Nani anahusika na kutunza kumbukumbu na Historia ya Baba wa Taifa?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
22,454
Reaction score
32,980
1771013993516.png

NANI ANAHUSIKA NA KUTUNZA KUMBUKUMBU NA HISTORIA YA BABA WA TAIFA?

JIWE LA KUMBUKUMBU YA NYUMBA YA MTUMWA SULEIMAN ALIYOFIKIA MWALIMU NYERERE 1954

Mmoja kati ya wafuatiliaji wa Maktaba kanitumia picha ya jiwe linalotumika kama kumbukumbu kueleza nyumba ambayo alifikia Mwalimu Nyerere, Mtaa wa Livingstone, Ujiji wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kweli ndugu zangu hali ya jiwe hili linaakisi heshima ya Baba wa Taifa na pia heshima ya mzalendo Mtumwa Suleiman aliyempokea Mwalimu Nyerere?

Kwa nini hatuthamini historia hii tukufu ya kupigania uhuru na ya wapigania uhuru wa Tanganyika?
 
Yaan km kila alipofikia kungekua na Mawe basi nina uhakika kila Mkoa kungekua na Mawe mpaka vijijini ndani ndani ni mwendo wa Mawe tu, ila ni jambo jema kihistoria
 
Hujaelewa mantiki ya mada
Huko vijijini ndio alikoanzia maisha ya siasa?
Huyo mpumbavu nyerere alikuja na kaptura yake na tranka mjini, akapokelewa na kupewa sehemu ya kuishi na ndio hapo alipojiunga na harakati zilizoanzishwa kabla, halafu kapewa nchi aisimamie ikiwa na uchumi mkubwa kushinda nchi nyingi kama Malaysia na South Korea akaja kuharibu kila kitu kwa ujamaa na mfumo kristo.
 
Wewe huisemi China sasa hivi au NORTH KOREA, kwanini? Si wanaishi kiujamaa au?
 
China ni habari nyingine na North Korea hiyo inaenda kuanguka sio muda mrefu, njaa kali huko
Sasa Nyerere alicopy kwa rafiki yake Mao ZeDong, km ulikua haujui leo nimekujuza ujamaa China ile pale ila Tanzania alipojichanganya Nyerere ni alipoingia tamaa ya kukichukua kisiwa cha Pemba na Unguja hapo ndipo mchongo wa ujamaa ukaanza kwenda fyongo, China kamsubiria Taiwan mpaka amekua mkubwa sasa anapambana nae ukubwani kwamba wewe wa kwangu hata ufanyaje, huyo kiduku wa NK ni mtata
 
Yaan km kila alipofikia kungekua na Mawe basi nina uhakika kila Mkoa kungekua na Mawe mpaka vijijini ndani ndani ni mwendo wa Mawe tu, ila ni jambo jema kihistoria
Verbose,
Unahitaji kujua historia za nyumba hizi kwanza.

Hizi si nyumba ambayo utazikuta kila mahali kwa hiyo kutakuwa na mawe ya kumbukumbu kila mahali.

Tuanze na Dar es Salaam.

Mwalimu alikaa nyumbani kwa Abdul Sykes baada ya kuacha kazi ya ualimu.

Huwezi kupata nyumba kama hii yenye historia muhimu ya Mwalimu kama hii kiasi kuwe na ''mawe hadi vijijini.''

Mwalimu alikaa nyumba ya Sued Kagasheki Bukoba.
Mwalimu alikaa nyumba ya Bi. Halima Selengia Moshi.

Mwalimu alikaa nyumba ya Ahmed Adam Mikindani.

Mwalimu alikaa nyumba ya Bi Aza Kilwa.

Mwalimu alikaa nyumba ya Issa bin Ali Naliwanda Lindi.

Huu ulikuwa wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika na ukisikia historia za wenye nyumba hizi na mchango wao mwili utakusisimka.

Sasa kuna nyumba ambazo wana TANU walizitoa kuwa ofisi za TANU kama nyumba ya Suleiman Masudi Mnonji, Lindi, nyumba ya Nyange bint Chande Tabora, nyumba ya Aikaeli Mbowe Machame nk.

PICHA: Nyumba ya Ahmed Adam ndiyo nyumba aliyolala Mwalimu Nyerere safari yake ya kwanza Mikindani Southern Province mwaka wa 1956.

Mwalimu Nyerere Kilwa alikuwa akilala nyumba ya Mwinyi Mcheni Omar na alikuwa akipakiwa kwenye pikipiki ya Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar kuzunguka vijijini kuitangaza TANU.

Ofisi ya kwanza ya TANU Southern Province ilikuwa nyumbani kwa Suleiman Masudi Mnonji, Makonde Street.

"Hii nyumba inafanana na nyumba ya Bi. Aza binti Mabruki wa Kilwa Kivinje walipokuwa wakifikia viongozi pamoja na mzee Kawawa.

Upande wa pili wa barabara ilikuwepo nyumba ya mzee Said Ali Bungara.

Ukivuka barabara kulikuwa na shule ya Muslim.

Mwaka wa 1967 Mwalimu alipumzika hapo kwa bi Aza kisha akaja kuhutubia wananchi kwenye uwanja wa shule ya Muslim.

Hapo Kilwa alikuweko Sheikh Umar bin Khalfan kiongozi wa twarika ya Qadiria.

Nyumba yake ipo Mayungiyungi wakati wa ziara zake Mwalimu alikuwa akienda hapo kwa Sheikh kuonana na wazee wa Kilwa pamoja na kuombewa dua.

Miongoni mwa masheikh waliokuwepo Sheikh Hussein Shadhilly, Sheikh Yusuf Mussa, Sheikh Mcheni na wengineo."

Hii ni historia ndefu tusimame hapa.

1771017408178.png

1771017434038.png

1771017460771.png
 
Hujaelewa mantiki ya mada
Huko vijijini ndio alikoanzia maisha ya siasa?
Huyo mpumbavu nyerere alikuja na kaptura yake na tranka mjini, akapokelewa na kupewa sehemu ya kuishi na ndio hapo alipojiunga na harakati zilizoanzishwa kabla, halafu kapewa nchi aisimamie ikiwa na uchumi mkubwa kushinda nchi nyingi kama Malaysia na South Korea akaja kuharibu kila kitu kwa ujamaa na mfumo kristo.
Maamuzi ya mtu yawe judged katika mazingira ya wakati ule anapoyafanya, not in hindsight. Hakuna uamuzi ambao ni timeless nor is there a socio-economic system that will never fail.
 
Verbose,
Unahitaji kujua historia za nyumba hizi kwanza.
Hizi si nyumba ambayo utazikuta kila mahali kwa hiyo kutakuwa na mawe ya kumbukumbu kila mahali.

Tuanze na Dar es Salaam.

Mwalimu alikaa nyumbani kwa Abdul Sykes baada ya kuacha kazi ya ualimu.
Huwezi kupata nyumba kama hii yenye historia muhimu ya Mwalimu kama hii kiasi kuwe na ''mawe hadi vijijini.''

Mwalimu alikaa nyumba ya Sued Kagasheki Bukoba.
Mwalimu alikaa nyumba ya Bi. Halima Selengia Moshi.

Mwalimu alikaa nyumba ya Ahmed Adam Mikindani.
Mwalimu alikaa nyumba ya Bi Aza Kilwa.

Mwalimu alikaa nyumba ya Issa bin Ali Naliwanda Lindi.

Huu ulikuwa wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika na ukisikia historia za wenye nyumba hizi na mchango wao mwili utakusisimka.

Sasa kuna nyumba ambazo wana TANU walizitoa kuwa ofisi za TANU kama nyumba ya Suleiman Masudu Mnonji, Lindi, nyumba ya Nyange bint Chande Tabora, nyumba ya Aikaeli Mbowe Machame nk.

Hii ni historia ndefu tusimame hapa.
Kwa hiyo yeye hakuwa na kawaida ya kukaa kwenye nyumba za Wakristo au hii history inategemea dini ya narrator?
 
Maamuzi ya mtu yawe judged katika mazingira ya wakati ule anapoyafanya, not in hindsight. Hakuna uamuzi ambao ni timeless nor is there a socio-economic system that will never fail.
Hakuna kitu
Huyo ni chanzo cha matatizo ya leo, ambapo waliokuwepo hawataki kuondoka kwa kuwa yule mjinga aliwatengenezea mazingira ya umilele na dio katiba ya leo, na kutia hofu wananchi.
Atabeba lawama zote yeye.
 
Tusipende cheap excuses. Hatuna sababu ya kumlaumu Mwalimu kwa ukondoo wetu—he has been gone for more than quarter a century! Zipo nchi nyingi sana zilizokuwa na mfumo kama wetu, lakini zimebadilika na wakati. Zambia is one of them!

Hata Katiba yetu ya sasa tungekuwa na balls za kuilinda, tusingekuwa kwenye hii hali tuliyomo. Katiba yetu inasiginwa kila uchao, lakini tunaangalia tu. Kwa ujinga wetu huu, hata tukiandika Katiba nzuri kiasi gani, mambo hayatabadilika. Mazafakas wataisigina hiyo Katiba mpya na hakuna tutakachofanya!
 
View attachment 3543404

NANI ANAHUSIKA NA KUTUNZA KUMBUKUMBU NA HISTORIA YA BABA WA TAIFA?

JIWE LA KUMBUKUMBU YA NYUMBA YA MTUMWA SULEIMAN ALIYOFIKIA MWALIMU NYERERE 1954

Mmoja kati ya wafuatiliaji wa Maktaba kanitumia picha ya jiwe linalotumika kama kumbukumbu kueleza nyumba ambayo alifikia Mwalimu Nyerere, Mtaa wa Livingstone, Ujiji wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kweli ndugu zangu hali ya jiwe hili linaakisi heshima ya Baba wa Taifa na pia heshima ya mzalendo Mtumwa Suleiman aliyempokea Mwalimu Nyerere?

Kwa nini hatuthamini historia hii tukufu ya kupigania uhuru na ya wapigania uhuru wa Tanganyika?
Afadhali hakuna jina la Sykes leo
 
Afadhali hakuna jina la Sykes leo
Gwapole,
Jina la Sykes lipo.
Halikwepeki.

Kama ni kumbukumbu ya nyumba alizolala Mwalimu Nyerere Dar es Salaam nyumba ya kwanza alipofika na kulala ni ya Joseph Kasella Bantu Temeke Wailesi.

Kasella Bantu ndiye aliyempeleka Mwalimu kwa Abdul Sykes kumtambulisha 1952.

Mwalimu kama inavyojulikana alipoacha kazi alikuja kuishi nyumbani kwa Abdul Sykes.

Tabu kumkwepa Abdul Sykes katika maisha ya Baba wa Taifa.
 
Verbose,
Unahitaji kujua historia za nyumba hizi kwanza.

Hizi si nyumba ambayo utazikuta kila mahali kwa hiyo kutakuwa na mawe ya kumbukumbu kila mahali.

Tuanze na Dar es Salaam.

Mwalimu alikaa nyumbani kwa Abdul Sykes baada ya kuacha kazi ya ualimu.

Huwezi kupata nyumba kama hii yenye historia muhimu ya Mwalimu kama hii kiasi kuwe na ''mawe hadi vijijini.''

Mwalimu alikaa nyumba ya Sued Kagasheki Bukoba.
Mwalimu alikaa nyumba ya Bi. Halima Selengia Moshi.

Mwalimu alikaa nyumba ya Ahmed Adam Mikindani.

Mwalimu alikaa nyumba ya Bi Aza Kilwa.

Mwalimu alikaa nyumba ya Issa bin Ali Naliwanda Lindi.

Huu ulikuwa wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika na ukisikia historia za wenye nyumba hizi na mchango wao mwili utakusisimka.

Sasa kuna nyumba ambazo wana TANU walizitoa kuwa ofisi za TANU kama nyumba ya Suleiman Masudi Mnonji, Lindi, nyumba ya Nyange bint Chande Tabora, nyumba ya Aikaeli Mbowe Machame nk.

PICHA: Nyumba ya Ahmed Adam ndiyo nyumba aliyolala Mwalimu Nyerere safari yake ya kwanza Mikindani Southern Province mwaka wa 1956.

Mwalimu Nyerere Kilwa alikuwa akilala nyumba ya Mwinyi Mcheni Omar na alikuwa akipakiwa kwenye pikipiki ya Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar kuzunguka vijijini kuitangaza TANU.

Ofisi ya kwanza ya TANU Southern Province ilikuwa nyumbani kwa Suleiman Masudi Mnonji, Makonde Street.

"Hii nyumba inafanana na nyumba ya Bi. Aza binti Mabruki wa Kilwa Kivinje walipokuwa wakifikia viongozi pamoja na mzee Kawawa.

Upande wa pili wa barabara ilikuwepo nyumba ya mzee Said Ali Bungara.

Ukivuka barabara kulikuwa na shule ya Muslim.

Mwaka wa 1967 Mwalimu alipumzika hapo kwa bi Aza kisha akaja kuhutubia wananchi kwenye uwanja wa shule ya Muslim.

Hapo Kilwa alikuweko Sheikh Umar bin Khalfan kiongozi wa twarika ya Qadiria.

Nyumba yake ipo Mayungiyungi wakati wa ziara zake Mwalimu alikuwa akienda hapo kwa Sheikh kuonana na wazee wa Kilwa pamoja na kuombewa dua.

Miongoni mwa masheikh waliokuwepo Sheikh Hussein Shadhilly, Sheikh Yusuf Mussa, Sheikh Mcheni na wengineo."

Hii ni historia ndefu tusimame hapa.

View attachment 3543473
View attachment 3543474
View attachment 3543475
Kweli mkuu hapa sasa nimekuelewa vizuri kabisa,
 
Back
Top Bottom