukiangalia chanzo cha matatizo mengi ya ndoa ni kukosa uvumilivu, kutokuridhika na ulie naye, kutokutosheka na ulicho nacho.Vile vile kuingia kwa vionjo vipya katika kila nyanja - mavazi, mapambo ya mwili, mridhishano vyumbani, mashindano ya kipuuzi,kutokujali wengine watasema nini, kutokuona aibu wala soni, ukatili na roho mbaya, kukosa huruma, kutokujali, n.k.Technolojia nazo zimerahisisha mambo - simu za mikononi zinafanya iwe rahisi watu kutongozana, mitandao nayo inarahisisha mawasiliano, usafiri, - yote haya ni matokeo ya utandawazi!KAZI IPO!

Enzi za zamani ilikuwa kazi kweli kufanya vituko kwa maana ungeonekana uko tofauti na binadamu wa kawaida.Ila kwa siku hizi ni kawaida ni maendeleo.Ukitendwa nawe unatenda mechi inatoka droo! NGOJA TUONE ITAISHIA WAPI.
 
Hii ndoa haikuwepo in the first place.....kwa maoni yangu haikumaanishwa waishi pamoja..wote mwanamke na mwanaume wana makosa as far as the marriage institution is concerned. Kilichopo, maadamu ushahidi wa kuzini upo, basi wafate taratibu waiterminate hiyo ndoa tu....
 
na wengi huchukulia hicho kigezo cha uvumilivu kuumizana. Simply because tunatakiwa kuvumilia basi hawa wenzetu huamua kufanya ya kufanya ili tuvumilie. Fakoff uvumilivu my foot
 
Kaka kaizer yaani kusema ukweli unapoamua kuoa huwa mnachagua mwanamke ambaye mnajua fika anakufaa sasa atakapobadilika anza kwanza kujichunguza wewe penmgine ndio chanzo

Mimim ninakueleza nimeshaingia dhambi ya kuwaza kucheat mara kibao na si kwa sababu simpendi laaziz wangu nampenda sana na ndio maana nikaghairi but matendo yanapelekea kuwaza vinginevyo

Ninafeel kabisa yalomkuta shogake nyamayao
 
na wengi huchukulia hicho kigezo cha uvumilivu kuumizana. Simply because tunatakiwa kuvumilia basi hawa wenzetu huamua kufanya ya kufanya ili tuvumilie. Fakoff uvumilivu my foot

Kuna imani inasema "watu wangu wanaangamia kwa ukosa maarifa"...sidhani kuna binadamu aliumbwa kwa kuumia kwa ajili ya mwingine.Huenda labda ni wazazi tu na hasa mama ndio wanapaswa kuumia kwa ajili ya mtoto na hata hivyo the rewards are plenty.Mwana atampenda mama yake siku zote.

Je mwanamke unapooumia kwa ajili ya mume unapata reward gani? Iweje mume akutese na kukuumiza mara kwa mara? ni kuwa hana roho ya utu? Kama ameshajitwika roho ya mnyama isiyoingiwa na huruma, kuna haja ya kuumia kwa ajili yake ili iweje? Hivi ni kwanini baadhi ya wanaume wanaendekeza sana vitendo vya mara kwa mara vya kuumiza wake zao kama huyu ndugu anayezungumziwa hapa? Kama kutendwa ni kubaya iweje wanaume wanawatenda wanawake kila leo? wanavyoumia wakitendwa wajue wanawake nao huumia ivyohivyo.Wakiona wanawake wananyamza na kuvumilia basi wajiulize hivi inakuwaje? food for thought! mwenye uerevu aelewe.
 
Mtendwa naye katendwa. Hawa wote wanamakosa hakuna hata wa kulaumiwa. Ama kweli ndoa ndoana. waliopo nje wanatamani kuingia, waliopo ndani wanatamani kutoka.
 
Back
Top Bottom