Kuhusu Angela Kairuki,, Naona kuna watu wanajidai wanamfahaaamu,, eti kwa vile uliwahi kufahamiana nae kwenye Kitchen party au Harusini,, tena inawezekana mlikua mshalewa serengeti za moto maana hamna kumbukumbu vizuri..
Nimefika sehem nimeanza kuona kwamba "Tatizo sio CCM wala serikali, tatizo ni watanzania wenyewe".. Maana minds zetu zimekua too much limited na zimekua zikiongozwa na jinsi magazeti yanavyoandika.. Thats a shame players... Inabidi tuanze kubadilika sisi wenyewe na badala ya kuchambua watu tuchambue maswala.. Kwa mfano NYANI NGABU ambaye amemcriticise sana bibi ANGELA ningemuona anabusara endapo angechambua miswada au sheria ambazo bi Angela alishiriki kuziandaa na kuziandika... hapo ndio nitakuona kweli umeelimika na una ujuzi wa sheria.. kuliko kukosoa English yake.. Ukienda Uingereza wapo waingereza wenye miaka 60+ wamezaliwa uingereza lakini ukiwaambia waandike kwa mfano barua kwa kiingereza itakua taabu.. sembuse bi angella,, halafu wewe mfa kunoga ndio unajidai unaijua ngeli,, check your self na hivyo viji vocabularly useless, eti sijui ili tukuone umesoma sana... he he he
Lakini cha msingi ninachojaribu kukisema,, hata kama CCM watawapitisha "Maimartha wa Jesse na Benny Kinyaia" kua wabunge, mie hilo halinihusu kwa sababu halina madhara kwenye maisha yangu ya kila siku.. Ila kama watapandisha bei za mafuta, au kodi, hapo sasa ndio nitaanza kuangalia kwa nini wanafanya hivyo na sitamshambulia yule aliepandisha hivyo vitu, bali nitaangalia takwimu na umuhimu kwa nini imekua hivyo.. thats how great minds operate,,sio tunakalia eti ooh huyo kaletwa na mafisadi, ooh huyo,, damn guys lets be serious
Washiriki wenzangu wa hapa Jamii forums, tunaelekea uchaguzi mkuu, nawaomba tugraduate kwenye lile kundi la "huu mtandao ni wa watu wenye "Small Minds" who are 100% motivated to discuss people.. Ni wakati wa kuchambua sera moja baada ya nyingine,,hilo ndio zuri na litakua na tija kwetu, watanzania wote na kizazi kijacho,, Otherwise tupigeni kelele ila Bi Angella teyari ashaingia bungeni na "She's better than you, and there is nothing you can do about it" take that
Asalaam aleykum