Kwa sababu ndio imeshika dola na uharibifu unafanyika mikononi mwaoWatu wa CHADEMA hawachoki kujadili CCM.
Zamani kulikuwa na chama cha mapinduzi; uongozi wake ulikuwa hauna utata, maamuzi yake yalikuwa yanaeleweka (hata kama hayapendwi), na mwelekeo wake kiitikadi ulikuwa wazi kabisa. Chama hicho cha zamani hakikuona haya au aibu kusema kuwa ni chama cha kimapinduzi chenye kutaka kujenga taifa la "watu walio huru na sawa".
Ndani yake kulikuwa na nidhamu ambayo ilitokana na kuelewa kuwa uongozi wake hauna utata na kama chama hawakuweza kuona haya kumchukulia mtu yeyote ambaye alikuwa ni tatizo kwa Taifa au kwa chama. Hivyo tangu enzi za TANU maamuzi magumu yalifikiwa na mengine yaliwagusa watu ambao waliaminika kuwa wana nguvu.
Ilipotishiwa uhaini hakukuwa na utata hata marafiki walishukiwa!
Ilipotishiwa Muungano hawakuwa na utata hata Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar na baadaye Waziri Kiongozi wote hawakuonewa haya.
Ilipotishiwa uhujumu wa uchumi hakukuwa na utata wa nini kifanyike (japo baadaye baadhi ya kesi ziligeuzwa na mchakato kuboreshwa). Hakukuwa na utata hata hivyo wa nani atachkua hatua!
Chama kweli kilikuwa kimeshika hatamu ya uongozi. Leo hii chama hiki kipya kilichoko madarakani, hakina mwelekeo, hakina itikadi, hakina maono ya mafanikio na kimebakia kama picha ya zamani iliyojawa na vumbi la ufisadi. Kimebakia kuwa chama cha kuangaliana, kukodoleana, kubezena, kutukanana, na sasa imefika mahali kuwa chama cha kusakamana!
Hakina tena hatamu za uongozi isipokuwa utamu; hakina kujitegemea bali kimebaki na kujimegea, hakina ujamaa tena bali kimebakia na utamaa! Ndiyo CCM hii siyo ile ile, zimebakia rangi za kijani, njano na nyeusi! Uongozi wake butu, mwelekeo wake hupo, na malengo yake yamebakia vitabuni!
Ndiyo, CCM haina uongozi tena unaoongoza, bali kinaongozwa na viiongozi wanaoongozwa na matukio! CCM hii haijui nchi yetu ni nchi ya mrengo gani na tunataka kujenga taifa la namna gani! SAsa hivi chini ya CCM hii ninachoshuhudia ni mambo kwenda mrama!
Taifa liko mashakani, hatima ya watu wetu matatani, na kwa hakika toka mbali kama kwenye ukungu hivi naweza kuona mahali ambapo ule unabii niliondika habari zake miaka mitatu uliyopita unazidi kutimia kwa haraka zaidi. Na wanaoutimiza ni wana CCM wenyewe!
CCM pole pole inaanza kusimamishwa kizimbani! Kizimba cha maoni na fikra za watu! Je itakutwa na hatia? Na ni nani anaiongoza! Je Kikwete ameishindwa?
Je, ipo haja ya haraka kwa Rais Kikwete kuitisha MKUTANO MAALUM WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA?
F. Kuweka utaratibu wa kuwa na serikali ya mseto.
N.k
Watu wa CHADEMA hawachoki kujadili CCM.
Na mwisho kumbukumbu yangu sio nzuri sana, ila ninachokumbuka yale maneno 'Tanzania ni nchi ya Kijamaa yaliwekwa mpaka kwenye katiba, hivyo ni above party politics. Kama yaliondolewa, then I support you CCM wayaondoe ili mzimu wa Baba wa Taifa uwashukie na lile neno lake la upinzani wa kweli litimie, na watu wapate altenative.
Mungu ibariki Tanzania.
- CCM haina kiongozi? Sasa tumeshindaje ubunge Mbeya bila ya kua na kiongozi? Eti huko upinzani mna viongozi? Nani Zitto na Lipumba? Au Mrema na Mtikila? Kwa viongozi kama hawa CCM tunahitaji viongozi? Wa nini hasa?
- Wakuu CCM tuko sawa, tunajua malumbano ya kidemokrasia huwa ni adimu sana kwetu Tanzania, kwa hiyo naona we are reading too much katika demokrasia inayoendelea sasa hivi ndani ya CCM.
- Tuna matatizo ya kuwa na baadhi ya viongozi wabovu na sasa malumbano haya ndio wmazo wa kuwafikia, regardless ya who is talking too much soon tutakaa chini na viongozi wabovu wataumbuliwa, kama vile tulivyomuumbua Mbunge wa wetu wa zamani Nyimbo, tunao utaratibu wa ku-deal na uovu ingwa tumekuwa very slow sometimes,
- Otherwise, we are just fine, sijui huko upande wa pili kuna nini hasa Sangara au Dowans? Wakuu tuongee alternative sio majungu majungu, maana wananchi sio wajinga tena, kwenye haya malumbano ukweli unajiweka kando na tunauona wazi and very clear, nani ni nani,
- Wa-Tanzania sio mabwege tena! Tusipojua kuheshimu vyama vya wengine vya siasa tutaheshimu vipi vya kwetu? Tusipojua kuheshimu viongozi wenzetu wa chama kimoja tutajiheshimu vipi sisi wenyewe na wananchi? Tusipoheshimu maagizo ya vyama vyetu vya siasa, tutaheshimu vipi maagizo ya wananchi na taifa lao?
We are all together int his boat, kusema CCM haina viongozi ni matusi kwetu wanachama wa CCM na it is unacceptable! Tunaweza kujadili matatizo ya vyama vyetu vya siasa yanajadilika, lakini sio matusi kama haya kwamba eti CCM hakuna kiongozi, tusichanganye heshima na uoga ni vitu viwili tofauti sana!
Respect!
Wazee wa sauti ya umeme FMEs!
Wazee wa Sauti ya Umeme FMEs! Respet mkuu na Taratiiiiiiiiiiibu ndiyo mwendo tunakaribia kufika.
Swali la Msingi ambalo hoja ya Mwanakijiji imejikita ni 'Nani anaiongoza CCM'?
Sidhani kama MMM alikuwa akimaanisha CCM haina Viongozi, ina Mwenyekiti, ina Katibu Mkuu, in Katibu Mwenezi ina Makamu Mwenyekiti na Viongozi wengine.
asante
2010 mkuu una kura yangu usinisahau kwenye ukurugenzi.....- CCM we are fine, kwa sababu hakuna upinzani, mpaka siku utakpopatikana upinzani wa kweli then CCM tutajirekebisha, not now kwa sababu ni clear kwamba sisi wananchi tumeshindwa kujenga upinzani, tunasubiri somebody aje atujengee huku tukilaumu tu bila kufanya anything serious, angalau hata Mrema asiyekuwa na elimu kubwa alijitahidi, sisi wenye elimu kubwa ndio haya!
- Wakuu tukazane tuingie wenyewe huko ndani, hakuna tena wa kutufanyia tukabadilishe wenyewe!
FMES!
Hoja hujibiwa kwa hojaWazee wa Sauti ya Umeme FMEs! Respet mkuu na Taratiiiiiiiiiiibu ndiyo mwendo tunakaribia kufika.
Swali la Msingi ambalo hoja ya Mwanakijiji imejikita ni 'Nani anaiongoza CCM'?
Sidhani kama MMM alikuwa akimaanisha CCM haina Viongozi, ina Mwenyekiti, ina Katibu Mkuu, in Katibu Mwenezi ina Makamu Mwenyekiti na Viongozi wengine.
asante
- Then angesema kwanza Upinzani unaongozwa na nani, alinganishe na CCM ili kuipa hoja nguvu ya kielimu, badala ya maneno ya mtaani. Kwa sababu CCM tunao viongozi wetu tuliowachagua tena kwa kura.
FMES!
CCM haina uongozi! kama hili ni tusi basi nalirudia kwa furaha. CCM haina uongozi kama iliyowahi kuwanao. sasa hivi wamebaki kuburuzana. Wapinzania na wenyewe wana matatizo yao na ya uongozi ni mojawapo tu. Hata hivyo, wapinzani hawanisumbui kichwa changu kwani hawaongozi nchi na hatima ya Taifa haiko mikononi mwao. CCM ndiyo wahusika wakuu.
CCM wamebakia kuwa na SIUONGOZI!
..CCM ukiwa mpinzani na wakijua ni tishio kwao,basi watatumia serikali yao ya kifisadi na vyombo vyake kukunyasa,kukusingizia kuanzia kodi mpaka uhaini na kukuweka ndani...yaani hakuna haki kabisa na hawa wapuuzi ndio maana nchi inazidi kuwa maskini tuu kila siku,dawa yao ni kuwamaliza mafisadi ndani ya chama chao na kukivunja vunja kama KANU,naanza kuamini upinzani wa kweli lazima uanzie ndani ya CCM au lazima wapinzani wawe na strategy za kukamata maeneo fulani kwanza kabla ya nchi nzima,najua wapinzani wakicheza kadi zao vizuri sehemu za Dar,Mwanza,Arusha,Mbeya,Kigoma na Mara CCM najua wanaweza kupigwa nje kirahisi sana