Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Haya mafuta mengi alijipaka siyo ili asizame bali ajikinge na baridi. Kwa wataalam wa haya mambo wanakwambia baridi ni kati ya vitu vya mwanzo vitakavyochukua uhai wako hata kama u mtaalam wa kuogelea.
Na inawezekana alitafuta na sehemu ya kujishikiza walau waokozi waweze kumkuta hai.
Huyu kazama majini asubuhi bna usitudanganye
 
Kivuko wakati kinatengenezwa kiliwekwa capacity kwa idadi ya abiria na mizigo, kupata majibu ya nani anapaswa kuwajibika lazima tuyafahamu haya.

Kama una kivuko kinachopakia watu 100 na magari kadhaa na ukaweka kiwango Cha nauli kwa abiria na watu na ukawa unajua Idadi ya trip kwa siku, alafu kila siku ukawa unapokea Mara nne zaidi ya kiasi kinachotakiwa kukusanywa kwa siku...utaendelea kusherekea kiasi hicho Cha fedha (makusanyo) au utajielekeza kwenye usalama wa abiria na mizigo? Naamini serikali kuanzia ngazi ya chini hadi serikali kuu walijielekeza kwenye mapato zaidi ya usalama na hivyo kuwawajibisha baadhi ya watu siyo sahihi.

Kwa mantiki hiyo Sumatra wana lawama, polisi wanalawama akiwemo rpc, tra, , baraza la madiwani, ofisi ya mkuu wa wilaya na mkoa, CAG anayekagua mahesabu,Waziri mwenye dhamana na vyombo vingine wanapaswa kuwajibishwa.

Lakini Mkuu wa Mkoa aliyeamini watu wamekufa na kutumia madaraka yake kuzuia uokoaji na Leo anakutwa mtu akiwa hai anapaswa kujiwajibisha moja kwa moja hata kama alipewa maelekezo kutoka wapi, Ni Jambo la ajabu kusimika kwa ajili ya mshahara na madaraka huku ukiteketeza nafsi za watu..

Kama ulitaka kumlaumu mkuu wa mkoa ungeenda tu moja kwa moja sio kuzunguka huku na kule!
Kuzama kwa Mv Nyerere, manahodha na wahusika wa kivuko wawajibishwe, serikali sijui kuu au ya mtaa unaiwajibishaje! Tunawajibisha watu…kama ni mkata tiketi, mkaguzi, kama ndio nahodha mwenyewe anaanza kuondoa chombo kilichosheheni vile hawa ndio wa kuwajibisha!
 
Waziri mwenyewe dhama no-1

Alipoambiwa bungeni hakujali alipuuza

Serikali - ya Pombe -no-2, kwasabab
- Imesahau majukum yake nakushinda kutwa nzima kufikiri inaufyeka upinzani kabisa, ikifanya matumizi ya hovyo makubwa nayakutisha kwakina waitara, askali na uhuni wa kila aina

- kukimbilia vipaumbele vikubwa vya madege kwa malipo ya cash bila kuzingatia watanzania waliowengi wanataka nini

Hakuna ni serikali ya sintofahamu.
 
Kama ni kweli tunajifunza kwa hili lisijirudie,kuzuia watu watulie walipokaa hadi meli itie nanga,kudhibiti uzito na idadi ya watu watakawao,kuongeza idadi ya vivuko kulingana na uhitaji,kuwepo kwa rescue team zenye fiber speed boat,helicopter, maboya yatanukayo hadi mita mia na kuwa kama jukwaa ili wanaookolewa wakalie kupumzika wakisubiri kupewa huduma za kwanza,madawa,spotlight za kwenye maji, wapiga mbizi,kamba zieleazo hata mita 100 zinazoweza tupwa kwa helicopter toka juu kama wavu eneo la tukio ili yeyeto anaetapatapa kuanzia mita 2 anaweza daka kamba hizo,kuwepo na mtoa mafunzo ya jinsi ya kujiokoa wakati wote tatizo likitokea kama ilivo kwenye ndege wale waelimishaji,kuwepo na standby nurse au watu wa huduma ya kwanza mda wote chombo kiwapo majini. Fedha ya akiba standby,mfumo wa maafa kila mkoa urudishwe na upewe fungu ambalo litakuwa likikaguliwa na taarifa zipelekwe ofisi ya raisi kudhibiti utumikaji wake,tuwe na backup standby rescue team,nk.Uhai wa mtz mmoja una thamani kuliko Marudio ya uchaguzi zisizo na tija kwa taifa.
Screenshot_2018-09-22-14-42-38.jpg
 
Anaandika Ninja Martin Maranja Masese (Nimefupisha)
_________________________________________
Tarehe 25 March 2016, huko Watchet, West Beach, Laguna, California.

COASTGUARDS, boti za uokoaji (lifeboats) mbili, paramedics (watoa huduma ya kwanza) pamoja na chopa (helicopter) zilihusika katika usiku wa kuvutia, kwa zaidi ya masaa sita wakati wa kuokoa baharia mmoja ambaye MASHUA yake ilipigwa na mawimbi mazito na kukosa uelekeo na kuzama.

Baharia huyu mzoefu sana, umri wa kati alikuwa akiendesha chombo hicho kutoka Penarth kwenda Watchet usiku wa Jumamosi tarehe 25/03/2016 kwenye mashua yake ya rangi ya blue 25ft fin-keeled, wakati 'injini' ilipogoma kufanya kazi.

Shuhuda wa tukio akatoa taarifa kwa haraka, baada ya kuona mashua ikipigwa na upepo wa Kaskazini Mashariki (North~easterly wind) kupelekwa kwenye miamba kutoka kwenye ukanda wa West Street Beach.

Shuhuda wa tukio hilo anaitwa Jeff Bourne, akatoa taarifa kwa LAPD (Los Angeles Police Department) wao wakafika na chopa, paramedics, na lifeboats mbili kwa ajili ya 'kuokoa mtu mmoja' walitumia saa sita kumtafuta, kumpata na kumuokoa (kama inavyoonekana pichani).

Tarehe 20 September 2018, Bugolora, Ukerewe, Mwanza, Tanzania.

Kivuko cha Mv.Nyerere chenye kufanya safari zake Bugorora hadi Ukara, kupitia Ziwa Victoria, kinazama majira ya saa 10 jioni just mita 100 tu kabla ya kufika ufukweni. Boti za wavuvi zinajaribu kuokoa watu kwa njia za jadi. Wavuvi hawana nyenzo wala hawana skills za uokoaji lakini wanajitahidi kuokoa watu karibu 40 wakiwa hai.

Kwa zaidi ya masaa matatu serikali haijachukua hatua yoyote zaidi ya kuangalia wavuvi wanavyozamia kuokoa manusura. Hakuna helcopter, hakuna boti za uokoaji, hakuna vikosi maalumu vya uokoaji, hakuna life jackets, hakuna paramedics, hakuna lifeboats. Kitu pekee kilichokuwepo ni mashangingi ya mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya, ambao wamesimama kando ya ziwa wakiangalia wavuvi wanavyohangaika kuokoa waliozama.

Saa 2 usiku Mkuu wa mkoa wa Mwanza anazuia zoezi la uokoaji lisiendelee kwa sababu "GIZA" limetanda. Yani alishindwa kabisa kufikiri kuhusu kuleta 'chopa' imulike eneo la tukio uokoaji uendelee? Labda tungeokoa watu wengi zaidi.

Kwamba hata kufikiri kuhusu kutafuta msaada wa haraka wa kununua spotlights zenye watts 1500~2000 ilishindikana? Au hata kuongeza Jenereta la KV 7 ili 'uokoaji' uendelee alishindwa? Kwamba kwa uwezo wake wa kufikiri aliona heri watu waendelee kufa aje kuokota maiti asubuhi, kuliko kutafuta alternative ya mwanga usiku? Hizi ndio akili za viongozi wetu? Na bado yupo ofisini hadi sasa?

Hivi huko ziwani Askari wa maliasili wanatumia boats gani kwenye ulinzi dhidi ya wavuvi haramu? Kwanini hizo boti hazikuitwa kusaidia uokoaji?

Kweli jeshi la polisi hakuna chopa? Kamandi ya JWTZ huko Lake zone pia haikuwa na helcopter? Mwanza nzima hakuna huduma ya rescue inayotumia chopa? Kwamba tulikosa Mwanga kabisa wa kumulika eneo la tukio? The best option tukaona ni kuhairisha zoezi, tukalale, tuamke asubuhi tuje kuokota maiti? Seriously?

Fidel Castro wakati wa jaribio la mapinduzi ya kumuondoa Dikteta Fulgencio Batista madarakani, mmoja kati ya wapiganaji wenzake alizama kwenye maji, safari ya kwenda Sierra Maestra ilihairishwa ili 'mpiganaji' huyo atafutwe na apatikane.

Mwandishi wa vitabu, Muingereza George Orwell alipata kusema "All human beings are equal but some are more equal than others" kwa tafsiri isiyo rasmi Orwell alimaanisha; Binadamu wote ni sawa lakini kuna ambao ni sawa zaidi kuliko wengine"

Hebu jiulize huko kwenye kivuko kungelikuwa na mtoto wa Rais, Waziri Mkuu, au IGP je huyo mkuu wa mkoa angetoa amri ya kusitisha zoezi la uokoaji kwa sababu ya giza? Au lets assume mtoto wake mwenyewe angekuwa huko, je angeruhusu watu kwenda kulala ili asubuhi aje kuokota maiti ya mwanae? Amin, amin nawaambia mtoto wa Mongela angekuwepo kwenye kivuko asingekubali kwenda kulala aje kuokota maiti ya mwanae asubuhi. He could fight to infinity because he believe to be more equal than others. Hivi ndivyo viongozi wetu walivyojengwa.

Hii inatufundisha nini? Marekani na nchi zilizoendelea uhai wa mtu mmoja ni muhimu kuliko jambo lolote. Wanathamini utu wa kila mtu bila kujalisha ni kiongozi au sio kiongozi, ni maarufu au sio maarufu, ni mzee au kijana. Kwao utu kwanza. Ndio maana wapo tayari kukesha ndani ya maji kutafuta mtu mmoja aliyepotea baharini na kumuokoa akiwa hai, bila kujalisha wametumia gharama kiasi gani.

Lakini hapa Tanzania thamani ya mtu inategemea yeye ni nani? ni wa chama gani? ana undugu na kiongozi gani? Hujawahi kuona watu wanabaguliwa kwa sababu ya chama? Hujawahi kuona watu wananyimwa fursa fulani kwa sababu hawana ndugu zao ambao ni viongozi? Hivi ndivyo jamii yetu ilivyojengwa. Ndio maana Mongela alipoona hakuna kiongozi yeyote kwenye hicho kivuko, wala hakuna mtoto wa Rais, PM, waziri au viongozi wengine wakubwa akaamua waokoaji waende kulala, watakuja kuokota maiti asubuhi.

Lakini asingepata usingizi kama kungekuwa na mtoto wa kiongozi mkubwa kwenye hicho kivuko. Wala asingethubutu kusimamisha zoezi la uokoaji. Angepambana zipatikane helicopter za kumulika hata kama ni za kukodi. Angepambana kupata boti za uokoaji, angepambana kupata life jackets za kuwarushia manusura. He could do anything save lives. Hapa sasa ndipo utamuelewa George Orwell aliposema "All human beings are equal but some are more equal than others"

Miaka 22 baada ya Mv.Bukoba bado hatujifunzi?

Martin Maranja Masese || MMM
Pagum ni hapo kwenda kulala uokozi uendelee asubuhi
Huyo jamaa bana sijui 2
 
Kama ulitaka kumlaumu mkuu wa mkoa ungeenda tu moja kwa moja sio kuzunguka huku na kule!
Kuzama kwa Mv Nyerere, manahodha na wahusika wa kivuko wawajibishwe, serikali sijui kuu au ya mtaa unaiwajibishaje! Tunawajibisha watu…kama ni mkata tiketi, mkaguzi, kama ndio nahodha mwenyewe anaanza kuondoa chombo kilichosheheni vile hawa ndio wa kuwajibisha!
Kwa mfano, unamtoaje Mkuu wa mkoa kwenye hii dhahama?
 
Thubutu huyo makonda tu na mavyeti yake amelindwa kama moyo wa MTU

Angelikuwa ndani ya hicho chombo, baba angeamuru watu wakaushe ziwa ili apatikane.
 
wote wasamehewe.
Kasoro yule aliyewaambia waokoaji wakalale.kesho ndo waendelee.
Aiseee.maji sio mchezo.
Idadi ingepungua kama wangeendelea na kazi..masaa 12 kwenye maji sio .mchezo
 
mkuu wa mkoa hahusiki na kuzama kwa kivuko bali kama ni kweli alisitisha zoezi la uokoaji basi awajibike kwa maelekezo mabaya ya uokoaji!
Kumbuka kuna tendo la kuzama ni moja…na kuokoa wahanga ni jambo jingine!
kubeba watu idadi kubwa kuliko hata viokozi nalo ni janga jingine na wanaoendesha vyombo hivyo wawajibishwe!
 
Kama ulitaka kumlaumu mkuu wa mkoa ungeenda tu moja kwa moja sio kuzunguka huku na kule!
Kuzama kwa Mv Nyerere, manahodha na wahusika wa kivuko wawajibishwe, serikali sijui kuu au ya mtaa unaiwajibishaje! Tunawajibisha watu…kama ni mkata tiketi, mkaguzi, kama ndio nahodha mwenyewe anaanza kuondoa chombo kilichosheheni vile hawa ndio wa kuwajibisha!
Ni Mara moja MV Nyerere imebeba zaidi ya uwezo wake? Lengo la kwanza la vyombo vya serikali ni kutoa huduma siyo biashara, lakini siyo kwa hapa kwetu. Hao unaowatetea wanapaswa kuwajibika maana haiwezekani mwaka 1978 uwe na meli inayobeba abiria 100 na 2018 uwe na meli hiyo hiyo na bado usipredict tatizo, basi wewe ni Zuzu.
 
Je huyu fundi mkuu aliyekaa saa 48 vipi? Usicheze na MUNGU mkuu
Je huyu fundi mkuu aliyekaa saa 48 vipi? Usicheze na MUNGU mkuu
Ndio maana tunasema nyie ccm badala ya kununua yale magari ya washawasha mngezingatia kupata vifaa vya uokoaji kama helmet zenye taa, na special jackets kwa ajili ya resque, na sio kujikalisha hapa mnatoa macho, watu wakitoa maoni yao mnasema wanatafuta umaarufu, manataka watu wakae kimya kama mazwazwa, this is our Freedom Country bwana, tusingependa kufanywa vibwengo
 
Ni Mara moja MV Nyerere imebeba zaidi ya uwezo wake? Lengo la kwanza la vyombo vya serikali ni kutoa huduma siyo biashara, lakini siyo kwa hapa kwetu. Hao unaowatetea wanapaswa kuwajibika maana haiwezekani mwaka 1978 uwe na meli inayobeba abiria 100 na 2018 uwe na meli hiyo hiyo na bado usipredict tatizo, basi wewe ni Zuzu.

Simtetei mtu, serikali haitakuja jikoni au chooni kwako kukupigia kelele kuhusu usafi ili usipate kipinduapindua, au ofisini kwako kama hutawajibika kikamilifu utakuwa unaishi na janga ambalo siku moja litachoka kukuvumilia…
ni hali hii ya kutokujari na kuishi kwa mazoea badala kwa umahili wa kazi yako ndio kunakopelekea majanga kama haya…ni wazi kuwa hawa wafanyakazi wa kivuko hicho na vingine vingi…na hata kwenye mabasi/magari, hali wakijua madhara yatokanayo na kuzidisha mzigo ukilinganisha na uwezo wa chombo ktk taaluma yao ya usafirishaji wanaleta mzaha na kuzoelea mzaha…na kama wahenga walivyosema…'mzaha mzaha hutumbua usaha' haya yametimia kwa manahodha na wote wanaoendesha Mv Nyerere 'wamekibinua na kuwaua hao waliokuwa wanawasokomeza kwenye kachombo hako! Serikali haina lawama ya moja kwa moja ktk hili bali kuna watu waliopewa kazi ya kuiendesha Mv Nyerere ndio waliotuangusha kwa kuibebesha zaidi ya uwezo! Inawezekana hata ktk uteuzi au uajiri wa wataalamu hao walipitia njia ya panya na hivyo kutokuwa na sifa sitahili!
 
Nasimama upande wako OKW, Eti kwamba hawa ni wapiga kura wangu kwa hiyo wasibomolewe, Nami nafurahi kuona hivi vipande vya Tanzania kwani kwa sasa havizuiliki

chuki za namna hii hazijawahi kumwacha mtu salama! haya ya wapiga kura wangu yanahusikaje hapa sasa!?!
 
Back
Top Bottom