Nani anawajibika kutoa ajira au kazi?

Philo_Sofia

Member
Oct 4, 2023
60
94
Tupo kwenye dunia ambayo mageuzo ni makubwa na athari ni kubwa hasa kwa jamii ambayo haijajiandaa.

Mbaya zaidi mageuzo hao hayajali umejiandaa au hujajiandaa, umeelewa au hujaelewa.

Hivi leo, kwa sababu ya maendeleo mbalimbali ikiwemo maendeleo ya teknolojia, dunia inakabiliwa na changamoto mbalimbali.

Moja ya mambo yanayohatarisha usalama wa dunia ni tatizo la ukosefu wa kazi. Tatizo hili ni kubwa zaidi kwa nchi masikini ikiwemo Tanzania.

Lakini kwa nini watu hawana kazi? Kwa nini hakuna ajira? Je, ni kweli kuwa tatizo la ukosefu wa kazi linasababishwa na maendeleo ya teknolojia; kwamba teknolojia ndio imesababisha watu wasie na kazi au ajira?

Tunaweza kujibu maswali hayo hapo juu kwa kutafakari swali hili: "Wajibu wa kutoa ajira au kazi ni wa nani"? Nani anawajibika kutoa ajira au kazi? Je, ni Serikali? Ni wazazi au walezi? Au ni jamii? Ni nani hasa anawajibika kuhakikisha mtu au watu wanakuwa na kazi?

Mtu wa kwanza anayewajibika kwa hili ni wazazi. Kwa nini mzae mtoto au mlete uhai mpya duniani wakati hujajiandaa au hujaweka rasilimali msingi na muhimu zinazohitajika kwa maendeleo na ukuaji wake?

Kuzaa si muhimu ikiwa kuzaa hakuzingatii ukweli wa kiakili. Tatizo la ukosefu wa kazi ni kosa la wazazi kukataa kutumia akili.

Anayezaa lazima ahakikishe usalama wa anayezaliwa. Usalama huo ni pamoja na kazi. Watu wazae kwa kufuata utaratibu wa akili.
 
Back
Top Bottom