Nani aliyemuumba Mungu?

Nani aliyemuumba Mungu?

Kwahiyo unapinga mungu ambaye yupo???!!, thats nonsense.

Katika huo mfano wako, Kumbuka pia kuna madaktari vilaza wasiojua taaluma yao na kujifanya wanajua huku upeo wa ufahamu wao umefikia mwisho.

Kumbuka sio kila kitu mtu anaweza kujua kwa akili yake binafsi bila kufundishwa na ndio maana kuna taaluma mbalimbali ikiwemo taaluma ya kumjua Mungu.

Jifunze kumjua mungu kwa watu wanaomjua na pia muombe huyo mungu kwa unyenyekevu ajidhihirishe kwako weka kiburi na majivuno yako kando kwani Mungu ni the Most supreme being, asiyehitaji chochote kutoka kwa yeyote na ni yeye aliyekupa hiyo akili kiduchu unayojivunia kumkufurisha.
Asante!
 
Sawa.

Hapa umetaja mambo mawili msingi katika hoja hii; hayo ni: sayansi na Mungu.

Jambo la tatu na la nne ni vipengee vya sayansi kama maarifa.

Kwahiyo, ili hoja hii iwe ya manufaa pia kuonyesha utimamu wetu; ni vema tujadili katika msingi wa taaluma yenyewe na sio hisia au hadithi.

Hivyo, basi, katika hoja hii tunalazimika kwanza kujibu maswali msingi haya, kwa kuzingatia maana inayokubalika na wanasayansi wengi; kwanza ni sayansi yenyewe.

1. Sayansi ni nini?

1a. Mantiki ni nini?

1b. Uthibitisho ni nini?

Na

2. Mungu ni nini?

Sasa, unakubali twende katika mwelekeo huu wa kitaaluma?
Karibu.
Nakubali.

Jibu vyote hivyo halafu utiririke kuthibitisha bila mkanganyiko wa kimantiki kwamba Mungu unayemsema yupo na si hadithi tupu tu.
 
Siyo kweli. Kwanza nilikwambia hakuna atakae taka ushahidi wa ndoto kama unaota au hauoti, sababu ndoto ni jambo halisi. Ni sawa na kutaka ushahidi wa Jua liko juu yako au chini yako ? Hili kila mtu mwenye macho analidiriki, na ni sawa na Ndoto.

Pili unaposema ulimwengu wa kiroho, ulimwengu huu una husisha ni na nini ?
Isome tena post yangu hiyo hapo juu inayo majibu ya swali lako hili ulilouliza hapa
 
The question: "If God is the creator, then who created the creator?" is illegitimate because by definition, the Creator is uncreated. He is eternal, without beginning, without end and all affairs return back to Him: (وَأَنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلْمُنتَهَىٰ) "And that to your Lord is the return (of all beings and affairs) (and of all perfections in attributes)." (53:42).

Thus to ask who or what created something that is uncreated is the way of:
a) an ignorant person devoid of intellect,
b) a lying deceiver, a sophist.

Note : Maelezo haya mafupi nime "copy" na ku "paste" toka kwenye tovuti iitwayo "www.aboutatheism.net", mnaweza tembelea huko mpate faida.

Tujadili hili, kwa wale wote ambao huuliza swali hilo, waje watuambie kwanini wanauliza swali hilo.

Ahsante.

Jurjani (Zurri)
Shida ni kwamba huyo Mungu mwenyewe wala haieleweki kama yupo kweli au ni stori tu zilizokuja baada ya sisi kushindwa kujua haswa asili yetu

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kuamini ni nini na kujua ni nini?

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Kuamini ni kuwa na maoni ya moyo yenye kufanya kuwa na mkabala fulani juu ya jambo au kitu. Na Kujua ni kufahamu kwa yakini bila ya shaka wala wasiwasi;kuwa na habari.
 
Chunguza vizuri mifano yako hapo utaona si rafiki kadiri ya maneno "kutibitisha" na "uthibitisho."

Naweza kusema, kimsingi kwamba hauko makini. Hivyo ni mtu usiyetaka kujifunza; mpingaji.

Sina mda wa kupingana na mtu mara nyingi natafuta sababu ya kujifunza kitu kwa mitazamo mipya

Ila sipendi watu wasumbufu kama wewe

Mimi nimesema hayo maneno yanamsingi mmoja

Sasa ni jukumu lako wewe unayeyaona katika utofauti kuyatolea maelezo na si kunilazimisha mimi tena ninayeyaona katika umoja niyaone katika utofauti_umeelewa.!
 
Jibu vyote hivyo halafu utiririke kuthibitisha bila mkanganyiko wa kimantiki kwamba Mungu unayemsema yupo na si hadithi tupu
Tuanze na maana. Kwanza maana ya sayansi:

Sayansi ni nini?

Sayansi ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli ambazo zimebainishwa hazijathibitishwa.

Kwahiyo, sayansi ni shughuli za kiakili na vitendo zinazojumuisha kujifunza mifumo ya miundo na tabia za maumbile na ulimwengu asilia kupitia uchunguzi na majaribio.

Mantiki ni nini?

Mantiki ni kile kinachosemwa; neno au wazo au kinachofundishwa.

Uthibitisho ni nini?

Uthibitisho ni alama inayowakilisha kweli za akili.

Na

Mungu ni nini?

Mungu ni uwepo wa hali ya juu yenye akili.

Unakubaliana na maana hizi?

Karibu!
 
Mimi nimesema hayo maneno yanamsingi mmoja
Nimekubali ulivyosema huko mwanzo kwamba meneno hayo (kuthibitisha na uthibitisho) mzizi wake ni mmoja. Lakini je, yanaeleza hali moja? Hilo ndio swali hapa.

Wakati huo huo, ukiwa unaandika kuwa makini na maneno yako; kwani yanakinzana.

Huwezi kujifunza mambo mapya wakati tayari umejenga msimamo wako.
 
Hata ukisema ulichambue kisarufi hilo neno 'uthibitisho' bado mzizi ni mmoja na neno 'kuthibitisha' ni viambishi tu vinaweza kukupa viashiria kwamba moja ni mchakato na nyengine ni ukamili wa huo mchakato
nilishajibu hapa
 
Tuanze na maana. Kwanza maana ya sayansi:

Sayansi ni nini?

Sayansi ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli ambazo zimebainishwa hazijathibitishwa.

Kwahiyo, sayansi ni shughuli za kiakili na vitendo zinazojumuisha kujifunza mifumo ya miundo na tabia za maumbile na ulimwengu asilia kupitia uchunguzi na majaribio.

Mantiki ni nini?

Mantiki ni kile kinachosemwa; neno au wazo au kinachofundishwa.

Uthibitisho ni nini?

Uthibitisho ni alama inayowakilisha kweli za akili.

Na

Mungu ni nini?

Mungu ni uwepo wa hali ya juu yenye akili.

Unakubaliana na maana hizi?

Karibu!

Katika definitions zako zote, naweza kukubaliana nandefinitionnya sayansi tu.

Tukianza na mantiki, mantiki si kile kinachosema, neno au wazo au kinachofundishwa tu.

Mtu anaweza kusema neno au wazo, akalifundisha, likawa bado halina mantiki.

Unaelewa hilo?
 
Kuamini ni kuwa na maoni ya moyo yenye kufanya kuwa na mkabala fulani juu ya jambo au kitu. Na Kujua ni kufahamu kwa yakini bila ya shaka wala wasiwasi;kuwa na habari.
You are wrong on both counts.

Moyo kazi yake kusukuma damu, hauhusiani na kuamini.

Na unaweza kufahamu kwa yakini bila shaka kwamba wewe ni Rais wa Tanzania, wakati wewe si Rais wa Tanzania, na hivyo, ukawa hujajua wewe ni nani.
 
Katika definitions zako zote, naweza kukubaliana nandefinitionnya sayansi tu.

Tukianza na mantiki, mantiki si kile kinachosema, neno au wazo au kinachofundishwa tu.

Mtu anaweza kusema neno au wazo, akalifundisha, likawa bado halina mantiki.

Unaelewa hilo?
Maana ya sayansi tumekubaliana.

Vizuri.

Turudi kwenye maana ya mantiki.

Umesema, nanukuu " mtu anaweza kusema neno au wazo, akalifundisha, likawa bado halina mantiki. Unaelewa hilo?"

Ndio, naelewa hilo.

Kwa sababu mantiki ni kipengee cha sayansi kinachoshughulika na kuthibitisha kile kinachosemwa, neno au wazo; au kinachofundishwa kama kinakubalika kiakili.

Hivyo ulichoandika nakubaliana nacho; kwani umefafanua maana ya mantiki niliyoileza hapo.
 
Maana uliyoiandika ya mantiki ilikuwa batili.

Unakubali hilo?
 
You are wrong on both counts.

Moyo kazi yake kusukuma damu, hauhusiani na kuamini.

Na unaweza kufahamu kwa yakini bila shaka kwamba wewe ni Rais wa Tanzania, wakati wewe si Rais wa Tanzania, na hivyo, ukawa hujajua wewe ni nani.
Sawa,haya eleza mahusiano ya kujua na uthibitisho?
 
Kwa nini?
Kwa sababu umekuwa ukihusisha kujua na uthibitisho,kwamba ili useme jambo fulani najua basi lazima uweze kuthibitisha.

Ndio nataka kujua kuna mahusiano gani ya kujua na uthibitisho?
 
Kwa sababu umekuwa ukihusisha kujua na uthibitisho,kwamba ili useme jambo fulani najua basi lazima uweze kuthibitisha.

Ndio nataka kujua kuna mahusiano gani ya kujua na uthibitisho?
Wapi nimehusisha kujua na uthibitisho?

Unaweza kunipa mfano hai kutokana na maandiahi yangu mwenyewe nilipohusisha kujua na uthibitisho?

Kujua ni nini? Uthibitisho ni nini?

Kuhusisha kujua na uthibitisho ni nini?

Unajuaje unajua na si kwamba unafikiri tu unajua?

Unajuaje uthibitisho wako ninsahihi na si kwambabunafikiri tu ni sahihi?

Unajuaje usahihi, njw ya muktadha maalum finyu, ni kitu kilichopo kweli na si njozi inayotokana na upotofu uliojengwa katika fikra zetu dhaifu tu?
 
"Ukiweza kuthibitisha, umeondoka kwenye kuamini, uthibitisho wako unasema kwamba wewe unajua."

Maelezo yako hayo yamehusisha kujua na uthibitisho,kwamba uthibitisho ndio unafanya useme unajua bila uthibitisho inabaki imani tu hivyo kwenye imani hakuna kujua.
 
Back
Top Bottom