Nani Kasema Tibaijuka Kafukuzwa Uwaziri ?

Nani Kasema Tibaijuka Kafukuzwa Uwaziri ?

Hapo ndipo utakapokumbuka Wakenya wanavyoshangaa Watanzania wanavyokwenda dukani na hela zao halafu wanasema "naomba..."

Ustaarabu unapotaka kufunika maana unageuka kuwa ukungu usiotakikana.

Rais Ali Hassan Mwinyi alisema ombi la mkubwa ni amri.

Lakini hata yeye alipochoshwa na baraza lake alilifukuza na kuacha kazi za mawaziri zifanywe na makatibu wakuu wa wizara, March 6 1989 for you younguns.
 
Mzee Mwanakijiji waungwana walisema hivi YOUR WISH IS MY COMMAND. kama dada yangu Profesori anashindwa kuelewa hata hilo basi hata aliemteua naye ana matatizo. Na kwa hali hio Anna anaweza popote na akabaki kuwa hana hatia
 
Last edited by a moderator:
Waandishi wa habari wengi walikula mgao wa ESCROW!
 
Hapa mnatulete spinning and twisting tu.
Hizi ni porojo tu , Tibaijuka is out. Period.
 
Siyaamini maneno ya jk hata siku moja hata jana sijaamini alichokisema Rais ni bingwa wa kuingiza watu mjini kama mnafikiri ni utani waulizeni ukawa habari wanayo
 
Hapa hatuchezi na semantics tu kweli?

mwanzoni nilifikiria hivyo; Rais hajawahi kuwa na utata katika kutengua uteuzi wa mtu. Huwa wanasema tu "Rais ametengua.." halafu kama kuna nafasi itajazwa basi anasema imejazwa au watajaza nafasi hiyo later. kwenye hili hakuna dalili kuwa Rais alimaanisha kuwa tangu dakika ile nafasi ile iko wazi. Hivi kuna ugumu gani kujaza nafasi ile tena mtu mmoja tu? kwanini kuchezea maneno?

Rais anaomba kweli mtu aliyemteua awapishe; akigoma?

Binafsi naamini kuwa Tibaijuka atatoa statement ya kujiuzulu baada ya kutafakari ombi la Rais... then it'll be official. Baada ya X'mass
 
Hapo ndipo utakapokumbuka Wakenya wanavyoshangaa Watanzania wanavyokwenda dukani na hela zao halafu wanasema "naomba..."

Ustaarabu unapotaka kufunika maana unageuka kuwa ukungu usiotakikana.

Rais Ali Hassan Mwinyi alisema ombi la mkubwa ni amri.

Lakini hata yeye alipochoshwa na baraza lake alilifukuza na kuacha kazi za mawaziri zifanywe na makatibu wakuu wa wizara, March 6 1989 for you younguns.

exactly; binafsi sioni kulikuwa na ugumu gani kwa Rais kusema tu "nimetengua uteuzi wa Waziri ..... na nimteua ndugu so and so kujaza nafasi yake" period.
 
exactly; binafsi sioni kulikuwa na ugumu gani kwa Rais kusema tu "nimetengua uteuzi wa Waziri ..... na nimteua ndugu so and so kujaza nafasi yake" period.

Kikwete anakiogopa kivuli chake mwenyewe.

Anataka kutembea lakini anahofia kukikanyaga kivuli chake.

Atatembeaje sasa? Matokeo ndo hayo anatoa tepid statements full of timid and pale overmeasurements.
 
mwanzoni nilifikiria hivyo; Rais hajawahi kuwa na utata katika kutengua uteuzi wa mtu. Huwa wanasema tu "Rais ametengua.." halafu kama kuna nafasi itajazwa basi anasema imejazwa au watajaza nafasi hiyo later. kwenye hili hakuna dalili kuwa Rais alimaanisha kuwa tangu dakika ile nafasi ile iko wazi. Hivi kuna ugumu gani kujaza nafasi ile tena mtu mmoja tu? kwanini kuchezea maneno?

Rais anaomba kweli mtu aliyemteua awapishe; akigoma?

Binafsi naamini kuwa Tibaijuka atatoa statement ya kujiuzulu baada ya kutafakari ombi la Rais... then it'll be official. Baada ya X'mass

Anamuonea huruma Mama Tibaijuka, hawajakutana njiani, wanajuana tangu JKT Ruvu 1972.
 
Rais anaomba kweli mtu aliyemteua awapishe;

Lakini wengine wanaweza kusema kuwa (rais) alimwomba (Tibaijuka) atumikie hiyo nafasi.

Kama ombi la bosi ni amri, atagomeaje ombi la bosi wake?

Haitakuwa insubordination hiyo?

Mimi nadhani ni suala la semantics tu kwani mwisho wa siku Tibaijuka hataendelea kuwa waziri.
 
Muhongo alichimba mkwara kuwa ikiwa watamfukuza uwaziri basi patachimbika, na kweli JK amemgwaya
 
exactly; binafsi sioni kulikuwa na ugumu gani kwa Rais kusema tu "nimetengua uteuzi wa Waziri ..... na nimteua ndugu so and so kujaza nafasi yake" period.

Mimi nadhani labda wewe binafsi ungependa tu kusikia rais akiyatumia maneno hayo.

Lakini mwisho wa siku ukiangalia, matokeo yatakuwa yale yale tu.

There is always more than one way to skin a cat, my friend!
 
Hapa haihitaji akili kubwa kutafsiri,yaani mtoto akijisaidia hata kama hajasema na unaona choo utaendelea kusema hajanya kwa sababu hajasema??ongezeni uwezo wa kufikiria. Hapa tujadili kwa nini sio wengine na iwe Anna??
 
Tibaijuka kageuka kuwa mhanga mkuu.....ajabu sana.....alafu tunashangilia!!!!
 
Point hapa kuwa kama Rais au kama wewe ni kiongozi; chukua hatua kama kiongozi. Huna ulazima wa kumung'unya maneno. Vinginevyo unaonekana dhaifu na usiyependa kuonekana mkali.
 
Lakini wengine wanaweza kusema kuwa (rais) alimwomba (Tibaijuka) atumikie hiyo nafasi.

Kama ombi la bosi ni amri, atagomeaje ombi la bosi wake?

Haitakuwa insubordination hiyo?

Mimi nadhani ni suala la semantics tu kwani mwisho wa siku Tibaijuka hataendelea kuwa waziri.

Mkuu iweje mamlaka kuu ya nchi imuombe mwajiriwa wake narudia tena imuombe mwajiriwa wake ajiondoe? Huu ni udhaifu wa hali ya juu, sikutegemea lugha kama hiyo kutoka kwa mkuu wa nchi na hasa an ex army commander. Hiyo lugha hatujaisikia kwa Nyerere, Mwinyi wala Mkapa. Mzee Mrema alitimuliwa na mzee Mwinyi na hakuombwa ajiondoe. Awamu hii ya uongozi imetia fora kwa maajabu.
 
Back
Top Bottom