WOS SIO kama watu wanaongea umbeya, nadhani pamoja na mapungufu ya hiyo Lugha lakini kikubwa, watu wanachokiongelea kuwa huyo mtu anaingia kwenye Bunge na Pia Uwaziri (Wizara ya Mama Six) kwa kupitia migongo ya watu, kuanzia kwa mama yake Ester Mkwizu na Rostam Aziz pamoja na Ngereja, tunasema ni kupendelewa mbona wakina Nape wanaangaika wenyewe kwa nguvu zao?
HApa hakuna majungu bali tuaangalia jinsi kikundi cha watu kinavyokuwa na uwezo wa kustructure uongozi wa nchi hii
Ajifunze kuandika basi, sio anajiaibisha kwa maswala madogo yanayoonyesha uvivu na uzembe, wengine watamuona a semi literate nincompoop without a econd glance.
Web image ni kitu muhimu sana, she should know that.
Kama ma lawyer wasomi wenyewe ndio hawa, we really need that Cultural Adjustment Programme.
Naamini kabisa ukikubali kuwa katikati hutaangaika sana na uwezo wa huyu dada kushindwa kuandika kiingereza, utaangalia zaidi uwezo wake na kumpa nafasi ya kuthibitisha elimu yake kwa vitendo.
Kama hayo maandishi ni yake kweli basi kwangu mimi keshashindwa kuthibitisha hiyo elimu yake inayodaiwa kuwa anayo.
Na ni bora aende huko bungeni kwa vilaza wenzake kuliko ku practise law....lawyer gani hajui hata kuandika? Syntax mbovu, punctuation hovyo, diction isiyoeleweka.....lawyer gani huyu?
Ni vigumu sana kuingia kwenye mambo ya siasa Tanzania bila support ya namna fulani.Iwe ni kupitia wazazi, ndugu, jamaa au marafiki, ndivyo hali ilivyo.Huyu dada apewe nafasi kuonyesha atakachowezesha kufanya badala ya kumchambua kama karanga hapa. ( Najua kuna watu wako stand-by kunijibu kwa mashambulizi yasiyo na lazima). Tujiulize swali moja tu: Hivi tukimchambua kuwa ati mama yake anahusiana na wanasiasa wa Tz, Mumewe ni mwanaye marehemu Dr Kairuki, mara ohh ni mwanasheria na mfanyabishara, yote haya yatamzuia kuingia mjengoni? Jibu is so obvious- a resounding NO! Why waste energy and time gossiping about her ( yes it is gossip coz its small talk which is unproductive!).
Tumeshamjua "mbunge mtarajiwa" viti maalum vya wanawake CCM kuwa professionaly ni mwanasheria, pia ni mjasiriamali, ni mke wa mtu, she is young- inatosha.
Mzimu wa Ufisadi ulilipotezea taifa muda wa miaka mitatu bila kujadili mambo ya maendeleo, nashangaa kwamba leo bado mjadala ni RA. We are wasting our precious time kumjadili mtu ambaye kama si mungu kuamua, hakuna litakalobadilika.
Moods, Ni vizuri mada ziwe zinafungwa ili kuendelea na maisha. Topic yoyote yenye neno ufisadi au RA nashauri isipite kwani inatupotezea muda. Kama kungekuwa na manufaa basi wananchi wa Igunga wangemkataa lakini ni kinyume chake.
Respect
Kaka Hebu nenda Wizara ya sheria tafuta miswaada ya sheria aliyoandika huyo dada ili utoe hukumu yako juu ya writting skills zake...au ukitaka nenda kwenye firm yao pale umpatie kazi ashindwe ndio ujithibitishie kama hana uwezo...la sivyo kwa sasa utaishia ku speculate tu...
WoS:
Support ya namna fulani ndiyo ipi? Huyu binti namfahamu vizuri - Hana mchango wowote anaoweza kuupeleka bungeni kusaidia kutetea haki za Wafanyakazi wa Tanzania - Hajui Wafanyakazi wa Tanzania wana matatizo gani - Nimeshekaa naye meza moja tukala tukanywa na kuongea - Upeo wake ni mdogo sana - Yes I mean it! Nafasi wapewe wenye kuonyesha japo uwezo wa kuchambua masuala to a certain degree!
She has reached so far kwa "kubebwa" - she can not stand on her own feet!
Ni makosa kusema inatosha, wakati huyu ni mbunge mteuliwa kupitia viti maalumu - hatuna sehemu ya kumuhoji atatufanyia nini - huyu hatafanya kampeini - anasubiri kuapishwa TU - Sehemu pekee ya yeye kuelewa nini tunahitaji kutoka kwake ni maeneo kama haya - Tukinyamaza na yeye atanyamaza!
I am a million times better than she is on anything you can imagine therefore I won't waste my time....
If you think you a million times better than she is....then wewe ungetufaa BUNGENI...ninashauri Ukagombee ili ulisaidie taifa. Angalizo, ukienda huko, usiendeshe mambo kiubabaishaji kama hivi unavyofanya uchambuzi pasipo kuwa na data kamili na kutegemea circumstantial evidence .... tabia za aina hii...ndio zinalipeleka taifa letu pabaya....supposedly, wewe na watu wa aina yako ndio wasomi wetu wenye kujiamini uwezo wao.
WOS SIO kama watu wanaongea umbeya, nadhani pamoja na mapungufu ya hiyo Lugha lakini kikubwa, watu wanachokiongelea kuwa huyo mtu anaingia kwenye Bunge na Pia Uwaziri (Wizara ya Mama Six) kwa kupitia migongo ya watu, kuanzia kwa mama yake Ester Mkwizu na Rostam Aziz pamoja na Ngereja, tunasema ni kupendelewa mbona wakina Nape wanaangaika wenyewe kwa nguvu zao?
HApa hakuna majungu bali tuaangalia jinsi kikundi cha watu kinavyokuwa na uwezo wa kustructure uongozi wa nchi hii
Mkuu hakika nakubalina nawe 100%. Kuna watanzania wamepoteza kabisa mwelekeo wa kutojitambua kutokna na kushambuliwa na chembechembe za "itikadi, dini, rangi, kabila, tabaka, na hata jinsia!".
Ndio hawa wanaofikia kushindwa kuona hatima yao na watoto wao kwa misingi tu ya kutetea/kupinga jambo ambalo dosari yake inaonekna kwa macho na akili ya kawaida ya mtu.
Haya mambo kujuana na kubebana ndio yameipeleka nchi yetu hapa ilipo na unashangaa hao hao watanzania washindwa kuona matabaka yanayojaribu kutengenezwa katika mfumo wa uongozi wa nchi hii.
Labda tufike wakati tukae kimya tukiamini kuwa "wenye nacho wataongezewa na wale wasio nacho, hata kile kidogo watanyang'anywa".
Hivi kama mfumo tunaoenda nao ni huu wa watoto wa "wakubwa na wenye nazo" kupasiwa kamba na wazazi wao ili waendelee kutawala wale walio masikini, mnadhani mnajenga jamii ya jinsi gani hapo?....Mpime kwa mizani sawa, hivi hawa wabunge walioteuliwa wakitajwa kuwa wanawakilisha makundi fulani (ikiwemo) kundi la wafanyakazi, ni kweli wamepitishwa kwa kuzingatia vigezo sahihi na wanasifa zinazohitajika kuwakisha kundi husika au wamepitishwa kwa kuwa tu wana nguvu ya kiuchumi ndani ya jamii yetu???
Tusizungumzie ushabiki wa itikadi zetu na jinsia katika masuala yaliyo wazi !!
Vuteni taswira ya miaka ishirini ijayo hii nchi itakuwaje, Je, watu kama akina Mizengo Peter Pinda wanaojiita sasa "Watoto wa Wakulima" watathubutu kusimama???.
Je, ikiwa mafisadi papa ndio waliowasimika viongozi wenu madarakani, mnatarajia watoto wenu watathbutu kusimama kupingana na maovu yeyote?.
YAPO MENGI MAGUMU YANAKUJA MSIYOWEZA KUYATABIRI SASA!!!
Wakati tunaiangalia Tanzania yetu katika scope ya miaka mitano au kumi, mafisadi wameshapiga darubini na kuangalia vipi watasalimika miaka 20-30 ijayo. Ndiyo maana sishabikii akina January Makamba kugombea ubunge Bumbuli, au huyu binti tunayemjadilia hapa kupewa nafasi ya ubunge. Mafisadi wameshajipanga. Wanaandaa watu wao kuchukua nafasi za ubunge kulinda madhambi yao katika miongo ijayo na sasa hivi wana harakati za kuhakikisha CCM inasalimika katika uchaguzi mwaka huu na 2015. Kuna kijana mmoja mtangazaji aliajiriwa na VOA mwaka jana. Ameondoka bila kuaga kwa sababu amegombea ubunge huko kwao, na kapitishwa na CCM lakini kafadhiliwa na Manji. I happen to know the young man, hana ideology, hana vision, lakini anafikiria tu shillingi millioni 12 na zaidi atakazolipwa kama mbunge, na kwa bahati aukwae unaibu waziri. Hii ni anatomy ya kuendelezwa kwa utawala wa kifisadi Tanzania. They are already looking and planning ahead.