Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,240
- 44,481
WAkati mwingine Watanzania tunasoma zaidi ya kile kilichosemwa au kuandikwa na kutoka huko tunafikia mahitimisho yetu sisi wenyewe. Wote waliopata nafasi ya kusikia hotuba ya Rais Kikwete wanajua kwa uhakika kuwa hakusema amemfukuza kazi au amemuondoa Uwaziri Anna Tibaijuka. Anasema "walimwomba" lakini hakutuambia kama alikubali au bado anafikiria. Inaonekana kana kwamba wamempa nafasi Tibaijuka kutangaza kujiuzulu nafasi yake badala ya kumfukuza.
Kitu ambacho hadi hivi sasa hatujui kwa uhakika ni kama baada ya kuombwa Tibaijuka amekubali au la. Kwa sababu kama angekuwa amekubali Rais angekuwa amefanya mabadiliko ya baraza la mawaziri na hata kututangazia huyo "mwingine" ni nani. Kwa vile Tibaijuka hajakubali ombi la Rais na kwa vile Rais hajatangaza mbadala (replacement) ya Tibaijuka inashawishi akili kuwa Anna Tibaijuka bado ni waziri akiendelea kutafakari ombi hilo la Rais.
Nani anabisha?