Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,921
- 30,264
INAKUWAJE MWANAHISTORIA ANAPOKUTANA NJIANI NA KIZAZI CHA CHIEF MAREALLE NA CHIEF MARUMA WOTE KWA WAKATI MMOJA?
Kuna mengi yasiyofahamika katika historia ya uhusiano waliokuwanao machifu wa Tanganyika na raia wa kawaida.
Halikadhalika na viongozi waliokuwa katika harakati za TANU za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Bahati mbaya sana machifu wenyewe wamekuwa kimya sana kusema lolote kuhusi kipindi hiki cha historia hata pale wanaposingiziwa yale ambayo hawakufanya.
Inawezekana hii ni kwa sababu za adabu za watawala kuwa kwa hadhi zao na kulinda heshima zao hawawezi kujiingiza katika ubishi.
Nimebahatika kusoma barua za Paramount Chief Thomas Marealle alizokuwa akiandikiana na Ally Sykes katika Nyaraka za Sykes na vilevile kuelezwa urafiki uliokuwapo baina ya Chief Thomas Marealle na Abdul Sykes na mdogo wake Ally katika miaka ya 1950.
Barua hizi zinasisimua.
Naamini iko siku watafiti watazifikia na kuandika.
Nimeelezwa habari za Chief Thomas Marealle na Ally Sykes na pia na Mwalimu Sakina bint Arab.
Mwalimu Sakina anasema kuwa kuwa siku zote Abdul akikutana na Marealle, Abdul akimwambia Marealle kuwa yeye ni ''King'' si Chief lakini Waingereza hawataki kumwita hivyo kwa kuwa wakifanya hivyo King George mfalme wao watamwitaje?
Mimi katika nikiishi jirani na David Marealle, Masaki lakini hatukupata kufahamiana kwa karibu.
Siku moja Abbas Sykes alikuja nyumbani kwangu na akaniomba nimsindikize nyumbani kwa David Marealle.
David Marealle alikuwa na nyumba nzuri sana katika nyumba zilizojengwa Masaki miaka ile.
David Marealle akaniambia kuwa mara yake ya kwanza kufika Dar es Salaam katika miaka ya mwishoni 1940 au mapema 1950 alifikia nyumbani kwa Abdul Sykes na hapo ndipo alipofahamiana na Abbas Sykes ambae umri wao ulikuwa umelingana.
Urafiki wao ulianza hapo.
David Marealle alipofariki Abbas Sykes alihudhuria mazishi yake halikadhalika alipofariki Chief Thomas Marealle.
Nakumbuka aliporudi kutoka maziko ya Chief Thomas Marealle aliniambia kuwa kakutana na David Marealle lakini afya yake si njema.
Leo nimekutana na Peter Marealle na yeye akanisalimia na akajitambulisha.
Mimi nilikuwa natoka benki na yeye ndiyo anaingia.
Tumekutana mlangoni.
Wakati tunasalimian mara akawa anakuja Harold Maruma akanitambulisha kwake na kumwambia kuwa mimi nina mengi niyajuayo kuhusu wao.
Hivi ndivyo mazungumzo yetu yalivyoanza.
Hii ilikuwa bahati kubwa sana kwangu.
Nikawafahamisha kuwa nina mengi ya wazee wao na nimefahamiana na ndugu zao wengine hapa Dar es Salaam sote tukiwa wanafunzi sekondari na wengine Chuo Kikuu: Philip Marealle, Kibo Marealle, Janet Marealle na Winston Maruma.
Historia ina kawaida ya kujirudia.
Kibo Marealle alikuja nyumbani kwangu Tanga ameongozana na Abraham Sykes na ndiyo siku tukafahamiana.
Nikawapiga picha hiyo hapo chini.
Baba zao walikuwa marafiki na wao watoto wamekuja kuwa marafiki.
Kibo alipofariki ni Abraham ndiye aliyenipa taarifa ya msiba.
Winston Maruma yeye alikuwa rubani.
Nilikutananae Maputo mwaka wa 1990, Ujamaa House baada ya kupoteana.
(Niliambiwa kuwa jumba hili refu Samora Machel aliwapa Tanzania siku Msumbiji ilipopata uhuru kwa kuiambia Tanzania wachague jengo lolote yeye atawapa bure na hapa Ujamaa House ndipo ulipo ubalozi wa Tanzania, Msumbiji).
Ilikuwa wakati wa Kombe la Dunia na Watanzania wengi walikuwa pale wanatazama mpira.
Winston Maruma tukakutana tena siku moja mwaka wa 2004 uwanja wa ndege wa zamani mimi nikitafuta ndege ya haraka kwenda Zanzibar.
Bahati mbaya sana nilikutana na mabwana Marealle na Maruma wao wakiingia benki mimi natoka.
Hatukuwa na muda wa kuongea sana.
''They made my day,'' kama wasemavyo Waingereza.
PICHA: Picha ya kwanza machifu watatu na majina yao.
Picha ya pili kulia ni Peter Marealle kushoto ni Harold Maruma na picha ya tatu kulia ni Abraham Sykes na Kibo Marealle.
Picha ya nne ni Mangi Mkuu Thomas Marealle.