Mimi nafikiri kila mtu atatoa opinion yake kutegemea na aina ya muziki unaomgusa....anayependa kitimtim na hekaheka anaweza kuangukia kwa akina Rose. Anayependa muziki wa kusifu na kuabudu anaweza kurudi kwa akina Muhone na Shusho (and the like)...
Kwa wataalamuRose Muhando? Bahati Bukuku? Christina Shusho? Bonny Mwaitege? Upendo Nkone? Jennifer Mgendi? Beatrice Muhone? Ambwene Mwasongwe? Martha Mwaipaja? Flora Mbasha?.............
Na hapo ndio Shusho anaponimaliza, hatoki jasho! Vijana wa mjini wanasema "mdogo, mdogo" lakini ujumbe unakuingia kumoyo. Soul soothing....
Watu8 kumbe na wewe umo, kiukweli nyimbo zile zilikuwa zinakosha, unajua zilikuwa zinakosha kiasi kwamba kwa wakristo wachanga kama sisi unakuta unapata mafundisho na visa za kwenye biblia.
Ila Shusho na Upendo Nkone ni kiboka maana pamoja na kwamba hawaimbi zile nyimbo za kutumbuiza (entertaining) za kuruka huku na kule lakini bado wakiimba unawasikiliza mpaka mwisho
New Life Band, Ulyankulu Barabara ya 13...
Hao wengine wote uliowataja ni wafanyabiashara nyuma ya nyimbo za injili...
Kha! Mkuu hebu tuache wenzako. Upako hatuna basi hata kufurahia nyimbo na kukiri kuwa kwa hakika wenzetu hawa wana upako nako tushindwe. Upako ungekuwa lotion walahi kila mtu angekuwa nao:wink2:Jamani Acheni Ushabiki, huwa mnasikiliza izo nyimbo? ni zipi zenye upako zaidi? maana huwez kuwa na nyimbo nzr kama ww mwnyewe haupo vzr kiroho, sawa?
Aisee ni kweli maana wengine kweli wanaambia na wana pumzi hasa ya kuimba lakini ile nyongeza ya kucheza nayo inawafanya wanoge ila huyu yeye ni mdogomdogo kama unavyosema lakini naye yumoNa hapo ndio Shusho anaponimaliza, hatoki jasho! Vijana wa mjini wanasema "mdogo, mdogo" lakini ujumbe unakuingia kumoyo. Soul soothing....
Mie huyo mama alinikamata na ule wimbo wake unaoenda kwa jina la usifurahi ndugu yangu... ujue kwa maombi yako mimi nitasimama tena..Huyu mama naye huwa ananikosha mno...
Nilimfahamu kupitia wimbo wake mmoja anaelezea kuwa pasipo maono watu wanaangamia...
Baadaye akatoa wimbo wake wa "Yesu ni wa rehema"...
Bila kumsahau Abiud Misholi
New Life Band, Ulyankulu Barabara ya 13...
Hao wengine wote uliowataja ni wafanyabiashara nyuma ya nyimbo za injili...
These are the best, jamani New life band imekwisha wamebaki watatu tu wale wa zamani, nilikuwa nikiwaona sana kny semina ya mwakasege wakiongoza sifa ila sidhani kama hivi karibuni wametoa
St. Joseph Arusha ni hatari, Watu8 amefunga orodha, ila kuna Ulyankulu wengine inaitwa mapigano kama sikosei, waliimba Mwenye Mamlaka. Hawa watu walikua wanaimba neno ndio maana nyimbo zao hazitakaa zichuje wala kuchosha kusikiliza.
Kuna Nkinga Christian Choir na Kilimanjaro Revival nao wanajitahidi.
Kwa ufupi, iwe ni kwaya au mwimbaji binafsi au kikundi, wakiimba neno na sio hizi nyimbo za maneno ya msimu, utagusa watu tu kwa nja moja ama nyingine.
Umeongea kweli,sijawahi kuona Kama ulyankulu barabara ya 13,nyimbo zao zinagusa,wamevaa kiheshima,nyimbo za nyingi zinaendana na maandiko,nawakubali Sana aisee