MKWAWA LEAF YAWAKOMBOA WAKULIMA WA TUMBAKU
Kampuni ya Mkwawa Leaf Tobacco imeshusha neema kwa Wakulima wa Tumbaku nchini, Kampuni hiyo inatojishughulisha na Ununuzi wa Tumbaku nchini imeungana na Sera ya Serikali ya Kilimo katika Kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hasan kwa kuhakikisha wakulima nchini wanawezeshwa ili kufanya kilimo chenye tija na faida kwa Wakulima.
Akizungumza Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ndugu Ahmed Mansoor Huwel ambaye pia ni mmiliki wz Kampuni ya Uchakataji wa Tumbaku ya Amy Holdings.
Ndugu Huwel alisema "Huu ni wakati sahihi wa kufufua zao la tumbaku na kulipa thamani, Ni wakati sahihi wa ushindani wa kibiashara ili kuweza kulipa thamani zao hili la Tumbaku na kuwanufaisha wakulima moja kwa moja ambao wao ndio wadau wa kwanza wa zao hili. Kupitia kampuni yangu Tanzu ya ununuzi wa Tumbaku ya Mkwawa Leaf, Nimeamua kuanza kuwawezesha wakulima, Mbegu bora ya Tumbaku pamoja na Mbolea ili kuweza kufanya kilimo chenye faida kwao.
Uwezeshwaji huu haumpangii mkulima soko la kuuza Tumbaku, Mkulima ataamua ni nani wa kumuuzia Tumbaku. Ila ninahakikisha kuwa Kampuni yangu ya hii itatoa ofa nzuri kwa wakulima tofauti na kampuni nyingine ili kuweza kununua tumbaku kwa wakulima kwa bei nzuri kwao." Alisema Ahmed Huwel
Hata hivyo kampuni ya Amy Holdings ni kampuni inayomiliki kiwanda cha Tumbaku kilichopo Mkoani Morogoro ambacho kipo katika mkakati wa kuhakikisha kinaongeza uzalishaji wa tumbaku nchini na kuwa kiwanda kikubwa cha Tumbaku nchini.
Vilevile Huwel aliongeza kwa kusema anaamini kuwa na ushindani ni afya, kwani kunapokuwa na ushindani kunakuwa na afya kwa wakulima wengi.
Aidha, alisema kuwa lengo la kuinunua kampuni hiyo ni kuwasaidia watanzania ili kuwanyanyua kiuchumi.
“Shida kubwa waliyopitia wakulima wa Tanzania ndio hasa iliyonisukuma mimi kuweza kununua hiki kiwanda ili kuwasaidia na kuwakomboa wakulima wenzetu wa nyumbani.” Amesema Huwel
Hata hivyo waziri wa Kilimo Mheshimiwa Husein Bashe alinukuliwa akiwaeleza wakulima wa Tabora kuhusu Kampuni ya Mkwawa Leaf kuwa Tayari kununua Tumbaku kwa wakulima kwa Bei nzuri, Huu ni mwanzo mzuri kwa kampuni hii kwa Wakulima wa Tumbaku.