Nani katudanganya lazima nchi iongozwe na wanasiasa kwa mfumo wa vyama au wafalme au ma-chief?

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
14,727
Reaction score
37,028
Kwa hasira sana natafakari ni kwanini tume block uwezo wetu wa kufikiri.

Kwanini tuna kariri ni lazima tuwe na ma-vyama ya kichawa- chawa na wanasiasa- waongo waongo ndiyo watuongozee nchi yetu

Sehemu nyingine wanakua na familia fulani inawatawala bila ukomo, ata kama hao watu ni ma-kenge au matahaira.

Mimi nasema hivi, sioni ufanisi wowote wa kuendesha nchi kwa mitindo hiyo ya kale.

Nataka, tutafakari model za uongozi za kisasa,

Tunaona makampuni makubwa yenye mafanikio na ufanisi mkubwa sana. Kwanini tusiiweke nchi yetu kwenye hiyo mifumo.

Kuna watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri watabisha.
 
Tumefungwa akili kwa mazoea na hila za kisiasa kiasi kwamba tumekuwa tukiamini mfumo wa “vyama vya kisiasa” na “wanasiasa waongo” ndiyo njia pekee ya kuendesha nchi. Hii ni upuuzi mtupu.

Mfumo wa vyama vya siasa mara nyingi hauzalishi viongozi bora, unazalisha watu wachache wenye uwezo mkubwa wa kutapeli akili za wengi. Wanaweka hoja dhaifu, ahadi za uongo, wanatengeneza miungano ya kifisadi, halafu wananchi wanabaki na umasikini na mateso.

Kuna sehemu nyingine duniani zimejenga mifumo ya kifamilia, urithi wa kifalme au madikteta wasio na mwisho – nao pia mara nyingi huishia kwenye kuendeleza ujinga, kwa sababu damu ya kifalme au urithi wa ukoo sio kipimo cha hekima wala uwezo wa kuongoza.

Kuhusu makampuni makubwa ya kisasa. Ukiangalia Google, Apple, Toyota, au hata kampuni kubwa za ndani Afrika, zinaendeshwa kwa ufanisi kwa sababu ya mifumo ya utawala wa kibiashara . Zina bodi za wakurugenzi, zina performance evaluation, zina strategic planning, na kila mtu anapimwa kwa matokeo. Hakuna nafasi ya “nina chama” au “nina ukoo” ..... hapo ni matokeo tu.

Sasa kwanini tusibuni mfumo wa nchi unaoendeshwa kwa mantiki hiyo? Taifa liwe kama shirika kubwa:
  • Wananchi wawe wanahisa .
  • Serikali iwe kama board of directors.
  • Viongozi wawe wanachaguliwa kwa competence na track record, sio kwa ahadi tupu au damu ya kifamilia.
  • Matokeo yapimwe kwa uchumi, elimu, afya, teknolojia, siyo kwa idadi ya mikutano ya kisiasa au maneno ya majukwaani.
Kama tungekuwa serious, tungeachana na huu usanii wa kisiasa wa kale, na kuingia kwenye mfumo wa ufanisi – mfumo wa kitaalamu unaofanana na namna makampuni makubwa ya kimataifa yanavyosimama na kustawi.

Wale wenye uwezo mdogo wa kufikiri watabisha, kwa sababu tayari wamezoea kufungwa kamba shingoni na vyama vyao vya kichawa-chawa. Lakini ukweli hauwezi kufichwa kwamba ufanisi upo kwenye mifumo ya kisasa, sio siasa za kizembe.
 
Umefanya uchambuzi makini sana

Nadhani tunatakiwa kufanya kitu

Siyo mbaya tukiwa taifa la kwanza kwenda kwa style tofauti

Kitu cha msingi ni ufanisi
 
Hata mimi siamini hii mifumo ya kiasa , imeletwa na wazungu mpaka leo ni tatizo ...Yaani wasomi wanataka demokrasia ya kupiga porojo na kuzalisha motivational speakers , waongo waongo ...Siasa mbaya sana.

Nchi inatka maendeleo sio kusifia wanawasiasa.
 
Inatia hasira sana, imagine product za mifumo ya kisiasa ni watu kama Baba Level na makenge mengine huko majimboni.

Wengi wa wagombea hawawezi ata kuwa shortlisted mfano hizo nafasi zingekua zinapatikana kwa ushindani (competitive selection)
 
Unaona hasara hiyo kwa sababu Tanzania haijawahi kuwa na mifumo ya utawala kupitia vyama vya siasa , iliyopo ni geresha tu .
 
Mkuu mada ni nzuri, lakini hebu utuambia kwanza wewe unafikiri huo uongozi utakuwaje.?
Nchi itaendeshwaje.
 
Nadhani ata kwenye sehemu ambazo tunadhani mifumo ya kisiasa imefanikiwa, bado hakuna meaningful contribution kwenye society. Bado kuna watu homeless, mifumo ya afya siyo rafiki, matatizo ya kijamii bado ni lukuki
 
Mkuu mada ni nzuri, lakini hebu utuambia kwanza wewe unafikiri huo uongozi utakuwaje.?
Nchi itaendeshwaje.
Nimetafakari model ya makampuni, yale makampuni yaliyofanikiwa, ambayo yanafanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
 
Back
Top Bottom