Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,214
- 3,587
- Thread starter
- #41
Umetufaa kwa viwango vilivyotukuka. Umepanua uelewa wetu, umeonyesha njia na namna ya kutanua mjadala. Ni kweli tuzo haijasitirika kwa wanasiasa pekee ila hao ndiyo wako kwenye global spotlight kwamba hadi sasa labda hatuna mwanasayansi aliyefanya ugunduzi wa kunyanyua nyusi za dunia.Douglas, heading yako inawaaminisha watu tuzo ya Nobel ni kwa marais tu kitu ambacho sio hata ya watani wetu wa Jadi Kenya hapo ilikwenda kwa Mama Wangarĩ Muta Maathai ambaye alikua mwanaharakati wa kijamii, mazingira na siasa then kama mbunge na naibu waziri to add up alikua mwanamke wa kwanza ukanda wa eastern africa kuwa na PhD na Nobel price yake ilikua category ya maendeleo thabiti, demokrasia na amani na mwanamke wa kwanza mwafrika kupata tuzo hiyo.
Hata hivyo ni kweli urais ama nyanja ya siasa hutolewa pia kama ilivyo tokea kwa Obama, Mandela, PM wa Ethiopia ambayo huhusisha mambo ya amani. Nyanja ya siasa/amani haikua lengo kuu la Nobel ingawa iliongezwa na kuwa maarufu kutokana na urafiki wake na Bertha Von Stunner ambaye alikua mwanaharakati wa amani.
Nguli wa kimapinduzi ya Vietnam aliyewahi kuchaguliwa kupewa tuzo na akaikataa ni Lê Đức Thọ. Na mwenzake Henry Kissinger baadae aliigawa charity home na mpunga akaurudisha.
Back to Tanzania, kwa marais wenye chances ni Samia Suluhu, J Kikwete na Mwinyi Mzee as nimewatoa JPM, Mkapa na JKN coz ni marehemu as tangu 1974 Nobel prize hawatoi kwa posthumously yaani wafu unless awe amechaguliwa kabla ya tarehe y kufa na mchakato umekamilika. Wote wangekua hai basi ningefikir JK Nyerere.Why? Kuchangia amani kwa ukanda wa Afrika na dunia enzi za uhuru wa Africa.
Mambo haya yaliishia 1961 kwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani.
Ni kama ilivyoniumaga kwa nini Mahatma Gandhi hakupewa despite kuwa nomiated zaidi ya mara nne. Nahisi hadi leo Nobel Prize Committee wanalijutia.
Siasa ndio ina run dunia no matter hatuwasikii akina Maria Curie na the likes walotufikisha hapa tulipo na gudunzi zao mbali mbali na wakapewa The Nobel Prize.
Nimepanua mjadala kidogo, mleta maada nina imani sijaweka matusi wala uchangiaji wa povu kama ukivoomba ingawa nimetype huku navuta mneri.
Rest In Peace Sir Abel Nobel.
Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app