Ng'wanamalundi
JF-Expert Member
- Feb 4, 2008
- 1,165
- 1,361
Umeuliza nani anamkumbuka David Wakati. Mimi ni mmojawapo. Ni kweli kabisa kwamba hata kipindi David Wakati akiwa Mkurugenzi Mkuu wa Radio Tanzania, bado alikuwa akishiriki kufanya kazi za kawaida za utangazaji. Kipindi cha 'Nipe Habari' hakikuwa na mtangazaji mwingine, mbali na David Wakati; labda awe na udhuru. Asilimia 90 ya vipindi hivyo alikuwa anavitangaza yeye mwenyewe. Ilikuwa kama mtangazaji mwingine akishika zamu inakuwa kama kipindi hakikuwepo siku hiyo. Kinapooza sana. Sawasawa na kipindi cha Majira kutangazwa na mwingine zaidi ya Ben Kiko. Msikilizaji huridhiki. David Wakati pia alikuwa akisoma taarifa za habari za Kiingereza ikijulikana kama Idhaa ya Nje. Nahisi walikuwepo watangazaji wachache tu Radio Tanzania waliokuwa wakikimudu Kiingereza ya kutosha, kama Rochus Matipa. Kwa hiyo ilibidi wapeane zamu hao wachache waliokuwa wanaimanya hiyo lugha. Matangazo kwenye ibaada za Kikristu wakati wa Noeli au Pasaka nayo alikuwa akiyamudu vizuri sana. Yeye alikuwa Anglikana. Lakini alikuwa akienda po pote pale ibaada inapofanyika na anafanya vizuri kabisa; iwe Kanisa Katoliki au la Kiluteri. Mola amlaze pema.David Wakati alikuwa mzungumzaji wangu sana tukikutana. Nikipenda sana vipindi vyake hasa, "Nipe Habari."
Signature tune ya kiindi hiki ilikuwa nyimbo maarufu, ''South of the Border.''
Katika kipindi hiki cha kila Jumamosi usiku David Wakati alifanya kipindi kilichonigusa sana alipofariki Raymond Chihota Harare na pia alipofariki Mamboleo Rashid Makoko London.
Raymond Chihota alipata kuwa mtangazaji wa TBC katika miaka ya mwanzoni 1960s kabla ya kwenda Urusi kwa masomo ya juu.
Ray kama alivyojulikana alikuwa mmoja wa vijana wa Chipukizi Club pamoja na marehemu Henin Seif, Hussein Shebe, Salum Hiriz kwa kuwataja wachache wakiendesha kipindi kilichopendwa sana na vijana wakati ule wakiwa na bendi wakipiga muziki wa Kizungu wa akina Elvis Presley, Cliff Richard na Beatles.
Kipindi hiki kikirushwa Jumamosi mchana kwa jina la "Chipukizi Club."
David Wakati aliwatia moyo hawa vijana kufanya kipindi kile hadi kilipopigwa marufuku na Regional Commissioner wa Dar es Salaam Mustafa Songambele.
David Wakati alikuwa na kipaji cha hali ya juu cha kueleza mambo na alimweleza vyema Ray Chihota.
Halikadhalika alimweleza Mamboleo Rashid Makoko kwa ukarimu wake kwa Watanzania waliokuwa wanafika London.
Akiwaalika nyumbani kwake na kuwapa kila aina ya msaada.
Mamboleo Rashid Makoko aliondoka Tanganyika mwaka 1958 na hakutaka kurudi. Alirudishwa kwao Tanga kuzikwa.
Namkumbuka David Wakati mwaka wa 1991 wakati akiwa Mkurugenzi wa Radio Tanzania. Serikali ilijikuta ikipambana na Waislam katika suala la elimu.
Waislam waliigeuza Shule ya Muslim kuwa seminari Nyerere akatoa agizo shule irejeshwe katika hali yake ya zamani.
Ugomvi huu ulikuwa umetoka mbali.
Vijana wa Kiislam wakifahamika kama Warsha walikuwa wamejipenyeza ndani ya BAKWATA ili kuibadili. Jukumu lao la kwanza walilojipa ilikuwa kuboresha shule za Kiislam.
Hapa ndipo walipopambana na serikali.
Ili kupinga amri ile ya serikali Warsha ikaitisha mkutano Shule ya Kinondoni agenda kuu ikiwa hali ya elimu ya Waislam Tanganyika toka uhuru.
Mkurugenzi wa RTD David wakati ndiye aliyeingia studio kusoma tangazo la kuwaonya Waislam kutoitika mwito wa mkutano ulioitishwa na Warsha.
David Wakati kwa ile sauti yake nzito ya wastani alisema mkutano huo ni haramu na Waislam watakaohudhuria watakamatwa.
David Wakati akiupenda Ukristo wake na ukitaka kumfaidi ni pale RTD inaporusha matangazo ya moja kwa moja kutoka St. Joseph's Cathedral wakati wa Pasaka au Mkesha wa Christmas yeye akiwa mtangazaji.
Palitokea malalamiko kuwa David Wakati katika moja ya vipindi vyake kaweka ''signature tune,'' nyimbo ya kanisani, yaani ''hymn.''
Alilieleza hili katika kipindi akakana kuwa nyimbo ile ni ya kanisani na akaendelea kuitumia.
Picha: Chipukizi Club waliokaa kulia ni Henin Seif na kushoto ni Hussein Shebe. Kulia aliyesimama ni Raymond Chihota.
Mamboleo Rashid Makoko