Nani Naibu Katibu Mkuu CHADEMA mtarajiwa?

Nani Naibu Katibu Mkuu CHADEMA mtarajiwa?

Hiyo nafasi ameililia lema sana..... ili team uchaga ikamilize Lema aitwae nafasi
 
Hivi ndivyo chama kinavyopaswa kutenda. Lazima watu waheshimiane na kufuata taratibu za chama ili kufikia malengo. Kuoneana haya na kuogopana ndiko kulikoifikisha ccm ilipo leo. ccm igeni mfano huo mkiwachekea watu kwaajili ya umaarufu wao na fedha mtapotea 2015. viongozi hawawezi kuishi kama familia ya kambale baba, mama na watoto wote wana sharubu. Wasaliti na wanaotanguliza maslahi binafsi wawekwe kando makamanda wanaotafuta ukombozi wa wengi wasonge mbele. Katika vita lazima kuwe na wasaliti, majeruhi na waliokufa. Watakaosalimika wataleta ukombozi, wasaliti waadhibiwe
 
Acheni kutaja majina badala yake tutaje sifa za kiongozi anayefaa kwa nafasi hiyo!majina sio hoja kwa sasa!
 
Anayeandaliwa kuwa naibu ni John Mnyika na ndio maana yote haya yakafanyika.huu ni mkakati kabambe kwa uchaguzi huu ndani ya chama.kama huamini subiri.
Uchaguzi haukucheleweshwa bure.siku zote Dr slaa amekuwa akimwachia mikoba Mnyika badala ya naibu wake na hii Zitto anaijua fika.
Ila tusubiri tuone lakini binafsi bado namuamini sana Zitto kwasababu sio kiongozi wa briefcase kama wengine
ZZK anaaminiwa sana CCM. Anafaa kuchukua nafasi ya Nape.
 
acha uzuzu, sio mambo ya chadema sema mambo ya wachaga.
"......pumbaaaaf......."



wewe kweli una akili??? Sababu mtu mwenye kuhubiri udini na ukabila ni wa kuogopwa kama ukoma,,,,tadhali jirekebishe ili nisikuogopeeee.
 
maandalizi ya kumrithisha mchaga chama baada ya mbowe imeshaanza, katika list yako umemueka lema kama choice ya kwanza, na sijui umetumia veting system gani, kwani huyu mwizi wa magari hawezi kuwa katika ligi moia na hao wasomi watatu wengine. Chadema kinaharibiwa na kimejipiga risasi ya miguuni kwa maamuzi mabaya

hata ningemuweka wa mwisho ,usingekosa neno la kuongea . Lakini jua hata nchi haiongozwi kwa makabila,acha ulimbukeni wa mambo. Ww kuna gari gani lema alikuibia ,au alishawahi jaribu kukuibia ? Au kuna pending kesi yeyote inayomkabili Lema mahakamani kuhusiana na wizi wa magari .?
 
Baada ya kupatikana kwa taharifa za Mh ZITTO KABWE Naibu katibu wa CHADEMA kuvuliwa vyeo vyote ndani ya chama na kupewa siku 14 kuandika maelezo ya kwanini asifukuzwe uwanachama, watu mbalimbali nikiwemo tumefurahishwa sana na uwamuzi huu.

Kwanza ni ukweli usio na mashaka kwamba Mh Zitto kwa muda mrefu sasa amekuwa akitajwa na kuhusishwa mara nyingi na mipango yake ya kukivuruga chama kwa maslahi yake binafsi na waliomtuma.

Chama kimemvumilia muda mrefu bila kumchukulia hatua za kinidhamu na badala yake kilimuonya. Ni huyu huyu Zitto ambae leo wana CCM wanampigania kwa nguvu zote kuwa Mwenyekiti wa Cdm Taifa anajiita Mpinzani huku ikionekana wazi kuwa tangia 2008 Zitto amekuwa Cdm kimwili ila Kifikra yupo Ccm.

Haiingii akilini Viongozi wa CCM kuwa Wazungumzaji wa Zitto ndani ya CDM huku tukijua wazi kuwa "Adui"wa CDM sio CUF,wala NCCR isipokua ni CCM.
Ikiwa wana CCM wanadhani kuwa Cdm hakuna Demokrasia kwa kukataa kumpa mtu wao nafasi ya kuwa kiongozi mkuu,si wamuite kujiunga na Ccm au wamshauri kwenda CUF,au NCCR ambako kunaonekana kuna demokrasia!?

Natoa ushauri kwa viongozi wangu Wakuu wa CHADEMA, mh Mbowe na Dr Slaa. Kwanza kutakuwepo na kelele nyingi za wale Wahafidhina na Mamluki kwa kufukuzwa au kufutiwa vyeo mnafiki na Msaliti no 1 Zitto Zuberi Kabwe!
Hili lisiwatishe kwa kuwa naamini wakati mnachukuwa uwamuzi huu Mgumu,yote haya mlijua.
Chukueni tena muda mfupi na kimtangaza Professa SAFARI kwamba ndie Naibu Katibu Mkuu sasa. Hii itasaidia Chama kuendelea kuaminika na Wanachama.

Professa Safari anaweza kuvaa viatu vya Zitto na ni Mwanamageuzi asiekuwa na Makuu,asieyumbishwa na Upepo wa pesa kutoka CCM na ni kiongozi Msomi asie na Majivuno wala Kujikweza na sio hivyo tu lakini pia ni Mwanasheria aliebobea. Kwa sifa hizi kedekede ninaamini Proffesa ANAWEZA!!!!!

MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!!!!
MUNGU IBARIKI CHADEMA!!!!!!
 
Sidhani kama Prof. Safari atakuwa rahis ku-deal naye kuliko Zitto. Sioni kivipi pro. Safari atakubali kutawaliwa na wakina Lema, Kilewo and co.!
 
Back
Top Bottom