Kavazi la Dr. Salim Ahmed Salim

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,925
30,273
1695789131160.png

Nimesoma kuhusu kavazi la Dr. Salim Ahmed Salim.

Hakika ni jambo kubwa sana kwetu na nadhani yeye ni wa kwanza kufanya kitu hiki.

Mimi nilibahatika kukutana na Dr. Salim nyumbani kwake kwa kipindi kifupi.

Dr. Salim alikuwa pamoja na mke wangu katika Tume ya Warioba ya Katiba siku hiyo nilimsindikiza kwenda kumuona Dr. Salim.

Nilikuwa na gazeti hilo hapo chini nikampelekea liwe katika maktaba yake na ikadasifu kuwa yeye hakuwanalo.

Siku ile moja ikawa kanifahamu na kila nilipokutana na yeye katika shughuli zetu yeye ni hodari wa kuhudhuria mazishi na khitma nikawa namuomba kumpiga picha na ananikubalia na namueleza kuwa ni kwa ajili ya Maktaba yangu binafsi.

Ninazo picha nyingi za Dr. Salim za miaka ya nyuma sana ambazo nimezikusanya kutoka kwa ndugu na jamaa zipo katika Maktaba yangu.

Katika kitabu cha maisha ya Mwalimu Nyerere: ''Julius Nyerere A Biography'' (2020) waandishi wamesema maneno hayo hapo chini: kuwa kuna maktaba tatu zilizo na kumbukumbu nyingi za Mwalimu Nyerere na taarifa zilizopangika vyema: Maktaba ya Dr. Salim Ahmed Salim, Mohamed Said na ya Brig. General Hashim Mbita:


+3
 
Back
Top Bottom