Hatutachoka Kumtaja Bi. Titi Mohamed

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,263
BI. TITI HATUTACHOKA KUMTAJA

Antar Sangali ana mapenzi makubwa na marehemu Bi. Titi Mohamed kila apatapo fursa humzuru na kumuombea dua.

Nimepokea picha na mengi kuhusu Bi. Titi kutoka kwake.

Picha ya kaburi hili la Bi. Titi lililowekwa sawa badala ya lile la zamani niliipata kutoka kwake.

Leila Sheikh alikuwa kipenzi cha Bi. Titi na alikusanya mengi kutoka kwake kuhusu maisha yake kwa nia ya kuandika historia ya maisha yake.

Mkusanyo huu una sauti na notes kutoka kwa Bi. Titi mwenyewe akimweleza Mwanlela kama mwenyewe alivyopenda kumwita historua yote ya maisha yake na yote yaliyotokea.

Leila alipata kuniambia kuwa Bi. Titi hakusaza kitu.

Bahati mbaya Leila amefariki kabla hajaandika maisha ya shoga wake kipenzi na bibi yake Bi. Titi Mohamed.

Mara nyingi nilizungumza kwa simu na Leila kuhusu hazina hii aliyoachiwa na Bi. Titi na nilifikia kumuomba Leila anifanye kuwa msaidizi wake katika kuandika historia ya Bi. Titi.

Kwa upande wangu nilimpa Leila mswada wa kitabu cha maisha ya Bi. Titi umsaidie katika kazi yake.

Pamoja na ule mswada nilimpa Leila picha zote nilizokusanya katika utafiti wangu wa maisha ya Bi. Titi zimsaidie katika kazi yake hiyo ya kuandika kitabu cha Bi. Titi.

Mategemeo yangu ni kuwa kitabu cha Bi. Titi Mohamed kitaandikwa.

Hiyo hapo chini naamini ni kati ya picha za awali zaidi katika picha za Bi. Titi Mohamed zilizopo, picha zilizopigwa na Mohamed Shebe na zimehifadhiwa na watoto wake hadi leo.

Picha hii inamuonyesha Bi. Titi Mohamed akiwa na Julius Nyerere wakihutubia mkutano wa hadhara Jangwani baada ya kuhamisha mikutano ya TANU kutoka Mnazi Mmoja kwenda Jangwani.







 
Bibi titi nyumba ndogo ya mwalumu.
Leila sheikh mvuta unga wa kinondoni kutoka Tsnga
Tulia na changia mada mkuu, soma sasa ulichokiandika hapo kama kinaleta maana, dot. Com mnajua sana yanayotokea nje ya nchi lakini ya kwetu hapa zero, kisa elimu ya kukariri
 
Usisahau kuandika na failures zao, huyo bibi titi alikua miongoni mwa warioshiriki kujaribu kupindua serikali ya Tanganyika, hakuwa muumini wa sera ya ujamaa.
 
Back
Top Bottom