Mbunge yeyote wa CCM hataingia bungeni kufanya mambo yaende sawa. Wanaingia bungeni kudumisha utamaduni wa kulindana tu. Angalia msuguano kati ya wapiganaji na mafisadi. Nani aliyeshinda?Nyani Ngabu natamani ungekutana na dada huyu ukamuona ni msomi wa kutosha. Watanzania wanahitaji wasomi kama Angela wawe bungeni kusaidia baadhi ya mambo ambayo hayendi sawa. Tumpe muda bunge litazinduliwa November utaona mambo yake...kwa nini uandikie mate ili wakati wino upo..? Ukiwa huko Atlanta marekani, ni vigumu kumfahamu huyu dada, mpe muda tu. Naamini utakuja omba msamaha hapa hapa baada ya kuona mambo yake
Hapo kwenye nyekundu unamwaribia na sio kama unavyodhania una unamtetea.Ni vyema tukakumbuka kuwa Angela Kairuki hii si mara ya kwanza kugombea ubunge. Aligombea 2005 na wakati huo wala hakuwa Vodacom. Sasa mbona kipindi kile hamkuona uhusiano wa Angela na mafisadi akina Rostam..? Hii ni maraya pili amejaribu na amekubalika kachagulika tena kwa kura nyingi sana. Napenda mfahamu taarifa hizi badala ya kumhusisha dada wa Watu na mafisadi. Wagombea waliofadhiliwa na mafisadi kwanza wengi walianguka vibaya sana. Wapo ambao walipewa fedha waende kwenye majimbo kama ya Mzee wetu Mpendwa Samuel Sitta lakini wameanguka ile mbaya.
WOS SIO kama watu wanaongea umbeya, nadhani pamoja na mapungufu ya hiyo Lugha lakini kikubwa, watu wanachokiongelea kuwa huyo mtu anaingia kwenye Bunge na Pia Uwaziri (Wizara ya Mama Six) kwa kupitia migongo ya watu, kuanzia kwa mama yake Ester Mkwizu na Rostam Aziz pamoja na Ngereja, tunasema ni kupendelewa mbona wakina Nape wanaangaika wenyewe kwa nguvu zao?
HApa hakuna majungu bali tuaangalia jinsi kikundi cha watu kinavyokuwa na uwezo wa kustructure uongozi wa nchi hii
kama vijana tunaotegemewa na taifa la kesho tunaongea pumba zote hizo kweli bado hatujakomaa kisiasa, hivi kwa nini hatuthubutu kuhoji nani huyu Zainab Kawawa ambaye CV yake by far amezidiwa na Angela na hana long experience kwenye ufanyakazi je huyu mnamwona anafaa? Bahati ya mtu msiilalie mlango wazi angela kapeta muhimu nasisi tutafute ni jinsi gani 2015 tunaweza kuwa wabunge
Mbona mnamuandama Anjela? Mmewahi kujiuliza Maji marefu atawawakilishaje wananchi wake? Na wengine wote ambao ni darasa la 7 au mnaosema wana elimu ndogo.
deisykama vijana tunaotegemewa na taifa la kesho tunaongea pumba zote hizo kweli bado hatujakomaa kisiasa, hivi kwa nini hatuthubutu kuhoji nani huyu Zainab Kawawa ambaye CV yake by far amezidiwa na Angela na hana long experience kwenye ufanyakazi je huyu mnamwona anafaa? Bahati ya mtu msiilalie mlango wazi angela kapeta muhimu nasisi tutafute ni jinsi gani 2015 tunaweza kuwa wabunge
kama vijana tunaotegemewa na taifa la kesho tunaongea pumba zote hizo kweli bado hatujakomaa kisiasa, hivi kwa nini hatuthubutu kuhoji nani huyu Zainab Kawawa ambaye CV yake by far amezidiwa na Angela na hana long experience kwenye ufanyakazi je huyu mnamwona anafaa? Bahati ya mtu msiilalie mlango wazi angela kapeta muhimu nasisi tutafute ni jinsi gani 2015 tunaweza kuwa wabunge
deisy
Join DateThu Aug 2010
Posts1
Thanks : 0
Thanked 0 Times in 0
Nina shaka kuu juu ya usemayo. Hayo maneno yenye nyekundu inaonyesha jinsi gani watanzania wengi tulivyo rahisi kununulika au kutumika kama "bendera fuata upepo". Kama hujui leo huyo mwenzio ameingiaje huko Bungeni, utaweza kujua hiyo 2015???.
Lakini pengine shida ni kuelewa hoja au labda kama umejiunga kwa kazi maalumu ya kujibu tu kwa maslahi binafsi ambayo yanapingana na mawazo ya wengi.
Kwanza ieleweke kuwa kila huwezi kuwachangua wote walioteuliwa kwa mara moja. Mada nyingine zilishaletwa na zitaletwa kuhusu hao ambao hawajaguswa hapa.
Pili, kinachozungumzwa ni kuwa "hawa watu wa jinsi hii hata huyo Kawawa wanaenda huko Bungeni kuwakilisha maslahi ya nani ikiwa wamebebwa na hata hilo kundi wanalodai kuingizwa (Wafanyakazi) lingekuwa ndilo linapiga kura kitaifa kupitia shirikisho lao (TUCTA) kupata mtu wa kuwawakilisha lingehoji uwezo na ufahamu wa watu kama hawa juu shida za wafanyakazi wote wa Tanzania.
Kumbuka ni miezi michache tu iliyopita, Serikali ya CCM kupitia Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Nchi yetu ilisimama na kuwabeza hadharani wafanyakazi na kutoa matamshi wa kashfa dhidi ya Uongozi mzima wa TUCTA...Je, unadhani watu kama hawa ambao wanagushwa kwa karibu na viongozi wakuu wa CCM na watoto wa vigogo wanaweza kupigania maslahi ya wafanyakazi huko Bungeni kama si dangaya toto??.
Jiulize ikiwa huyu mbunge mtarajiwa ana wasifu ambao una mawaa (kuhusu kazi anayofanya sasa na ofisi aliyopo), unadhani kuna kitu hapo kama si kupachikwa tu ili yatimie maandiko?.
Twaelewa kuwa Ubunge hauihitaji elimu ya juu sana na hata ukiwa na Phd. bado haimaanishi uwezo wako wa kuelewa mambo upo juu..lakini wasifu wa masuala ya kijamii na hasa kundi unaloliwakilisha ni muhimu sana katika kunagalia iwapo mhusika anauwezo unaolingana na nafasi aliyopewa..Kumbuka, kukaa kazini kwa muda mrefu hakumaanishi wewe unauzoefu wa matatizo ya wafanyakazi wengine ambao umewakuta au watakuja baada yako.
You and your rinky dinky "lawyer' can kiss my ass....
There is no need to kiss your beautiful Ass my friend, huna hoja,,, nenda mitandao ya shigongo ndio size ya mind yako,, useless