Nani anakumbuka hii??

Nani anakumbuka hii??

Sidhani kama kuna kijana wa sasa ambae hakuuchezea mpira kama huo utotoni
 
Tulikua na afya si mchezo hutakaa usikie mafua wala malaria bhana aah sie tulikua tunasema kupiga ndole sio dochi
 
Dah mbaaaali......nakumbuka kama wewe ndiye uliyetengeneza mpira hukosi namba
 
Dah mbaaaali......nakumbuka kama wewe ndiye uliyetengeneza mpira hukosi namba

Kweli mkuu! Ha ha hahahaa

Mwenye huo mpira haruhusiwi kuchezewa rafu, ukimkwatua na chachacha zako unatolewa nje, ila yeye akikukwatua poa tu. Tuliliita sembo,
 
Au wengine walikuwa wanafunga soksi za shule unakuwa mpira, ila nadhani pembezoni mwa miji hilo bado lipo usishangae kuona

Ni sehemu chache sana hii ipo watoto wa siku hizi kutokana na mazingira waliokulia wengi wao si wabunifu maana kila kitu kipo kama hakuna uwezo wa kununua original kuna vya mchina
 
Kweli mkuu! Ha ha hahahaa

Mwenye huo mpira haruhusiwi kuchezewa rafu, ukimkwatua na chachacha zako unatolewa nje, ila yeye akikukwatua poa tu. Tuliliita sembo,[/Q

Hii imenikumbusha mbali kweli ingeendelea mpaka sasa nadhani hizi plastic bag zingekuwa zimeisha kabisa, alafu kulikuwa na watu wachache sana wataalamu wa kusuka mipira hii katika kiwango cha juu wengine mkisuka mnazuia watu wasipige kwa kutumia dole gumba maana mpira unafumuka
 
Kweli mkuu! Ha ha hahahaa

Mwenye huo mpira haruhusiwi kuchezewa rafu, ukimkwatua na chachacha zako unatolewa nje, ila yeye akikukwatua poa tu. Tuliliita sembo,

Sawasawa kabisa nafikiri tuliishi maeneo yanayofanana na sisi kwetu iliitwa sembo......wakati mwingine kuna gombania goli.............Viatu vya chachacha (vingine mabondo) ndiyo ilikuwa fasheni ila kwenye jua kali utajuta kuvivaa!
 
Daah! mbali kinoma..nilimaliza kirago cha bibi.. ikiitwa "ANANGA"..ukimkwaza mwenyenayo mwisho wa gemu, na enzi
hizo tunavaa "ACHWOGA"!
 
Sidhani kama kuna kijana wa sasa ambae hakuuchezea mpira kama huo utotoni
na

Wapo wawili wa tatu kuna ambao walikuwa watoto wa chai ya saa 10 ikifika saa 9 wanakwenda kulala wakiamka wanapewa vitabu kisha wabachukua vigari au baiskeli na kuanza kucheza wakati wengine wanakukuruka kwenye jua na mpira wakati huohuo asubuhi yake walicheza komborela
 
Linaitwa SAMBI!Halafi ilikuwa marufuku kupiga doso ama ndoso!

Enzi hizo nikuwa Dodoma maeneo ya Chamwino tulikuwa tunaita jina hilo la sambi na hakuna kupiga dochi maana mwenye mpira anakuja juu na kubeba mpira wake
 
Dotworld hiyo stock ya mipira ulikuwa nayo maktaba maana sidhani kama mpaka sasa inapatikana au ulitunza picha japokuwa utamaduni wa kupiga picha ulikuwa haupo
 
Last edited by a moderator:
Sawasawa kabisa nafikiri tuliishi maeneo yanayofanana na sisi kwetu iliitwa sembo......wakati mwingine kuna gombania goli.............Viatu vya chachacha (vingine mabondo) ndiyo ilikuwa fasheni ila kwenye jua kali utajuta kuvivaa!

wengine ilikuwa tunavaa soksi mguu mmoja ule unaoutumia au kiatu mguu mmoja alafu kiatu cha mguu wa kushoto unampa mwenzako, ukiwa na viatu vya kuchezea mpira wewe unaonekana ni mwamba (viatu hivi tulikuwa tunaviita NJUMU)
 
Usisahau kuna wengine walikuwa hawataki kusikia habari ya viatu........wanasema vinawafanya wakose kontroli ya mpira!
 
Usisahau kuna wengine walikuwa hawataki kusikia habari ya viatu........wanasema vinawafanya wakose kontroli ya mpira!

Nakumbuka ilikuwa umishumta (mashindano ya shule za msingi taifa) yalifanyika Dodoma ilikuja timu toka Songea ilipiga mpira mzuri walianza wengi wakiwa na viatu lakini kadri muda unavyokwenda wakawa wanavua viatu mmojammoja.
 
ha ha ha......duh tumetoka mbali
 
Kwetu Pwani huita chandimu au sodo. Palikuwa hapatoshi wakati wa kucheza timu tatu...balaa!
 
Back
Top Bottom