Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,214
- 3,587
- Thread starter
- #21
Yawezekana kilichomkwamisha Mwl kutopewa tuzo ya Nobel ni uamuzi wake binafsi wa kuipiga Uganda, kung'oa na kupandikiza uongozi 1979, uamuzi ambao aliuchukuwa baada ya Jumuiya za Kimataifa kumkalia kimya hata alipoziandikia barua kwamba nchi yake imevamiwa hivyo wachukuwe hatua kumuagiza adui aondoke kwa amani. Kimya cha Jumuiya za Kimataifa huenda kilichukuliwa na Mwl kama muhuri na saini ya Jumuiya hizo kwamba jitetee/jihami, ilhali baada ya uamuzi huo wa Mwl, Jumuiya hizo zikaja kupiga kelele baada ya kuona uwezo wa kivita wa Tz kwamba Mwl ameenda hadi chumbani kwa adui kinyume na mila na desturi za Jumuiya za Kimataifa ambazo Tz iliziridhia kwa kuwa mwanachama. Yawezekana Jumuiya za Kimataifa zilidharau Tz kwamba haina silaha za kumdhibiti adui hivyo Mwl angesurrender na hivyo kusingekuwa na vita au vita vingehamia kwenye meza-mduara za Jumuiya hizo kutafuta suluhu (ambayo huenda Mwl alistukia janja hiyo kwamba labda Jumuiya hizo zilitaka kumpa adui mkoa wa Ziwa Magharibi sasa Kagera), kumbe wasijuwe kwamba yawezekana kweli Mwl hakuwa na silaha lakini kumbe alikuwa na ujuzi, akili na utaalam wa silaha za adui na zile ambazo adui hana na kwamba falsafa ya vita ya Mwl ilikuwa ni stratejia ya kumpiga adui kwa kutumia silaha zake mwenyewe kwa asilimia kubwa. "Vamia, teka, chukuwa, shambulia, songambele" Yawezekana Jumuiya za Kimataifa zilitumia sababu hii kumuona Mwl kwamba hastahili tuzo ya Nobel, kwamba ni mvamizi kama adui alivyokuwa mvamizi pia (Balance of Perspective).Ila pia, sina hakika kama Tuzo hii ni ya nchi za Magharibi au ya jumuiya za kimataifa, Alfred B. Nobel ni Mswedish ambayo ni nchi iliyokuwa rafiki wa Tz wakati huo wa mawazo hayo ya Mwl Nyerere yaliyopingwa na Magharibi yalipokuwa yakitoka.
“Having come into contact with a civilization which has over-emphasized the freedom of the inpidual, we are in fact faced with one of the big problems of Africa in the modern world. Our problem is just this: how to get the benefits of European society – benefits that have been brought about by an organization based upon the inpidual — and yet retain African’s own structure of society in which the inpidual is a member of a kind of fellowship.”
Julius Kambarage Nyerere as quoted in the New York Times Magazine on 27 March 1960. -
Hiyo ya Mwl ni tofauti na JK ambaye alivamia Anjuan, akang'oa na akakabidhi kwa Comoros KWA KIBALI CHA JUMUIYA ZA KIMATAIFA akiwemo mkoloni Mfaransa.