VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Chama cha siasa ni ubunifu. Ubunifu ulio maarufu. Kubuni ni jambo moja,kufanikiwa ni jambo lingine. Kubuni ni kuonesha uhai wa fikra za viongozi na wanachama wao. Kubuni nako ni siasa.
Kati ya vyama vya siasa hapa nchini,CHADEMA ni wabunifu. Ingawa ukweli huo unaniuma hata mimi,sina budi kuusema. Ili nipate amani. Ni wao waliobuni operesheni mbalimbali za kichama. Ni wao waliotaja elimu bure na vita dhidi ya ufisadi kwa mara ya kwanza.
Wengi tumenufaika na ubunifu wao. Wengi tumeshughulika na mambo yao. Mwanzoni,nilidhani think-tank wao ni Dr. Slaa. Lakini,pamoja naye kuwaacha mkono ubunifu unaendelea. CCM tumechoka kukopi na kupesti. Tumechoka kudandia kwa gia hoja. Tumsajili think-tank wao atusaidie.
Ubunifu wao,kwakweli,unasumbua. Tuchangamke wasitufunike!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam