Nani hasa ni 'think-tank' wa CHADEMA? Anapaswa asajiliwe CCM

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,800
Chama cha siasa ni ubunifu. Ubunifu ulio maarufu. Kubuni ni jambo moja,kufanikiwa ni jambo lingine. Kubuni ni kuonesha uhai wa fikra za viongozi na wanachama wao. Kubuni nako ni siasa.

Kati ya vyama vya siasa hapa nchini,CHADEMA ni wabunifu. Ingawa ukweli huo unaniuma hata mimi,sina budi kuusema. Ili nipate amani. Ni wao waliobuni operesheni mbalimbali za kichama. Ni wao waliotaja elimu bure na vita dhidi ya ufisadi kwa mara ya kwanza.

Wengi tumenufaika na ubunifu wao. Wengi tumeshughulika na mambo yao. Mwanzoni,nilidhani think-tank wao ni Dr. Slaa. Lakini,pamoja naye kuwaacha mkono ubunifu unaendelea. CCM tumechoka kukopi na kupesti. Tumechoka kudandia kwa gia hoja. Tumsajili think-tank wao atusaidie.

Ubunifu wao,kwakweli,unasumbua. Tuchangamke wasitufunike!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Think tank wa CCM ni kina Bulembo na Mgeja na Lusinde....

Sasa wamesajili timu mpya ya Mpendazoe...

Usitegemee jipya hapo, kwa resources walizo nazo kulinganisha na CHADEMA wangetakiwa kuwa mbali sana, lakini ndio hivyo tena wamewekeza kwenye matumbo badala ya kichwani.
 
CHADEMA Wangekuwa wabunifu wangeshinda Uraisi.huwezi sifia kuwa timu fulani ni timu bora wakati haifungi magoli wala kutwaa kombe lolote kutwa ni kushuka daraja.
Usiseme kombe lolote,tumekosa ligi kuu tu ila mengine tumebeba!Angalia kwa mara ya kwanza majiji mengi yanaongozwa na upinzani
 
CCM sijui kama huwa inajua maana ya kushinda. Maradona aliwafunga uingereza bao la Mkono linalowauma sana waingereza mpaka leo, hapa kwetu Nape naye akasema wapinzani watafungwa bao la Mkono, maana yake nini? Bao la Maradona lilikubaliwa na Refa na likahesabiwa kuwa ni bao, lakini mpaka leo sidhani kama walioona Maradona akifunga kwa mkono badala ya mguu wanalikubali lile bao kama ni "halali" ila waajentina wana mpaka dini ya kuabudu bao lile.
 
Ukweli mchunga asante mzee tupatupa kwa kulijua hilo, ukweli ni kwamba operation UKUTA imefanikiwa kwa 85% kabla ata ya tarehe moja, ccm imeshindwa kujua mtego wa chadema, nao ccm ikaingia miguu miwili na matokeo yake ujumbe wa maudhui yamefika kwa wananchi bila ata maandamano wala mkutano wa siasa, ikumbukwe kuwa nia na mazumuni ya UKUTA ni kuwafikishia wananchi kile ambacho Chadema wanakiamini kuwa mkuu wa kaya anavunja katiba ambayo alihapa kuitetea na kuilinda.

Kwa minajili hiyo CCM wakaingia kichwa kichwa kupambana na ukuta, kwakuwa ndio chama tawala imepelekea vyombo vya dola asa polisi nao kuingia kichwa kichwa kupambana na UKUTA, na matokeo yake wao ndio wakawa wasambazaji wa UKUTA uku wakisahau kuwa UKUTA ni idea ipo vichwani, UKUTA sio maandamano bali ni fikra ambapo uwezi kuzitoa kichwani kwa mtu ,ila maandamano yaliwekwa ili zile idea zipate kuwafikia wananchi as the result ccm imejikuta ikiitangaza UKUTA bila kujijua, nachelea kusema kwamba UKUTA imefanikiwa kwa 85% kabla ata ya tarehe moja.

UVCCM wamestukia hii wakati ni too late, ndio mana na wao wakatangaza maandamano mwisho wa mwezi huu.

Kwa minajili hiyo na ni ukweli usiopingika chadema kuna great thinker wanaotumia akili za juu kufikili kisiasa kuliko chama tawala, natambua kuwa chama tawala kuna wasomi wengi kuliko chadema, je wapo huru kushilikisha akili zao na zikafanyiwa kazi?
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom